Mzee Mwinyi katika hili la kuongeza muda wa Asante kwa Rais Magufuli hapana, tunakukatalia kwa nguvu zetu zote

Mzee Mwinyi katika hili la kuongeza muda wa Asante kwa Rais Magufuli hapana, tunakukatalia kwa nguvu zetu zote

Mzee wetu mzee Mwinyi, Shikamoo

Mimi ni mtanzania, kwa umri niseme labda ni mjukuu wako, ni Mtanzania, naipenda nchi yangu na ningependa iwe na mustakbali mwema.

Mzee wetu nimekusikia mara kadhaa ukieleza hamu yako ya kumuona rais aliyeko madarakani akiongezewa muda wa kutawala kinyume cha katiba ya sasa inavyotaka.

Mzee wetu, mimi kama mtu mzalendo, mwenye uchungu na nchi hii, nimeitafakari kauli yako, hapo mwanzo nilitaka niiache kama ilivyo lakini nikaona nitakuwa sijaitendea haki nchi yangu kama nitaiacha hilo suala lipite hivihivi bila kulizungumzia, hususan baada ya kuona kuwa hilo suala linaweza kuwa sumu ya amani ya nchi yetu na mustakbali wake, Mheshimiwa rais mstaafu baba yetu mzee Mwinyi hebu tusemezane katika haya yafuatayo kuhusu suala hilo:

1. Je ni nini lengo la kuweka ukomo wa utawala katika katiba?

Mzee Mwinyi bila shaka ulikuwepo wakati Baba yetu wa Taifa alivyoongoza Taifa letu katika mchakato wa mabadiriko ya katiba yaliyohakikisha kuwa tunaweka ukomo wa madaraka katika katiba mwaka 1984, Kwa hakika Baada ya vuguvugu la wananchi katika Afrika kutaka kubadiri serikali zao kwa njia amani na iliposhindikana kujaribu kutumia nguvu za kijeshi, busara ilimuingia raisi wetu wa wakati huo baba wa Taifa letu mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuwa ipo haja na ulazima wa kuweka Transition ya amani ya madaraka kutoka generation moja kwenda nyingine. Na hii ilifuatia majaribio kadhaa ya mapinduzi dhidi yake.

Mzee wetu mzee Mwinyi unataka kuturudisha kwenye utaratibu wa utawala wa maisha?. Je mzee wetu unadhani tukimruhusu rais wa sasa aendelee kutawala tutaweza kweli kuwazuia na marais wajao kuendelea kutawala kwa kisingizio kuwa wanafanya kazi vizuri?, Je mzee wetu unataka kuwaandalia mazingira Watanzania utaratibu wa kufanya machafuko ili kumtoa rais ambaye watadhani hawafai, raisi ambaye atakuwa anatawala kwa katiba inayomruhusu kutawala bila ukomo?

Mzee wetu usidhani ukibadili katiba kwa ajili ya Magufuli, hiyo katiba itaishia kwa Magufuli tu, hata Magufuli baada ya kutawala tani yake akaamua kubadili katiba tena na kurudisha utaratibu wa zamani, atakayemfuata naye anaweza kuibadili tena naye akatawala tani yake!. Mzee wetu hayo ndiyo unayoyataka?

2. Mzee wetu, kumbuka Msisitizo wa Baba wa Taida kukutaka usibadili ukomo wa kutawala

Mzee wetu, mwaka 1999 pale uwanja wa Taifa kwenye msiba wa mwalimu, ulikuwa miongoni mwa watu waliopewa nafasi ya kumzungumzia Mwalimu, ulieleza mambo mengi, ulieleza jinsi alivyokuwa Mlima wa fikra na uongozi n. k na uliahidi kulinda yale mazuri yote aliyotuachia. Sasa mzee wetu mzee Mwinyi, hata hili la ukomo wa madaraka nalo unaliwekea question mark?. bado una chembe ya shaka juu ya umuhimu wake?

