Mzee Mwinyi asimulia alivyopotea Ulaya alipokuwa mwanafunzi; mzungu akataa kugusa hela yale isipokuwa kwa ncha ya penseli

Mzee Mwinyi asimulia alivyopotea Ulaya alipokuwa mwanafunzi; mzungu akataa kugusa hela yale isipokuwa kwa ncha ya penseli

Hicho kitabu cha Mwinyi inaonekana kimejaa SOGA za kwenye GAHAWA tu.

Bora hata Mkapa aligusia masuala ya Tume huru, Demokrasia na kukiri mauaji ya Pemba.
 
Rais mstaafu wa DRC, Joseph Kabila, naye alishushwa kwenye basi huko Mbeya kwa kuwa hakuwa na nauli ya kutosha. Huo ulikuwa wakati wa hayati Mobutu na wakina Kabila walikuwa wakimbizi hapa Tanzania. Baadaye Kabila akaja kuwa Rais wa DRC.
Ha! Hii itakua ni template inayofuatwa na waandishi wote wa vitabu, sio? JK naye atasema alikosa nauli kwanye basi la Mkaramo akasaidiwa na mzee fulani 🤣
Ni kama inspirational speakers, wote wana "rag to riches stories"
 
Yule mkata tiketi asingeamini kama angeambiwa baadae kuwa "yule uliyemkatalia kisa hana nauli itoshayo ndiye Rais wa JMT".

Ama kweli USIONE UKADHANI
Wala asingebabaika maana haoni kama Tanzania ni nchi ya maana.
 
Rais wa JMT mzungu wala asingejali na hamhusu. Yeye dharau zile tu zilimtosha
Hata wananchi wanataka kujua mambo muhimu kama Loliondo kumilikishwa kwa waarabu miaka 99 under Mwinyi's watch.

Simulizi za kupotea London awasimulie wake zake na wajukuu.

My hope is JK atapoandika kitabu chake atatujuza yale mapesa ya escrow tuliyoambiwa yalisombwa kwa magari ya Ikulu alikuwa anapelekewa nani.
 
Katika kitabu chake cha 'Mzee Rukhsa, Safari ya Maisha Yangu', Mwinyi anasema siku hiyo alikuwa anarejea Newcastle kutoka London alikokwenda kwa ajili ya likizo ya chuo.

Anabainisha kuwa kipindi hicho alikuwa anaishi kwenye nyumba iliyokuwa inamilikiwa na Kanisa la Methodist, ikipokea wageni kutoka sehemu mbalimbali wakiwamo wanafunzi kutoka makoloni ya Uingereza.

Mwinyi anasema balaa lilianzia kituo cha treni alikokuwa kwenye foleni ndefu ya kukata tiketi pasi na kujua kwamba hakuwa na nauli kamili.

"Ilipofika zamu yangu nikatoa kiasi kilekile cha fedha kama nilizokatia tiketi wakati wa kuja London kutoka Newcastle, muuza tiketi akaniambia ‘wewe husomi magazeti? Imetangazwa katika redio na kuandikwa magazetini kuwa nauli za treni zimepanda.

“Kusikia vile nikashtuka, nikatoa mfukoni mwangu pesa zote nilizokuwa nazo noti na sarafu nikamkabidhi, yule mzungu akaziangalia fedha zangu kwa dharau akachukua penseli aliyokuwa ameipachika kwenye sikio lake na kutumia ncha yake kuhesabia fedha nilizoweka mbele yake," anasimulia.

Anasema baada ya kuambiwa kuwa nauli yake haitoshi, aliamua kukata tiketi ya kuishia katika Mji wa Darlington badala ya Newcastle, ili baadaye maili 31 (Km 50) atatembea kwa miguu baada ya juhudi zake za kumshawishi mkatisha tiketi kumsamehe shilingi moja iliyokuwa imepelea kwenye nauli yake kugonga mwamba.

Hata hivyo, Mwinyi anasema alijitokeza mzungu aliyejitolea kumwongezea shilingi moja na hivyo kufanikiwa kusafiri hadi Newcastle kama alivyotarajia lakini anasema haukuwa mwisho wa matatizo yake kwa kuwa baada ya kufika huko Newcastle alipotea alipoamua kupita njia ya mkato badala ya kufuata barabara kubwa.

"Baada ya kuhangaika kwa muda, nikakutana na bwana mmoja nikamuuliza njia ya kunifikisha Methodisdt International House. Akaniambia tuongozane maana ya yeye anakwenda huko," anasimulia.

Mwinyi anasema raia huyo mwema alimsindikiza hadi karibu na nyumba hiyo na kuhakikisha kuwa ameiona na yeye kurejea alipotoka jambo ambalo anasema aliliona ni la kiungwana na akabaini mzungu huyo hakuwa mkazi wa eneo hilo bali aliamua kumpeleka tu.

Chanzo: Nipashe



ilipelea shilingi moja au pound moja

au umetumia neno "shilingi " kama
kivumishi tu
 
Back
Top Bottom