Swali lilikuwa huyo mgombea binafsi akishinda atatekeleza sera gani?
Kwani lazima aweke maandishi ambayo hayatekelezeki ?
Katiba imeandikwa nataratibu mbalimbali zipo kwa maandishi lakini kila siku tunalalamika kwamba katiba haitekelezwi ?
Kwa nini iwe lazima kuwa na sera wakati hizo zilizoandikwa nyingi hazitekelezwi ?
Pili ugumu wa kufanya kazi akishinda.Mfano kashinda uraisi halafu wabunge wote wanatoka kwenye chama.Aweza pigiwa kura ya kutokuwa na imani naye wakati wowote na akatolewa madarakani.
Mkuu sidhani kama hii sheria ya kuwa na imani ingekuwepo laiti kama angepitishwa mgombea binafsi.
Na bila shaka hili la kuwa na imani ama kutokuwa na imani na raisi halikuwa rasmi kwamba ndo litakuwepo endapo angechaguliwa mgombea binafsi.
Maana yake ni kwamba unasema nyerere alichemka kupendekeza mgombea binafsi kwa kutumia kipengele ambacho hakikuwa rasmi kwamba kitumike kwa mgombea binafsi.
Hivyo kusema nyerere kachemka sio sawa.
.Pia aweza kwamishwa na walio wengi bungeni na kwenye watendaji
Shida yako unadhani kuwa huo utaratibu ungepita basi taratibu zingine zingebaki vilevile.
Unatakiwa uelewe kuwa taratibu zingebadilishwa.
Pengine lilipendekezwa hilo kwanza alafu lingekubaliwa ndo marekebisho mengine yangefuata.
Kwa maana hiyo unatakiwa uiwache kauli ya kusema nyerere alichemka wakati alipendekeza jambo ambalo lingekubaliwa ndipo mabadiliko ambayo unasema wewe maechemka ndo yangefanyika