Mzee wetu mzee Mwinyi labda nikukumbushe tu namna mwalimu alivyotueleza wazi Watanzania kuwa wakati wa utawala wako, walikuwepo watu na harakati za kukutaka wewe ubadili katiba ili uendelee kutawala baada ya miaka kumi, Mwalimu alielezea jinsi alivyokuwa concerned na suala hilo na akatueleza kuwa jinsi wewe binafsi ulivyomhakikishia kuwa huna nia hiyo.

Sasa mzee wetu mzee Mwinyi, unadhani Mwalimu hakupenda usiendelee kutawala kwa sababu alidhani wewe hufai au alidhani kuwa wazo hilo siyo jema kwa mustakbali mpana wa nchi yetu?. Je Mzee wetu mzee Mwinyi, mbona basi na wewe unakuwa kama wale watu waliokuwa wanasukumasukuma mambo ili wewe uendelee kutawala kinyume cha ukomo wa vipindi kipindi cha utawala wako?.

Au mzee wetu mzee Mwinyi wakati ule ulikubaliana kishingo upande na mwalimu lakini wewe binafsi siyo muumini wa ukomo wa vipindi vya utawala?

3. Mzee wetu Mzee Mwinyi, Je una maslahi binafsi na utawala wa Magufuli?

Jana kwenye mkutano mkuu, Raisi Magufuli alituibia siri kuwa mwaka 2015 alikuwa yeye binafsi amempendekeza mwanao Hussein Mwinyi ili awe mgombea mwenza, Pia Mwanao Hussein Mwinyi amepata nafasi ya kuwa Mgombea wa CCM kwa tiketi ya Uraisi Zanzibar katika kipindi hiki ambapo Magufuli ni rais.

Sasa sisi tunajiuliza, hivi je mzee wetu unataka kulipa Shukrani kwa Magufuli kwa kumfanyia makubwa mwanao?, Je una maslahi binafsi yanayokusukuma kutaka Magufuli aendelee kuwa raisi, Je unamuandalia njia njema zaidi Mwanao kwa kutaka tuendelee na kile ambacho waswahili walisema kwenye methali "Zimwi likujualo"?

4. Mzee wetu, Mzee Mwinyi kumbuka hotuba ya baba wa Taifa kuhusu Nyufa zilizoikumba nchi yetu

Kabla ya uchaguzi wa mwaka 1995, baba yetu wa Taifa alizungumza nyufa mbalimbali ambazo zilianza kuikumba nchi yetu, na miongoni mwa mambo aliyoyasema ni suala la kutoheshimu katiba.

Mzee wetu mzee Mwinyi, mimi binafsi nilisikitishwa sana kusikia ukisema, Katiba tuiweke pembeni ili tumpe tena Rais wa Sasa miaka mitano kama Ahsante. Mzee wetu hata kama Rais Magufuli angeleta maendeleo ya namna gani, Je unataka tutoe ahsante kwa mtu aliyetimiza wajibu wake tuliomtuma afanye kupitia kuvunja katiba?. Mzee wetu mzee Mwinyi, wewe si uliapa kulinda katiba, Mwenzio naye si aliapa kulinda katiba, Sasa unamshawishi avunje katiba?

5. Mzee Mwinyi, Ushauri wako haujengi, ni mbaya na unatuma meseji mbaya kwa vizazi vijavyo

Mzee wetu mzee Mwinyi, wewe ni mtu mkubwa sana, wewe ni role model wa wengi, fahamu kwamba kauli zako zinawekwa kwenye rekodi na huenda zikawa rejea vizazi na vizazi hata miaka maelfu ijayo. Kauli za "huba" unazozitoa juu ya mtawala wa sasa hata kutaka katiba ipindishwe kwa ajili yake, wapo watu watakaokuja huko mbeleni watazitumia kama rejea ili kufanya hayahaya ambayo unatamani Taifa lifanye kwa ajili ya Magufuli, Watasema mbona miaka 50 iliyopita Rais wa awamu ya pili alitaka rais wa awamu ya tano naye aendelee kutawala?, basi kwa nini na sisi tusifanye?. Kwa kweli mzee wetu katika hili hauko sahihi kabisa, haujalitendea haki Taifa kabisa

Hitimisho
Ni dhahiri ushauri wa mzee wetu mzee Mwinyi ni ushauri mbaya kabisa kwa Taifa letu, ni ushauri usiozingatia hekima bora kabisa ya baba wa Taifa letu mwalimu Nyerere aliyeamua kuingiza ukomo wa utawala kwenye katiba, kitu ambacho leo hii tunajivunia Taifa letu kubadirishana uongozi kwa amani.

