Mzee Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Hayati Magufuli, walisifiwa, walikosolewa! Haki ya kusifu/kupongeza iende sambamba na haki ya kukosoa!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa huja na makala zangu za " Kwa Maslahi ya Taifa". Makala ya leo ni kuhusu moja ya haki muhimu sana ndani ya katiba, kwenye Ibara ya 18, iitwayo haki ya uhuru wa kutoa maoni, "freedom of expression" ni haki inayotolewa na katiba yetu lakini kufuatia kushambuliwa kila kona kwa Dr. Bashiru, kutokana na kutoa nawazo yake ya ukosoaji, naona kuna watu wanataka kuingilia haki hii muhimu na kujimilikisha wao kwa kuingilia uhuru wa maoni wa watu wengine na hata kuwapangia ni maoni gani watoe!. Yaani wenye haki ni wanaosifu tuu na kupongeza, lakini ukikosoa, inakuwa nongwa kama anavyoshukiwa Dr. Bashiru!

Kwa vile wengi humu ni madogo, sisi kaka zenu tuna wajibu wa kuwaelimisha ya nyuma, toka enzi za Mzee Rukhsa, Ben, JK na JPM, wote walisifiwa na walikosolewa!. Ile haki ya Freedom of Expression provided na katiba yetu, yenye haki ya kusifu na kupongeza, inapaswa kwenda sambamba na haki ya kukosoa!. Hivyo kuna watu wanataka haki ya Mama ni asifiwe tuu na apongezwe tuu, lakini akikosolewa ni kosa, ni dhambi!.

Naomba tukumbushane tuu uhuru wa kutoa maoni yaani freedom of expression ni haki ya maoni huru ya kila mtu, wa kusifu na kupongeza wawe huru na wa kukosoa pia wawe huru, haki yao iheshimiwe, mtu akitoa mawazo yake kuhusu jambo lolote, hata kama hukubaliani nalo, mawazo yake yaheshimiwe!.

Bandiko hili ni kufuatia ukosoaji uliofanywa na Dr. Bashiru, watu wanamshukia kila kona, utadhani amemkufuru Mungu!, kumbe ni ametoa tuu mawazo yake na maoni yake, hata kama haukubaliani naye, heshimu mawazo yake, kama unatofautiana, pangua hoja zake, hoja kwa hoja na sio kwa viroja vya kumshambulia yeye binafsi. Hoja zake zijibiwe au zipingwe kwa hoja!

Ukimuondoa Rais Nyerere, marais wengine wote waliofuatia, walisifiwa na walikosolewa hadharani, kama Ilivyokuwa kwa Rais Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli na sasa Rais Samia, wote wanasifiwa nav wanakosolewa na hakuna ubaya wowote na ukosoaji sii dhambi, sii kosa!

Freedom of expression ya haki ya kumpongeza rais, inakwenda sambamba na haki ya kumkosoa rais, hivyo ukosoaji wa Dr. Bashiru, naomba uheshimiwe!

Ukosoaji Enzi za Nyerere
Kwa vile mimi ni mtu wa mastori mastori ya kimepanda kikashuka, naomba wale wa short and clear muishie hapa na ku jump kwenye cònclusion, wale wa mastori stori, tuendeleeni

Tukawasisitiza watu humu kuwa Rais Samia na yeye ni binadamu, sio malaika!, Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda

Hivyo kama ilivyo kwenye haki ya kupiga kura, inakwenda sambamba na haki ya kupigiwa kura, vivyo hivyo kwenye haki ya kusifu na kumpongeza rais Samia, haki hiyo ya kumpongeza, inakwenda sambamba na haki ya kumkosoa rais Samia, mkosoaji asishambuliwe yeye, ishambuliwe hoja yake!.

Wapongezaji wa Mama kwa jinsi anavyoupiga mwingi wana haki ya kusifu na kupongeza, ila wanapotokea watu ma critiki, wanaopinga Mama kuupiga mwingi, wapongezaji wasijimilikishe haki za wengine kumkosoa Mama Samia, hivyo kuwashukia wakosoaji as if ni wamemkufuru Mungu kama sasa Dr. Bashiru anavyoshukiwa kama mwewe anavyo sarandia kunyakuwa kifaranga cha kuku!.

Hitimisho
Wanaosifu wasifu kwa hoja, ni haki yao kusifu, lakini pia, wanao kosoa, wakosoe kwa hoja kwa kutumia ukosoaji wa contructive criticism, ukosoaji wenye nia njema ya kujenga, kwa kutumia lugha ya staha na amini usiamini, unaweza kukuta, wanaomkosoa Rais Mama Samia, ndio wanao msaidia kuliko wanaomsifu!.

Wasalaam

Paskali
 
Tatizo sio kukosoa unadhani haya matamshi yangetoka toka mwanachama wa chama chochote cha upinzani ingekuwa hoja? ungetuwaambia labda hao kina Mkapa, JK na JPM kama walikosolewa na wana CCM au watu wa serikalini.

