Nimenukuu maneno ya rais Mstaafu kutoka kwenye kitabu chake ambapo alikua akizungumzia suala la yeye kunteua Lyatonga Mrema kama Naibu Waziri Mkuu. Mwinyi amekiri bayana kua cheo hicho hakipo kwenye katiba.
Kwa muktadha huo,je Rais Samia hana washauri wazuri ama haoni kua amevunja katiba?!
Kama amevunja, hakuna taasisi za kupinga uvunjaji huo wa katiba?!!
Soma nukuu hiyo-
Je Waziri Mkuu aliyepo anapwaya hivyo ilibidi apate msaidizi? Je na kumtoa madarakani ni kuvunja serikali na ingebidi kuitisha uchaguzi?!
Angefanyeje ili kumtoa?!! Angem-Ndugai tu, naam,kama spika Ndugai alivyoachia kiti baada ya Mama kutoa hutuba fulani na kufuatiwa na sauti za chawa fulani chamani na hatimae Ndugai akaitisha press na kulia "nimekosa Mimi,nimekosa Mimi" na akatangaza kuhiuzulu. Aliepo nafikiri angesema tu kwa sababu za kitabibu!!
Je Mama amesigina katiba kwa kuteua Naibu Waziri Mkuu kwa maslahi ya Taifa ama maslahi binafsi?!!
Nafikiri sababu kuu pia ni maandalizi ya uchaguzi wa 2025. Kivipi?!! Waziri Mkuu aliyepo hana mvuto mkubwa wa kisiasa na hata Makamo wa Rais aliyepo hana kabisa mvuto mkubwa wa kisiasa japo anatokea kanda ya ziwa na amekua mbunge na waziri kwa muda mrefu.
Kwa nini Biteko awe Naibu Waziri Mkuu?!! Ili angalau upate kura nyingi za uraisi Kanda ya Ziwa inabidi uwe na strong base ya watu wanaokubalika kanda ya Ziwa. Kwneye wabunge wote wa CCM wanaotoka kanda ya Ziwa,wenye walau ushawishi na usafi nafikiri ni Mh Angela Mabula na Mheshimiwa Biteko.
Kumuandaa makamo wa Raisi Mpya anaetoka kanda ya ziwa mbadala wa Mpango ndio lengo la teuzi hiyo.
Kwa Biteko imebidi maana ni mwanaume na Mabula ni mwanamke, haiwezekani kwenda kwenye uchaguzi na Rais Mwanamke na Makamu mgombea pia mwanamke.
Nafikiri ndio maana Biteko akaumbiwa hicho cheo tata kikatiba na nafikiri hata ulinzi anaopata unaonekana kua ni asset kwenye next project.