Mzee mmoja alikuwa haudhurii misiba leo kafariki, kinachoendelea hapa naona ni msiba wa familia tu

Mzee mmoja alikuwa haudhurii misiba leo kafariki, kinachoendelea hapa naona ni msiba wa familia tu

Kuna haja yakuanzisha Kampuni za kufanya mazishi, ili tuache haya mambo ya ujamaa jamaa, Ukifa hata watu wawili wanakuzika tu, lamsingi uzikwe na kulingana na dini yako uliyokuwa unaadudu.

Haya mambo ya nzengo sijui kujuana Juana ni issue za kimasikini wakati mwingine.
Sahihi
 
Mleta mada namfananisha na wapumbavu fulani wanasemaga usiposhiriki jumuiya, kanisani na kutoa zaka hatuji kukuzika 🤣🤣🤣

Yani wanajiona wajanja sana kumbe kumbe wangejua ninavyowadharau wasingeamini

Hata mimi huwa siwaelewi kabisa.
Wako mwilini wakati wote wakati Mungu ni roho.
Wanatumia hiyo kama fimbo Eti kutishia watu.
Imagine 🤔🤔🤔
niliwahi kushauri hizo jumuia zifanyike makanisani,
Kwanini muwe mnaenda kwenye nyumba za watu ?
Hamuoni ni risks kubwa ?
Kuna watu wanavamia na kuibiwa sababu wezi walikuja jumuia wakachora ramami za vita, wakaja kuwafanyia ujambazi.
Makongo hapo.
Yani bongo kuna mambo ya kijima sana.
Kwanini mtake kwenda kwenye nyumba za Watu.
Life is about privacy.
Kwanza wengine wachawi wakubwa .
Wengine umbea tu na kutaka kuwathaminisha.
Wengi Hawana Mungu moyoni.
 
Ndio maana kuna umuhimu wa kuwepo na yale makampuni ya mazishi hata huku Tanzania.

Jamaa wanahandle kila kitu hadi mourners (watakaolia msibani)
Makampuni yapo ingawa sio kwa wingi. Tatizo la waafrika ni ngumu sana kufata huo utaratibu, tunapenda kujikusanya na kusaidiana mwisho wa siku hakuna lolote michangp hakuna na majungu hayakosekani
 
Kuna jamaa tulimaliza nae shule na darasa moja akafariki. Nikaleta hoja kwenye kundi la shule tusaidie mchango jamaa hela ipatikane asafirishwe. Mtu anajibu alikuwa hachangii misiba ya wenzake, hahahanikajua ukichaa ni real duniani. Sasa usipochangia akazikwa unamkoa yeye au nyie mliobaki
Kujamiiana ni kitu cha muhimu
 
Mzee mmoja amefariki na M/Mungu alimjaalia kweli enzi za uhai wake mali kweli kweli za kutosha, katika kujumuika na nzengo Mzee hakuwa na historia ya kuhudhuria misiba ya wengine na hata kushiriki tu hakuwa anafanya hivyo enzi za uhai wake kabisa na hakuwa anajali.

Sasa ya Mungu mengi bwana leo yeye ndio amefariki toka Jumatatu. Nyumbani kwake pamewekwa maturubai na ratiba ya mazishi ila hakuna watu.

Bahati mbaya hata watoto wake mke pia walimuiga tabia. Wapo wenyewe na ndugu majirani hakuna hata mmoja na watu hawana habari napo ni kama vile hakuna kitu vinaendelea pale kila mtu anaendelea na mambo yake.

Hii stori inakuja kufanana kidogo sana na hii yangu ambayo niliishugudia.

Hii imenikumbusha mwaka 2019 nilihudhuria msiba wa babu huko Musoma kijijini cha Nyabange Wilaya ya Butiama. Nzengo walikuja kama kawaida wakashughulika kila kitu wakaandaa, lilipofika suala la kula kile chakula wakaitana baadae nikaona kila mtu anaenda kwake, kila kitu walicho andaa walikiacha kama kilivyo tukabakia ndugu tu.

Wakasema, mjomba ambae ndio msiba ulikuwa umepangwa hakuwa anakula kwenye misiba na yeye alikuwa anachangia tu. Na mke wake alikuwa anakuja kupika na kuondoka kula hawali wala hawakai kwenye msiba wa nzengo. Waligoma kabisa, sasa chakula walichokuwa wameandaa nikama sisi ndugu tusingekimaliza hata kama tungekula siku 2 bado kingebaki kingi tu. Ikabidi ndugu waitane na wakaongee na wazee mjomba akapigwa faini ya mbuzi ndio wakaja kushiriki.

Toka hapo mjomba hajawahi kuacha kuhudhuria misiba anakwambia nilichokiona sikuile ni fedheha hata kama unauwezo ile ni mbaya sana.
Kuhudhuria MISIBA ni Upumbavu.
 
Makampuni yapo ingawa sio kwa wingi. Tatizo la waafrika ni ngumu sana kufata huo utaratibu, tunapenda kujikusanya na kusaidiana mwisho wa siku hakuna lolote michangp hakuna na majungu hayakosekani
Wazee wa 'vishughuli'
 
Halafu umajuaje kuwa haendagi kwenye misiba ya wengine ?
Je mnakuwaga 24/7 kwenye kila msiba kutambua wanaokuja ??
What if mmekuwa mkipishana labda yeye akiwepo wewe unakuwa haupo ??
Mbona waswahili mmezidi kwa nongwa jamani ?!
Hebu tupendane jamani tuache kuhusudiana na kuumana.
 
Bado mpo na uzamani ukishakufa what matters is kufukiwa hayo mengine sijui nani alikuja msibani ni nonsense tu
 
g
Ndo huu ujinga naupinga mia kwa mia,
wakati unakuta mtu wa kijijini kwenu akiumwa akapangiwa hospitali tuseme muhimbili,unapigiwa simu.
anafikia kwako,unamhudumia na pengine huko mhimbili hapajui unampeleka n.k
ila ukifa ukapelekwa maiti,wanavuta midomo kwamba huwa huji kuwazika.
Inafikirisha sana mkuu, huwa tunasahau wema wa mtu upesi sana.
Kifo tuliadhibiwa kisawasawa
 
Ndio ujinga pia wa wengi kwenye ma-group ya Whasap ya michango Sijui rambirambi na kupangiana kiwango.
Kwani maana ya rambirambi ni nini ?
Je ni Kwanini sasa ulazimishe kiwango Eti kisipungue kiasi fulani ??!
Don’t follow the crowd follow the right way
 
Ila ni sawa tu maana wasioenda wamewapunguzia gharama wafiwa. Kama familia inajiweza kiasi hapo ni kununua tu jeneza, wakodi watu wachache wa kusaidia kuzika makaburini, siku imeisha.
Huwa tunacomplicate sana misiba
Uko sahihi sana mkuu
 
Afrika ni ujinga ni kama kikojozi na kopp la mkojo,
Bakhera au Modewji hauudhirii mazishi lakini leo hii akifa watu watajazana zaidi ya kariakoo.
 
Ila ni sawa tu maana wasioenda wamewapunguzia gharama wafiwa. Kama familia inajiweza kiasi hapo ni kununua tu jeneza, wakodi watu wachache wa kusaidia kuzika makaburini, siku imeisha.
Huwa tunacomplicate sana misiba
Ndugu hayajakukuta
 
Back
Top Bottom