Mzee wetu Mzee Mwinyi akumbuke tu, Wakati mwalimu Nyerere anamuachia kijiti hapo mwaka 1985,Mwalimu alikuwa ni "kijana" kabisa wa miaka 63, pamoja na hali ngumu ya uchumi tuliyokuwa nayo wakati huo, Mwalimu alikuwa na uwezo wa kwenda kwenye uchaguzi na bado akashinda kwa kishindo, lakini aliona busara pana ni kung'atuka na kumuachia mtu mwingine kijiti.

Sasa swali la kujiuliza ni hili, kama Mwalimu asingeng'atuka mwaka 1985 yeye angekuwa rais?, Mkapa asingeheshimu mihula ya utawala Kikwete angekuwa rais?, Kikwete asingeheshimu katiba juu ya mihula ya Utawala Je Magufuli angekuwa rais?. Tunamuomba Mzee wetu alifikirie sana suala hili

Ama kuhusu Ahsante anayotaka tumpe Magufuli, Kama kuna ahsante yoyote ya kutoa kwa mtawala basi Watanzania wangetoa ahsante kwa mwalimu Nyerere kwa kuwaletea uhuru. Hakuna kitu kikubwa kilichofanywa katika nchi hii kuliko uhuru wetu. Lakini wananchi hawakuona eti wamfanye Mwalimu mfalme kisa katuletea uhuru.

Kama ni ahsante kwa sababu mtawala kaitendea jema familia, hata Mwalimu alikuwa na watoto pia akina madaraka Nyerere, Makongoro Nyerere, Rose Nyerere, lakini baba yetu wa Taifa hajawahi kuwa nice kwa mtawala teyote aliyekuja baadae ili watoto wake watendewe mema.

Mwisho kabisa nimpongeze katibu mkuu wa CCM ndugu, Bashiru Ally kwa kuzungumza wazi kupitia mahojiano na Tido Mhando kuwa suala la kubadili katiba ili kuongeza mihula ya utawala halimo katika ajenda ya CCM na si sera ya chama hicho na kwamba likiibuka CCM watalikataa. Mimi nasema hiyo ni busara kubwa sana

Pia nimshukuru rais Magufuli Mwenyewe ambaye yeye Mwenyewe kwenye mkutano mkuu alionyesha kutokubaliana na wazo hilo la mzee Mwinyi waziwazi, na ambaye mara kadhaa ameongea na kusema kuwa hana mpango huo

Mwisho kabisa ningependa Watanzania wote tulikatae wazo hilo la mzee Mwinyi, ni wazo baya, si jema kwa nchi yetu na halina mustakbali mwema kwetu na vizazi vyetu
Haka kadingi ni kafisadi ndo maana wakati wa urais wake ikulu iligeuka pango la walanguzi hata mwalimu Nyerere akakemea,sikushangaa hata yule kijana alipokatandika kofi msikitini.Wakati umefika Mwinyi apuuzwe na asipewe fursa ya kuhutubia umma.
 
Bahati nzuri hata Mh Rais kashasisitiza mara nyingi kuwa ataheshimu katiba
Atalitumia bunge kuweka kipengere cha kufuta ukomo wa urais wa vipindi viwili kwenye katiba kisha atasema anaheshimu katiba.Hayo aliyafanya Louis Napoleon ( Napoleon iii) wa Ufaransa mwaka 1852.
 
Kheee mnadhani Jiwe ndio alimchagua acheni propaganda huyo kachaguliwa na wazanzibar wenyewe kuingia tano bora. Kimsingi wote walio wachafua tano bora walikuwa na equal chances of being selected.kule dodoma walikuwa wa natafuta tu mshindi mmoja tu
Mwinyi kachaguliwa na kura za Wabara wenzake,Zanzibar hawajamchagua,angalia Nahodha kura 16,yule mwingine 19 jumla 35.
 
