Wanabodi,
Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa huja na makala zangu za " Kwa Maslahi ya Taifa". Makala ya leo ni kuhusu moja ya haki muhimu sana ndani ya katiba, kwenye Ibara ya 18, iitwayo haki ya uhuru wa kutoa maoni, "freedom of expression" ni haki inayotolewa na katiba yetu lakini kufuatia kushambuliwa kila kona kwa Dr. Bashiru, kutokana na kutoa nawazo yake ya ukosoaji, naona kuna watu wanataka kuingilia haki hii muhimu na kujimilikisha wao kwa kuingilia uhuru wa maoni wa watu wengine na hata kuwapangia ni maoni gani watoe!. Yaani wenye haki ni wanaosifu tuu na kupongeza, lakini ukikosoa, inakuwa nongwa kama anavyoshukiwa Dr. Bashiru!
Kwa vile wengi humu ni madogo, sisi kaka zenu tuna wajibu wa kuwaelimisha ya nyuma, toka enzi za Mzee Rukhsa, Ben, JK na JPM, wote walisifiwa na walikosolewa!. Ile haki ya Freedom of Expression provided na katiba yetu, yenye haki ya kusifu na kupongeza, inapaswa kwenda sambamba na haki ya kukosoa!. Hivyo kuna watu wanataka haki ya Mama ni asifiwe tuu na apongezwe tuu, lakini akikosolewa ni kosa, ni dhambi!.
Naomba tukumbushane tuu uhuru wa kutoa maoni yaani freedom of expression ni haki ya maoni huru ya kila mtu, wa kusifu na kupongeza wawe huru na wa kukosoa pia wawe huru, haki yao iheshimiwe, mtu akitoa mawazo yake kuhusu jambo lolote, hata kama hukubaliani nalo, mawazo yake yaheshimiwe!.
Bandiko hili ni kufuatia ukosoaji uliofanywa na Dr. Bashiru, watu wanamshukia kila kona, utadhani amemkufuru Mungu!, kumbe ni ametoa tuu mawazo yake na maoni yake, hata kama haukubaliani naye, heshimu mawazo yake, kama unatofautiana, pangua hoja zake, hoja kwa hoja na sio kwa viroja vya kumshambulia yeye binafsi. Hoja zake zijibiwe au zipingwe kwa hoja!
Ukimuondoa Rais Nyerere, marais wengine wote waliofuatia, walisifiwa na walikosolewa hadharani, kama Ilivyokuwa kwa Rais Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli na sasa Rais Samia, wote wanasifiwa nav wanakosolewa na hakuna ubaya wowote na ukosoaji sii dhambi, sii kosa!
Freedom of expression ya haki ya kumpongeza rais, inakwenda sambamba na haki ya kumkosoa rais, hivyo ukosoaji wa Dr. Bashiru, naomba uheshimiwe!
Ukosoaji Enzi za Nyerere
Kwa vile mimi ni mtu wa mastori mastori ya kimepanda kikashuka, naomba wale wa short and clear muishie hapa na ku jump kwenye cònclusion, wale wa mastori stori, tuendeleeni
Tukawasisitiza watu humu kuwa Rais Samia na yeye ni binadamu, sio malaika!,
Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda
Hivyo kama ilivyo kwenye haki ya kupiga kura, inakwenda sambamba na haki ya kupigiwa kura, vivyo hivyo kwenye haki ya kusifu na kumpongeza rais Samia, haki hiyo ya kumpongeza, inakwenda sambamba na haki ya kumkosoa rais Samia, mkosoaji asishambuliwe yeye, ishambuliwe hoja yake!.
Wapongezaji wa Mama kwa jinsi anavyoupiga mwingi wana haki ya kusifu na kupongeza, ila wanapotokea watu ma critiki, wanaopinga Mama kuupiga mwingi, wapongezaji wasijimilikishe haki za wengine kumkosoa Mama Samia, hivyo kuwashukia wakosoaji as if ni wamemkufuru Mungu kama sasa Dr. Bashiru anavyoshukiwa kama mwewe anavyo sarandia kunyakuwa kifaranga cha kuku!.
Hitimisho
Wanaosifu wasifu kwa hoja, ni haki yao kusifu, lakini pia, wanao kosoa, wakosoe kwa hoja kwa kutumia ukosoaji wa contructive criticism, ukosoaji wenye nia njema ya kujenga, kwa kutumia lugha ya staha na amini usiamini, unaweza kukuta, wanaomkosoa Rais Mama Samia, ndio wanao msaidia kuliko wanaomsifu!.
Wasalaam
Paskali