Mzee Tashrif kafariki leo na kazikwa leo. Waislam wanajua heshima, umuhimu na maana ya mazishi

Sio hvo tu marehemu anapakwa shedo lipstick...jaman ifike muda Mungu TUMUOGOPE haya mapokeo ya Dunia yatatupeleka pabaya siku ya kiama
 
Isitoshe enzi hizo hakukuwa na mochware
 
Nimeona kila sehemu watu wanasema kama marehemu kazimia tu inakuaje, inapaswa wajue Waislamu hawaziki mtu bila report ya daktari na vipimo kupita kuthibitisha kifo.
 
Kukaa na mzoga ndani usio kuwa na faida yeyote siku tano ni moja wapo ya dalili ya upumbavu.
 
Kila mmoja na utaratibu wake kikubwa hatufanyi makosa
 
Muslims wako smart sana kwenye mambo yao. Haitumiki busara ya mtu bali miongozo ya vitabu.

Uislaam umetoa miongizo namna ya kumuhudumia maiti baada yamtu kufariki mpaka mazishi.

Ukristu ni vurugu mechi kila mtu anafanya limfaalo yeye. Hakuna maelekezo wala miongozo ya kufuata .

Mtu akifariki ni maamuzi yenu marehemu azikwe ama akae tu hata mwaka.

Ndio maana wakristo utakuta marehemu kafa ana wiki mbili manjemba hayashtuki wala nini.

Wakristu akifariki maskini anaweza kuzikwa siku hiyo kuondia bugudha.

Akifariki tajiri hatua ya kwanza inaundwa kamati ya msiba na kutengeneza majukumu.

1. Kutengeneza sare za msiba
2. Kukodi mziki mzuri mzito wa kuburudisha waombolezaji
3. Kuandaa usafiri marehemu akazikiwe kwao kakonko
4. Kuandaa vyakula na vinywaji kwa muda usio eleweka kama sio walokeole hapa msiba utageuka kilabu ya pombe.

Wakristu wenzangu sijui tunakwama wapi?
 
Mambo haya ya kuwaishana kuzikwa haya unaweza kuzikwa mzima mzima labda mtu ulilala Tu kidogo hiyo hapana siafiki

Sent from my Nokia C2 using JamiiForums mobile app
 
Tatizo baadhi ya wenzako kukuelewa ni vigumu kwa sababu wanaendeshwa na hisia.Umefanunua vizuri.
 
Mkiambiwa msome dini yenu muielewe maana yake ni kuepusha rai za kibinadamu zinazoweza kuleta hasara, Sasa huoni tu hapa unapuyanga tu kwa akili zako binafsi wakati ushaambiwa kabisa mkitaka kupata ukweli juu ya jambo lolote basi rejeeni katika Quran na Sunna. Dini sio maoni ya kila mtu ila ni muongozo kamili na muongozo huo unapatikana kwenye Quran na Sunna, Sasa haya sijui technology unayatoa katika lipi kwenye hiyo miongozo? Quran ishaweka sawa toka kuumbwa kwa Dunia mpaka mwisho wake hakuna kitu hakina jibu lake. Unachotakiwa kujua tu ni kwamba wewe ni maamuma unahitaji kusoma dini yako uijue.
 
Unaakili kuliko shekh sharif majini watu nyie ndio mpewe ushekh na umufti
Sio kina mazige na ponda wanawadharirisha sana
 
Naona wafia dini hapo juu wananiattack sana, naomba nitoe kauli yangu.

1.Hakuna sehemu niliyosema kuwa uislam uendeshwe kwa matakwa yangu

2. Hakuna nilipodeclare kwamba mimi ni msomi.

3. Hakuna mahali nilipozuia wafu kuzikwa haraka.

Ila nilitoa maoni yangu kulingana na Uislam na utamaduni wa Kiarabu kwamba hili jambo la kuwahisha kuzika nadhani ni kutokana na ukosefu wa teknolojia wakati huo kama mawasiliano, uhifadhi wa maiti na pia uchukuzi, ndio maana ikashauriwa kuwa maiti azikwe haraka, nimeandika neno imeshauriwa kwa sababu hakuna sehemu iliyoweka amri katika jambo hili.

Kuhusu uharaka wa kuzika hiyo ni perceptions za watu, kwa mfano mimi naweza kusema kuzika haraka ni ndani ya masaa mawili baada ya mtu kufa, mwingine akasema kuzika haraka ni baada ya masaa 24 ndugu wakishafika, mwingine anawesa kusema watoto wa marehemu wapo Marekani wanataka kushiriki ibada ya mazishi hivyo tutasubiri kwa siku tatu ili wafike, hiyo pia ni haraka kwa sababu hakuna maiti inayowekwa tu ndani halafu watu wakae nayo bila sababu.


Hayo yalikuwa ni maoni yangu, ssa tuje kwenu wafua dini mnijibu maswali haya mawili.

1. Tafsiri ya neno haraka nyinyi ni muda gani?
2. Mtume (S.a.w) alipofariki hakuzikwa siku hiyo hiyo, nini kilifanya wacheleweshe kuzika na je hapo hakukuwa na ulazima wa kufuata hiyo haraka mnayoipigia kelele.


NB:
Raha ya dini uamini kwa tafakuri sio kukaririshwa bila kufanya reasoning.
Kuna Uislam na kuna utamaduni wa kiarabu.
 
Ukifa kakamuliwe mavi
 
Wanawahi nn sasa???
 
Elimu haina mwisho ndugu yangu na kuniita maamuma kwa kejeli bado hujaniumiza as long as ni muislam na nimeelekezwa kuifuata elimu popote basi hakuna tabu nitazidi kusoma ila sio kukariri tu bila kufanya reasoning.

Nyinyi ndio mnaotuambiaga kitu fulani ni bidaa eti kwa kuwa hakikuwepo enzi za mtume (mmekaririshwa),ila nikikuuliza simu unayotumia hapo ilikuwepo wakati wa mtume? Sijui utajibu nini.
 
Wakati nimesikia alizimia ila kwa bahati mbaya wakamzika hivyohivyo.

Wewe una uhakika alikufa?
 
Toka lini Kusi na Kaskazi zikafanana,
Kila mtu ashike yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…