Mzee Sumaye: Niliambiwa mapema ndani ya Chama chetu hakuna Demokrasia, ukigusa uenyekiti wa Mbowe utashughulikiwa

Mzee Sumaye: Niliambiwa mapema ndani ya Chama chetu hakuna Demokrasia, ukigusa uenyekiti wa Mbowe utashughulikiwa

ukawa2020

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2016
Posts
339
Reaction score
1,315
Uchaguzi uliofanyija Jioni hii Kibaha Pwani wa kumpata mwenyekiti wa Kanda ya pwani, Chadema umekanilika

Kwa nafasi ya Mwenyekiti, Mgombea alikuwa Mzee Sumaye Peke yake ndipo zikapigwa kura za Ndio au hapana

Matokeo: Kura za Ndio kwa Mzee Sumaye ni 28, na kura za Hapana ni 48

Hivyo, nafasi ya Mwenyekiti bado iko wazi!

Mme mchanganya na ametahayari

---

NAFASI ya Uenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Pwani imekosa mridhi baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Kanda hiyo, Frederick Sumaye kushindwa kupata kura za kutosha.

Akisoma matokeo hayo leo tarehe 28 Novemba 2019, Msimamizi wa uchaguzi huo, Ole Sosopi amesema kwa matokeo hayo aliyepaswa kushinda alitakiwa apate kura za ndio zaidi ya asilimia 50 na nafasi hiyo inabaki wazi kwa sababu Sumaye hajafikisha asilimia hizo.

“Kutokana na Sumaye kugombea nafasi hiyo peke yake bila kuwa na mpinzani, tulipiga kura za ndio na hapana na baada ya kupigiwa kura, zilipatikana kura za ndio 28 sawa na asilimia 36.3, kura moja iliharibika na kura za hapana 48 sawa na asilimia 62.3, hivyo nafasi hiyo itabaki kuwa wazi, hivyo mamlaka itamtangaza Mwenyekiti baadaye,” amesema.


Sumaye afunguka kukosa kiti

Baada ya Matokeo hayo kutangazwa MwanaHALISI Online ilimtafuta Sumaye na kumuuliza juu ya namna alivyoyapokea matokeo hayo na kueleza kuwa,

“Nilikuwa mgombea pekee wa kiti cha Kanda na sikutegemea kwamba ningeweza kushindwa ingawaje baada ya gazeti moja kutoa taarifa kwamba nimechukua fomu ya kugonbea uenyekiti mambo yaliweza kubadilika, matokeo yaliyotokea ni kwamba nimeadhibiwa kwa kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya mwenyekiti taifa,” amesema.

Amesema kuwa aliwaeleza kwamba amechukua fomu lakini hajajaza hivyo baada ya matokeo hayo ataamua kama nitaichana chana au nitaijaza.

Ameueleza mtandao huu kuwa jambo lililomsukuma kuchukua fomu ya kugombea uenyekiti Taifa ni kwamba alihiyaji kushiriki demokrasia katika chama kwa sababu kimekuwa kikituhumiwa kuwa hakina demokrasia.

“Lengo langu lilikuwa ni kwamba Chadema huwa inatuhumiwa kwamba hakuna demokrasia na nafasi ya Mwenyekiti haiguswi hivyo nilitaka kuvunja hiyo watu wajue kuna demokrasia na kwamba nafasi ya Mwenyekiti ipo huru kwa mtu yoyote lakini kwa yaliyotokea ni kinyume chake,” amesema.

Katika uchaguzi huo inadaiwa kuwepo kundi kubwa pa wapambe wa Mbowe ambao walifika katika hoteli ya Njuweni mjini Kibaha, kwa lengo la kuhamasisha wapigakura kutomchagua Sumaye.

“Tumefika hapa kwa kazi moja tu. Nayo ni kumzuia Sumaye kuwa mwenyekiti wa Kanda kwa kuwa ameamua kutaka nafasi ya Mbowe,” ameeleza mmoja wa viongozi wa Chadema anayemuunga mkono mwenyekiti wa chama hicho.

Chanzo: Mwanahalisi





 
Ni nani alimshauri Mzee Sumaye kuhamia CHADEMA?

Hakujua kuwa CHADEMA ina mwenyewe? Ninapatwa na wasiwasi kuhusu IQ yake!

Unamtingisha Mbowe halafu unategemea kubaki na cheo ndani ya chama chake! Thubutu!

Ninamuhurumia sana huyu Mzee!

Baada ya Uchaguzi ndani ya CHADEMA kuna uwezekano wa kufukuzwa au kuondoka CHADEMA hasa ikichukuliwa kuwa amechukua fomu kupambana na Mbowe katika kiti cha Mwenyekiti Taifa!
 
Duh...!, kama kakataliwa Kanda tuu, huku mimi nilishauri ampokee Mbowe, then ni bora tuu arejee nyumbani!.

P
 
Mbona tulikuwa naye kwenye mahafali ya OUT tena alikuja na Escort.ya Polisi naona ameshawaacha Solemba!

Naomba usemacho kiwe kweli. Siafiki kabisa Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti wa cdm na sitamsupport kwenye nafasi hiyo, ila siko tayari kuona nafasi hiyo inaangukia kwa mwanaccm yoyote. Maana inaeleweka fika Sumaye sio mwanaCHADEMA, bali ni mwanaccm aliyeko likizo huko CHADEMA.
 
Ni nani alimshauri Mzee Sumaye kuhamia CHADEMA?

Ninamuhurumia sana huyu Mzee!

Baada ya Uchaguzi ndani ya CHADEMA kuna uwezekano wa kufukuzwa hasa ikichukuliwa kuwa amechukua fomu kupambana na Mbowe!
Yani kashindwa uenyekiti wa kanda ndio aende akashindane kuwa mwenyekiti wa taifa? 😂 au unamaanisha nn
 
Uchaguzi uliofanyija Jioni hii Kibaha Pwani wa kumpata mwenyekiti wa Kanda ya pwani, Chadema umekanilika

Kwa nafasi ya Mwenyekiti, Mgombea alikuwa Mzee Sumaye Peke yake ndipo zikapigwa kura za Ndio au hapana

Matokeo: Kura za Ndio kwa Mzee Sumaye ni 28, na kura za Hapana ni 48

Hivyo, nafasi ya Mwenyekiti bado iko wazi!
Safi sana,hii ndo demokrasia.I wish wamkatae Mbowe pia.
 
Ni nani alimshauri Mzee Sumaye kuhamia CHADEMA?

Ninamuhurumia sana huyu Mzee!

Baada ya Uchaguzi ndani ya CHADEMA kuna uwezekano wa kufukuzwa hasa ikichukuliwa kuwa amechukua fomu kupambana na Mbowe!

Kwa nini wamfukuze? Kama kweli kushindwa ngazi hiyo tayari mkakati wa kummaliza kisiasa umefanya kazi. CHADEMA imemalizana naye ki-hivyo. Imekula kwake. Hawahitaji kumfukuza.
 
Back
Top Bottom