Mzee Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Hayati Magufuli, walisifiwa, walikosolewa! Haki ya kusifu/kupongeza iende sambamba na haki ya kukosoa!

Mzee Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Hayati Magufuli, walisifiwa, walikosolewa! Haki ya kusifu/kupongeza iende sambamba na haki ya kukosoa!

Hata mahakamani mtu anaweza fungwa maisha au kuachiliwa huru kama "motive" imejukikana.....


Huwezi sema ni freedom of speech wakati motive ya mhusika inajulikana.......motive ndo inafanya MTU anapoongea ionekane ni Busara au majungu ...motive...Motive ya Bashiru ni kuendeleza demokrasia?ambayo akiikanyaga alipokuwa na power?au kushambulia kundi moja ili kundi lake lipate mileage?

Ujinga ni kutokujua...lakini upumbavu ni kujua na kukataa kitu kiko wazi kabisa
Tatizo lenu mmelelewa kwenye kizazi cha kusifu na kuabudu, ndio maana anapotokea mtu kutaka lifanyike jambo tofauti na hilo kwenu inakuwa nongwa.

Mnataka kutengeneza taifa la wajinga wa kusifia tu, hasa anapoguswa kipenzi chenu, na usituletee habari za motive hapa, alichokifanya Dr. Bashiru ni haki yake, na ni halali yake.

Hizo hisia zenu za anataka kumuharibia mama yenu pelekeni pengine, hili taifa linaongozwa kwa sheria na taratibu, sio kwa hisia kama zenu.

Kama unaona Dr. Bashiru amekosea kwa ile kauli yake mpelekeni mahakamani ambapo unasema wanaangalia motive, halafu uone kama hiyo motive yako bila "established facts" itafanya kazi, usifundishe watu ujinga hapa, mahakama haiamui mambo kwa hisia.
 
Tatizo lenu mmelelewa kwenye kizazi cha kusifu na kuabudu, ndio maana anapotokea mtu kutaka lifanyike jambo tofauti na hilo kwenu inakuwa nongwa.

Mnataka kutengeneza taifa la wajinga wa kusifia tu, hasa anapoguswa kipenzi chenu, na usilete habari za motive hapa, alichokifanya Dr. Bashiru ni haki yake, na ni halali..

Hizo hisia zenu za anataka kumuharibia mama yenu pelekeni pengine, hili taifa linaongozwa kwa sheria na taratibu, sio kwa hisia kama zenu.

Kama unaona Dr. Bashiru amekosea kwa ile kauli yake mpelekeni mahakamani ambapo unasema wanaangalia motive, halafu uone kama hiyo motive ystopako bila established facts itafanya kazi, usifundishe watu ujinga hapa.
Stop quoting me....shambulia hoja sio kushambulia wachangiaji
 
Stop quoting me....shambulia hoja sio kushambulia wachangiaji
Usinitishe, nitaku-quote kila nikiamua, una hoja gani ya maana uliyoandika hapo juu zaidi ya kuleta hisia zako kwa mgongo wa "motive"?

Hapa duniani hakuna motive mbaya inayopewa support na sheria, they are all good.

- Unauliza vipi motive ya Dr. Bashiru kwenye kuendeleza demokrasia ikiwa alichofanya kipo kisheria? sema una yako mengine.

- Unataka kutumia historia ya Dr. Bashiru ili kumnyima haki yake, utambue hata mwizi ana haki zake na zinaheshimiwa kisheria.

Kachezee akili za wajinga wasiojielewa, nimekwambia kama unaamini hizo hisia zako ulizozipa jina la "motive" zipo kisheria, nenda mahakamani kamfunge Dr. Bashiru
 
Hata mahakamani mtu anaweza fungwa maisha au kuachiliwa huru kama "motive" imejukikana.....


Huwezi sema ni freedom of speech wakati motive ya mhusika inajulikana.......motive ndo inafanya MTU anapoongea ionekane ni Busara au majungu ...motive...Motive ya Bashiru ni kuendeleza demokrasia?ambayo akiikanyaga alipokuwa na power?au kushambulia kundi moja ili kundi lake lipate mileage?

Ujinga ni kutokujua...lakini upumbavu ni kujua na kukataa kitu kiko wazi kabisa
Ahh The Boss akili kubwa

Hebu agiza kinywaji hapo ulipo

Nakuja kukulipia

Ova
 
Wanaomkosa Bashiru wapo sahihi na Bashiru yupo sahivi sababu wote ni wasaka fursa hakuna ambaye yupo ajili ya wananchi au nchi, Bashiru alihusika na mauji sn enzi ya dikteta
Inatosha kama unakubali hojayake ipo sahihi.
Hayo mambo ya mauwaji ni mambo ya kuhisi tu, hapa mjadala ni kilealichoongea hadharani kilamtu akaona na kusikia.
 
James Henry kuna wakati alituambia wote wanaomkosoa bwana yule wake zao watatiwa mimba! Hii tabia ya viongozi kutopenda kukukosolewa imeanza zamani kidogo.
Mpaka sasa hakuna hata mmoja kati ya wanao mshambulia Bashiru ambae anaweza kuonyesha kosalake katika hotuba yake.

Wote wanamshambulia kwa mambo ya kipuuzi tu, yani wanamshambulia kwa mambo binafsi na sio kwa hojazake za kupinga kusifiasifia.

Kifupi wanachuki binafsi to na wengi wanajipendekeza Ili waonekane wanampenda mkuu,Ili ugali uendelee.

Tumefika pabaya sana.
Watu wanajitoa akili kupambana na ukweli kwasababu ya ulafi wa madaraka.
 
