Mzee Mwinyi: Nyerere alitaka pawepo mgombea binafsi lakini CC ya CCM ilimkatalia, pia CCM ilipinga vyama kuungana ikihofia itakufa

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Hiki kitabu cha mzee Mwinyi kimejibu maswali mengi sana na unaweza kuamini kabisa CCM inakwamisha mambo mengi kwa maslahi yake binafsi.

Mzee Mwinyi anasema Nyerere alipendekeza pawepo na mgombea binafsi katika mfumo wa vyama vingi lakini kamati kuu ilikataa kwa madai anaweza kutokea mtu maarufu ndani ya CCM akaamua kugombea baada ya kukatwa na hivyo chama kitaangushwa.

Kadhalika mzee Mwinyi anasema CCM ilikataa vyama vya siasa kuungana kwa sababu vinaweza kujenga chama kimoja chenye nguvu na kuiangusha CCM.

Mungu Ibariki Tanzania.
 
Hapo Mzee Nyerere alichemka

Swali lilikuwa huyo mgombea binafsi akishinda atatekeleza sera gani? sababu hana sera yeyote anakuwa tu kama mlevi tu anayetoa tu ahadi hewa za majukwaani

Pili ugumu wa kufanya kazi akishinda.Mfano kashinda uraisi halafu wabunge wote wanatoka kwenye chama.Aweza pigiwa kura ya kutokuwa na imani naye wakati wowote na akatolewa madarakani.Pia aweza kwamishwa na walio wengi bungeni na kwenye watendaji

Lakini mgombea binafsi akiruhusiwa hata leo wa kwanza kufa ni vyama vya upinzani sababu havina network kubwa mijini na vijijini.Pia ni rahisi mtu kushinda kwa kutumia mtandao wa chama kuliko wa kibinafsi laba awe bilionea!! Kampeni nchi nzima sio lelemama
 
Nilitarajia mzee Mwinyi angekua mtu ambaye angetuachia katiba mpya ila bado naye alichemka katiba mpya ni mwiba kwa wanaccm sababu wanataka wawatawale watanzania na sio kuwaongoza...

Mwalimu alisema mwaka 1982 kuwa kwa katiba iliyopo ipo siku kuna mtu ataitumia vibaya sababu inampa mamlaka makubwa na yasiyo na ukomo na hawezi kuhojiwa popote kwa afanyayo!

Kweli miaka 33 baadaye tulijionea kilichosemwa! Kwangu mimi Mwalimu alifanya mengi mazuri ila la kutuachia katiba hii alichemka na Mwinyi akafuata njia ile ile ! Jk alijaribu kidogo kama kawaida CCM wakambana hii ni kiashiria kuwa ni mwiba mkali wa CCM

Mkapa hakutaka kuongelea kabisa ila alijitahidi kuzungumzia Tume huru ya uchaguzi akikumbuka madhila aliyoyaleta kule Zanzibar 2001 ila suala la katiba alilijua vizuri sana ila hakujihusisha
 
Mgombea binafsi ni porojo tu hata ulaya na marekani wagombea uraisi huwa na vyama

Sana sana labda mbunge na diwani ndio waweza penya ugombea binafsi !!! Tena wa kumulika na tochi.Uraisi si rahisi mgombea binafsi kushinda iwe Africa au ulaya au marekani
 
Kukataa mgombea binafsi ni kinyume cha Katiba!
Ref; vyama vyote vyote vilivyopo sio kila mtu anaona vinamfaa!
Jee hana Haki ya Kuchaguliwa na kuchagua kama Mwananchi?
 
Hapo Mzee Nyerere alichemka

Swali lilikuwa huyo mgombea binafsi akishinda atatekeleza sera gani? sababu hana sera yeyote anakuwa tu kama mlevi tu anayetoa tu ahadi hewa za majukwaani

Pili ugumu wa kufanya kazi akishinda.Mfano kashinda uraisi halafu wabunge wote wanatoka kwenye chama.Aweza pigiwa kura ya kutokuwa na imani naye wakati wowote na akatolewa madarakani.Pia aweza kwamishwa na walio wengi bungeni na kwenye watendaji

Lakini mgombea binafsi akiruhusiwa hata leo wa kwanza kufa ni vyama vya upinzani sababu havina network kubwa mijini na vijijini.Pia ni rahisi mtu kushinda kwa kutumia mtandao wa chama kuliko wa kibinafsi laba awe bilionea!! Kampeni nchi nzima sio lelemama
Kama hivyo ndivyo Kwamba wakwanza Kufa itakua vyama Pinzani sasa CCM ina hofu gani?

Mbona wao ndio vinara wakupinga Mgombea Binafsi?
 
Mgombea binafsi ni porojo tu hata ulaya na marekani wagombea uraisi huwa na vyama

Sana sana labda mbunge na diwani ndio waweza penya ugombea binafsi !!! Tena wa kumulika na tochi.Uraisi si rahisi mgombea binafsi kushinda iwe Africa au ulaya au marekani
Kanye West ni wa chama gani?
Amandla...
 