Waliomkosoa JPM na yaliyowakuta tunayajuwa na Bashiru ndio alikuwa mbele kuwahoji kwenye vikao au kasahahu? JK alitukanwa sana tu lakini wapinzani tuambie nani alitoka ndani ya CCM akamtukana kiongozi wake akabaki salama.

Hata Mbowe anatukanwa lakini tuambie nani katika Chadema aliwahi kumkosoa kiongozi wake akabaki salama. Ukosoaji mzuri kama unaona sikubaliani na chama changu unakaa pembeni sio uko ndani ya system halafu unamtukana kiongozi wako.

Chama ina vikao vyao vya kukosoana na haya aliongea mwenyewe BASHIRU.
 
Unakumbuka hoja za HUSSEIN BASHE kwa usalama wa Taifa kabla hajawa waziri
 
"Akili kubwa hujadili hoja ,akili ya Kati hujadili matukio na akili ya chini hujadili watu"Socrates

Ni bora watu hasa walio ndani ya chama Cha mapinduzi wajikite kujibu hoja za Dr Bashiru kwa kutumia lugha Safi na staha kuliko vijembe na kejeli ambazo kimsingi hazina tija kwa taifa na chama.

Tumekuwa taifa la ajabu Sana kwa kuwa na tabia ya kumshambulia mleta hoja badala ya hoja hata mzee kikwete kasha wahi sema "hoja ya mtu haupingwi rungu" pamoja na jaji mstaafu jaji warioba amesisitiza Bashiru ajibiwe kwa hoja, sitaki kuamini chama Cha mapinduzi hakina watu makini wa kujibu hoja za Dr Bashiru.

"Kukatwa kwa kisu ni tofauti na kukatwa kwa ulimi"
 
tatizo walisifiwa na kukoselewa na watu gani?

Nadhani mwezi/miezi imepita kuna msimamizi wa mhimili alijitokeza akawaambia wanajamii yeyote atakayemkosoa mheshimiwa raisi, awe CCM ama chama kingine wasimwache hata kidogo, wahakikishe wanadeal nae perpendicular

Wengi wa wakosoaji wakiwa nje ya chama tawala huwa ndani ya dakika/saa/siku kadhaa huishia kupatwa na madhila mabaya kama sing-bad the sailor ni vigumu sana kuukubali ukweli katika zama hizi na kutetea uongo
bora ukosoaji uendelee ndani ya chamaa
 
Hata mahakamani mtu anaweza fungwa maisha au kuachiliwa huru kama "motive" imejukikana.....


Huwezi sema ni freedom of speech wakati motive ya mhusika inajulikana.......motive ndo inafanya MTU anapoongea ionekane ni Busara au majungu ...motive...Motive ya Bashiru ni kuendeleza demokrasia?ambayo akiikanyaga alipokuwa na power?au kushambulia kundi moja ili kundi lake lipate mileage?

Ujinga ni kutokujua...lakini upumbavu ni kujua na kukataa kitu kiko wazi kabisa
 
Mpaka sasa hakuna hata mmoja kati ya wanao mshambulia Bashiru ambae anaweza kuonyesha kosalake katika hotuba yake.

Wote wanamshambulia kwa mambo ya kipuuzi tu, yani wanamshambulia kwa mambo binafsi na sio kwa hojazake za kupinga kusifiasifia.

Kifupi wanachuki binafsi to na wengi wanajipendekeza Ili waonekane wanampenda mkuu,Ili ugali uendelee.

Tumefika pabaya sana.
Watu wanajitoa akili kupambana na ukweli kwasababu ya ulafi wa madaraka.
 
Wanaomkosa Bashiru wapo sahihi na Bashiru yupo sahivi sababu wote ni wasaka fursa hakuna ambaye yupo ajili ya wananchi au nchi, Bashiru alihusika na mauji sn enzi ya dikteta
 
Bashiru na wana CCM wenzake ni mashetani tupu
 
"baada ya uchaguzi niliendesha kipindi cha "Kiti Moto" produced by Masai Studio, huko ni ukosoaji mwanzo mwisho!. Kuna viongozi walukuwa wakialikwa Kiti Moto, wanakimbia!."

Daaaah Mkuu leo ndio umenifumbua macho. Kumbe aka ya ile nyama yetu maarufu, chanzo ni hapa[emoji1787][emoji1787][emoji1787].

Nyama ya Nguruwe aka Kitimoto aka Pascal Mayalla.

Sent from my SM-A715F using JamiiForums mobile app
 
Nawe mbona mgumu kuelewa, tumesema Bashiru alichokisema kiko sahihi kwa kiwango cha juu sana. Tatizo haya anayoyakemea aliyafanya yeye wakati wa magufuli kwa vile alikuwa anakula mlo wake, and therefore ni mnafiki. Siyo kuwa anataka advancement ya wakulima, anawatetea wakulima, never, ni kwa vile amepokwa madaraka aliyorundikiwa na magufuli!
Once a traitor, always a traitor. It only takes true repentance and a turn -around to regain public Trust! by Maria sarurungi
 
Paskali mbona sikuelewi, wewe unakataa Chadema wasijieleze na wewe huyohuyo unataka uhuru wa kujieleza uwepo! Unajipa upopo huku ukiwa mwanasheria.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…