Usinitishe, nitaku-quote kila nikiamua, una hoja gani ya maana uliyoandika hapo juu zaidi ya kuleta hisia zako kwa mgongo wa "motive"?

Kachezee akili za wajinga wasiojielewa, nimekwambia kama unaamini hizo hisia zako ulizozipa jina la "motive" nenda mahakamani kamfunge Dr. Bashiru
Hajui lolote kuhusu sheria, sometimes muonekano au maandishi hutambulisha kilichomjaa mtu kichwani na moyoni mwake.

Huyo ni wakala wao " team anaupiga mwingi" in Bashiru's voice.
 
Magufuli alikosolewa na Wana ccm? Pili Kuna kukosoa na kukejeli..

Bunge lililopita bila Shaka umeona ukoeoaji lakini Bashiru kakosoa au kakejeri na kuchochea wakulima wawe wakaidi na wahaini.
 
Wanabodi,
Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa huja na makala zangu za " Kwa Maslahi ya Taifa". Makala ya leo ni kuhusu moja ya haki muhimu sana ndani ya katiba, kwenye Ibara ya 18, iitwayo haki ya uhuru wa kutoa maoni, "freedom of expression" ni haki inayotolewa na katiba yetu lakini kufuatia kushambuliwa kila kona kwa Dr. Bashiru, kutokana na kutoa nawazo yake ya ukosoaji, naona kuna watu wanataka kuingilia haki hii muhimu na kujimilikisha wao kwa kuingilia uhuru wa maoni wa watu wengine na hata kuwapangia ni maoni gani watoe!. Yaani wenye haki ni wanaosifu tuu na kupongeza, lakini ukikosoa, inakuwa nongwa kama anavyoshukiwa Dr. Bashiru!.

Kwa vile wengi humu ni madogo, sisi kaka zenu tuna wajibu wa kuwaelimisha ya nyuma, toka enzi za Mzee Rukhsa, Ben, JK na JPM, wote walisifiwa na walikosolewa!. Ile haki ya Freedom of Expression provided na katiba yetu, yenye haki ya kusifu na kupongeza, inapaswa kwenda sambamba na haki ya kukosoa!. Hivyo kuna watu wanataka haki ya Mama ni asifiwe tuu na apongezwe tuu, lakini akikosolewa ni kosa, ni dhambi!.

Naomba tukumbushane tuu uhuru wa kutoa maoni yaani freedom of expression ni haki ya maoni huru ya kila mtu, wa kusifu na kupongeza wawe huru na wa kukosoa pia wawe huru, haki yao iheshimiwe, mtu akitoa mawazo yake kuhusu jambo lolote, hata kama hukubaliani nalo, mawazo yake yaheshimiwe!.

Bandiko hili ni kufuatia ukosoaji uliofanywa na Dr. Bashiru, watu wanamshukia kila kona, utadhani amemkufuru Mungu!, kumbe ni ametoa tuu mawazo yake na maoni yake, hata kama haukubaliani naye, heshimu mawazo yake, kama unatofautiana, pangua hoja zake, hoja kwa hoja na sio kwa viroja vya kumshambulia yeye binafsi. Hoja zake zijibiwe au zipingwe kwa hoja!.

Ukimuondoa Rais Nyerere, marais wengine wote waliofuatia, walisifiwa na walikosolewa hadharani, kama Ilivyokuwa kwa Rais Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli na sasa Rais Samia, wote wanasifiwa nav wanakosolewa na hakuna ubaya wowote na ukosoaji sii dhambi, sii kosa!.

Freedom of expression ya haki ya kumpongeza rais, inakwenda sambamba na haki ya kumkosoa rais, hivyo ukosoaji wa Dr. Bashiru, naomba uheshimiwe!.

Ukosoaji Enzi za Nyerere
Kwa vile mimi ni mtu wa mastori mastori ya kimepanda kikashuka, naomba wale wa short and clear muishie hapa na ku jump kwenye cònclusion, wale wa mastori stori, tuendeleeni


Tukawasisitiza watu humu kuwa Rais Samia na yeye ni binadamu, sio malaika!, Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda

Hivyo kama ilivyo kwenye haki ya kupiga kura, inakwenda sambamba na haki ya kupigiwa kura, vivyo hivyo kwenye haki ya kusifu na kumpongeza rais Samia, haki hiyo ya kumpongeza, inakwenda sambamba na haki ya kumkosoa rais Samia, mkosoaji asishambuliwe yeye, ishambuliwe hoja yake!.

Wapongezaji wa Mama kwa jinsi anavyoupiga mwingi wana haki ya kusifu na kupongeza, ila wanapotokea watu ma critiki, wanaopinga Mama kuupiga mwingi, wapongezaji wasijimilikishe haki za wengine kumkosoa Mama Samia, hivyo kuwashukia wakosoaji as if ni wamemkufuru Mungu kama sasa Dr. Bashiru anavyoshukiwa kama mwewe anavyo sarandia kunyakuwa kifaranga cha kuku!.

Hitimisho
Wanaosifu wasifu kwa hoja, ni haki yao kusifu, lakini pia, wanao kosoa, wakosoe kwa hoja kwa kutumia ukosoaji wa contructive criticism, ukosoaji wenye nia njema ya kujenga, kwa kutumia lugha ya staha na amini usiamini, unaweza kukuta, wanaomkosoa Rais Mama Samia, ndio wanao msaidia kuliko wanaomsifu!.

Wasalaam

Paskali
Kama Bashiru Ali alivyofanya,nimekuelewa P
 
Back
Top Bottom