Huyu mzee alipoteza akili tangu alipozabwa kibao msikitini
 
Watu walimwekea sumu mangula wakamwacha huyu mfyuuuuu
 
Angalau huyu mzee mwinyi tunaeza sema amezeeka, akili imeisha na tukapuuza kabisa kauli zake.

Kuna watu wengine wenye wazo hili la kubadili Katiba ili kuongezea jpm muda wa kutawala, mfano ndugai, juma ngamia, kessy, nk, Hawa wachumia tumbo ni hatari sana kwa mustakabali wa taifa hili
 
Mimi pia awali nilifikiria sana umuhimu wa kubadilisha katiba angalau kwa mazingira maalum ya Rais Magufuri kwa kazi ya kipekee na nzito aliyoifanya kwa muda mfupi na matokeo makubwa kuonekana. Maeneo yaliyonishawishi zaidi kuwa Rais anastahili kuongezwa angalau miaka 5 au 10 baada ya muda wake ni kupiga vita rushwa, ubadhirifu, na ufisadi ambao nchi nyingi za Afrika zimeshindwa. Pili uwezo wake wa uongozi na maono, tatu utekelezaji wa mipango ya maendeleo kwa kasi kubwa na kwa maslahi ya taifa na mipango kadhaa ya kiuchumi ambayo ni ya kihistoria mf Stiglers umeme, Kuhamia Dodoma , Ujenzi wa fly overs, REA. Na hatimaye kuingiza uchumi wa kati.Pamoja na changamoto alizopata za utekelezaji amesukumwa mno na utashi binafsi wa kisiasa. Siyo kitu rahisi kupata Rais mwingine wa aina hii tutakapokosea huko mbele baada ya muda wake kuisha itakuja kuwa majuto ni mjukuu. Pengine hata Mwalimu Nyerere angekuwa hai angeshauri aongezwe muda Rais wa sasa -who knows -kwa vile yule mzee alikuwa Pragmatist na mwenye maono ya mbali.Hivyo kama nchi kadhaa zilivyofanya mf China, Urusi kwa maslahi ya nchi zao zimebadilisha katiba zao na kuongeza muda wa maraisi sisi ni nani. Ni kweli Katiba siyo msahafu au biblia kwa hili la eneo la muda wa kuongoza linaweza kufanyika kwa KURA YA MAONI ya wananchi ambao ndiyo wenye nchi kuamua na kwa sababu maalum ya kimaslahi ya taifa. Iwapo hoja hii itashindikana basi maandalizi makubwa ya kuweka succession plan yafanywe kwa kumtambua mtu makini atayeingia viatu vya magufuri au katiba isukwe upya kulinda mafanikio yaliyopatikana na mifumo thabiti iwekwe kipindi hiki kutupeleka mbele.Nchi kama Marekani imeweza kuendelea na mfumo wa vipindi vya miaka miwili kutokana na mifumo yake imara na sera za kitaifa ambazo hazibadilishwi kwa upepo wa Rais. Hii inaweza kuwa option 2. Tunashauri Usalama wa Taifa waanze kazi ya kufanya utafiti na upekuzi maalum na wa kina hali itakavyokuwa baada ya Magufuri na nani mzalendo atatuvusha huko mbelena bila kusahau optios mbalimbali.Tukishindwa kuwa na Open program basi nakubaliana na wanaosema aongezwe muda huyu aliyepo baada ya miaka yake 10 Uongozi wa nchi haujaribiwi.
Umeanza vibaya lakini umemaliza vizuri. Kipindi hiki anachomalizia Magufuli anatakiwa atuoneshe kama yeye pia ni mwalimu kwa kufundisha na kuwaandaa vijana kufuata nyayo zake nzuri. Aandae watu wasio na tamaa, waadilifu, wanaopiga vita rushwa, wachapa kazi, wasio na makundi, wenye kujiamini na wenye kuipenda nchi yao. Sio wanafiki. Magufuli amefanya kazi kubwa na mfano wa kuigwa, baada ya miaka kumi anahitaji kupumzika na kula matunda ya yale aliyoyafanyia kazi kimaendeleo kama walivyofanya watangulizi wake.
 
Back
Top Bottom