Wewe una akili kuliko Nyerere alieona umuhimu wake?
Hapo Mzee Nyerere alichemka

Swali lilikuwa huyo mgombea binafsi akishinda atatekeleza sera gani? sababu hana sera yeyote anakuwa tu kama mlevi tu anayetoa tu ahadi hewa za majukwaani

Pili ugumu wa kufanya kazi akishinda.Mfano kashinda uraisi halafu wabunge wote wanatoka kwenye chama.Aweza pigiwa kura ya kutokuwa na imani naye wakati wowote na akatolewa madarakani.Pia aweza kwamishwa na walio wengi bungeni na kwenye watendaji

Lakini mgombea binafsi akiruhusiwa hata leo wa kwanza kufa ni vyama vya upinzani sababu havina network kubwa mijini na vijijini.Pia ni rahisi mtu kushinda kwa kutumia mtandao wa chama kuliko wa kibinafsi laba awe bilionea!! Kampeni nchi nzima sio lelemama
 
CC siku zote inahofia kivuli chake tu hakuna jipya wao wanakwamisha mambo mengi sana hata ndio hao walimpiga mkwara JK akaishia kati katiba mpya.....
 
Hapo Mzee Nyerere alichemka

Swali lilikuwa huyo mgombea binafsi akishinda atatekeleza sera gani? sababu hana sera yeyote anakuwa tu kama mlevi tu anayetoa tu ahadi hewa za majukwaani

Pili ugumu wa kufanya kazi akishinda.Mfano kashinda uraisi halafu wabunge wote wanatoka kwenye chama.Aweza pigiwa kura ya kutokuwa na imani naye wakati wowote na akatolewa madarakani.Pia aweza kwamishwa na walio wengi bungeni na kwenye watendaji

Lakini mgombea binafsi akiruhusiwa hata leo wa kwanza kufa ni vyama vya upinzani sababu havina network kubwa mijini na vijijini.Pia ni rahisi mtu kushinda kwa kutumia mtandao wa chama kuliko wa kibinafsi laba awe bilionea!! Kampeni nchi nzima sio lelemama

Kwa katiba hii wala rais hahitaji kuwa na chama huko bungeni ili kumuunga mkono. Ukishakuwa rais kisha una ule mlolongo wa uteuzi, hao wote wanakutosha kuburuza wananchi wote. mfano halisi wa madaraka ya kimungu aliyopewa rais umeonekana wakati wa Magufuli. Chochote alichotaka ametekeleza na akasifiwa kinafiki. Ilani ya ccm ilisema mwanafunzi akipata mimba akimaliza kujifungua atarejea shule, Magufuli alikataa mchana kweupe hadharani. Ilani ya ccm iliongelea mwendelezo umeme wa Gas, Magufuli kaingia kaacha, kutekeleza umeme wa maji, na ccm wako kimya.

Namna ya kutawala nchi hii ukiwa rais bila hata chama, unaunda kikundi cha watu wasiojulikana, kazi yake ni kuteka na kuua yoyote anayekupinga na hakuna uchunguzi. Mbunge yoyote huko bungeni kuanzia spika akifungua mdomo, anatekwa, kushambuliwa kwa risasi popote alipo. Katika mazingira hayo mgombea binafsi wa urais anashindwaje kuongoza nchi? Tena ukiwa mgombea binafsi inakuwa rahisi kuongezewa muda wa kukaa madarakani kupitia hofu utakayokuwa umeijenga kwenye nchi. Mfano wa uwezo wa rais binafsi kuoongoza nchi tumeuona ndani ya hii miaka mitano.
 
Hapo Mzee Nyerere alichemka

Swali lilikuwa huyo mgombea binafsi akishinda atatekeleza sera gani? sababu hana sera yeyote anakuwa tu kama mlevi tu anayetoa tu ahadi hewa za majukwaani

Pili ugumu wa kufanya kazi akishinda.Mfano kashinda uraisi halafu wabunge wote wanatoka kwenye chama.Aweza pigiwa kura ya kutokuwa na imani naye wakati wowote na akatolewa madarakani.Pia aweza kwamishwa na walio wengi bungeni na kwenye watendaji

Lakini mgombea binafsi akiruhusiwa hata leo wa kwanza kufa ni vyama vya upinzani sababu havina network kubwa mijini na vijijini.Pia ni rahisi mtu kushinda kwa kutumia mtandao wa chama kuliko wa kibinafsi laba awe bilionea!! Kampeni nchi nzima sio lelemama
Daah unauliza mgombea binafsi akishinda atatekeleza sera gani? Aisee huu ni ukilaza wa hali ya juu
 
Hapo Mzee Nyerere alichemka

Swali lilikuwa huyo mgombea binafsi akishinda atatekeleza sera gani? sababu hana sera yeyote anakuwa tu kama mlevi tu anayetoa tu ahadi hewa za majukwaani

Pili ugumu wa kufanya kazi akishinda.Mfano kashinda uraisi halafu wabunge wote wanatoka kwenye chama.Aweza pigiwa kura ya kutokuwa na imani naye wakati wowote na akatolewa madarakani.Pia aweza kwamishwa na walio wengi bungeni na kwenye watendaji

Lakini mgombea binafsi akiruhusiwa hata leo wa kwanza kufa ni vyama vya upinzani sababu havina network kubwa mijini na vijijini.Pia ni rahisi mtu kushinda kwa kutumia mtandao wa chama kuliko wa kibinafsi laba awe bilionea!! Kampeni nchi nzima sio lelemama
Mataga a.k.a SUKUMA GANG katika ubora wako[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Mgombea binafsi ni porojo tu hata ulaya na marekani wagombea uraisi huwa na vyama

Sana sana labda mbunge na diwani ndio waweza penya ugombea binafsi !!! Tena wa kumulika na tochi.Uraisi si rahisi mgombea binafsi kushinda iwe Africa au ulaya au marekani
Kwa hiyo leo unawaiga mabeberu wezi wa rasilimali?
 
Back
Top Bottom