Mzee Tashrif kafariki leo na kazikwa leo. Waislam wanajua heshima, umuhimu na maana ya mazishi

Mzee Tashrif kafariki leo na kazikwa leo. Waislam wanajua heshima, umuhimu na maana ya mazishi

Mleta Uzi huu ana point moja yenye umuhimu katika wakati huu ambapo tumekuwa wengi na vifo ni vingi.
Pointi ni kuhusu muda mrefu unaotumika katika utaratibu wa mazishi ya Wakristo na gharama zake. Marehemu anaweza kusaliwa mara 3 hadi 4 tangu huko alikofia hadi kaburini. Mara nyingine waongoza ibada hawajali kabisa usalama wa waombolezaji wanaosafiri Kurudi walikotoka wakicheleweshwa na kulazimika kusafiri usiku. Sitaki kutaja wanaotumia madhishi kama fursa.
 
Elimu haina mwisho ndugu yangu na kuniita maamuma kwa kejeli bado hujaniumiza as long as ni muislam na nimeelekezwa kuifuata elimu popote basi hakuna tabu nitazidi kusoma ila sio kukariri tu bila kufanya reasoning.

Nyinyi ndio mnaotuambiaga kitu fulani ni bidaa eti kwa kuwa hakikuwepo enzi za mtume (mmekaririshwa),ila nikikuuliza simu unayotumia hapo ilikuwepo wakati wa mtume? Sijui utajibu nini.
Kwaanza Maamuma sio tusi, rejea hata kwenye kamusi za kawaida tu utaona, kuhusu kuitafuta Elimu nako kuna miongozo kwa kuwa hata uchawi, wizi navyo ni Elimu na inatafutwa.
Hili la bidaa ni ukosefu tu reasoning kwa wanaotumia mfano wako wa simu na ukiona mtu anatumia mfano huo usipate tabu kujiuliza kuhusu elimu yake, huyo ni katika watu wanahitaji kuelimishwa tu. Bidaa zina milango yake na ukipata muda jifunze acha kutetea hoja zako kwa fikra ndogo kiasi hicho.
 
Uislam hauendeshwi kwa mawazo na busara zako, uislam unaendeshwa kwa kufata Quran na Sunnah

Katika uislam mambo matatu yanatakiwa yafanywe haraka.
1.Mtu anapohitaji kuoa aozeshwe haraka
2.Mtu anapotaka kuslim asilimishwe haraka
3.Mtu anapo fariki azikwe haraka.

Huo ndo uislam kila kitu kimefundishwa katika uislam had staili ya Kutembea, kula&Kunywa, kuvaa, kulala, kuamka, kiiila kitu kimefundishwa na huo ndo unatakiwa uwe mwenendo wa waislam na siyo burasa zako na maoni yako.
Juzi hapa kulikuwa kuna mjadala kuhusu adhabu ya mtu aliye convert kutoka kwenye uislamu kwenda dini nyingine.

Maoni ya waislamu wengi waliyotoa kupitia Quran yalisema ni hukumu ya kifo kwa mtu huyo

Quran imesema atayetoka kwenye uislamu achinjwe, lakini naamini jambo hilo huwezi kulitekeleza kwa ndugu yako kipenzi eti kwakua tu Quran imesema.

Hiyo ndio sababu ya mdau kuweka opinions zake kuwa kuna muda anakuwa freethinker, anafanya kitu kulingana na utashi wake na sio kila muda ni kuifata Quran kwasababu kuna errors kama hizo.
 
Asilimia kubwa wanaojifanya kuifuata sana dini huishia kuishi maisha ya kiarabu ndani ya Africa, unakuta mtu amevaa kanzu nyepesi huko Mafinga hata koti hajavaa ukimuuliza ooh nimevaa mavazi ya kiislam, baridi inampuliza tu kama ngedere hajui kanzu ni vazi la jangwani kwenye joto.

Waafrica lazima tufahamu kuwa Uislam sio Uarabu, dini hizi sio asili yetu ila kwa kuwa tumeamua kuamini basi tunapaswa kufanya reasoning sio kila kitu walicholeta waarabu basi nasi tuking'ang'anie bila kujali hakiendani na mazingira yetu.

Kuna siku fulani nilienda kijiji fulani kusini huko, nikakuta misikiti miwili ila kila mmoja una msimamo katika jambo fulani, jambo lenyewe ni kuwa msikiti mmoja wao wametengeneza jeneza la chuma kwa ajili ya kubebeba maiti. Msikiti mwingine wao wametengeneza jeneza la mbao ndio wanabebea maiti wakati wakwenda kuzika. Sasa kuna baadhi ya waislam wakama kuswali kutoka msikiti wenye jeneza la chuma wakahamia msikiti wenye jeneza la mbao sababu eto hawa waliotengeneza la chuma wamefanya kitu ambacho hakipo katika dini, unabebeaje maiti kwa kutumia lichuma. Mgogoro ukawa mkubwa sana hata baadhi tuliokuwa tunajaribu kuwasihi tufanye tafakuri kwanza ya suala hilo then tupate muafaka bado tukaonekana hatuna elimu kama nikivyodhihakiwa hapa.

Lakini ukitafakari na ukisoma historia huko uarabuni walikuwa wakienda kuzika kwa kutumia kitanda cha mbao, wanazika kisha wanarudi na kitanda kwa ajili ya kutumika kuzikia wengine, na yote ilisababishwa na ukosefu wa miti ya kutosha huko uarabuni kwa sababu sehemu kubwa ni jangwa. Sasa leo hii unakuta mwafrica aliyezungukwa na miti kila sehemu akatengeneza jeneza badala ya kitanda, kutokana na kukua kwa teknolojia watu wakabuni majeneza ya chuma ili yadumu kwa muda mrefu lakini wanatofautiana hapo tu kisa wamekariri hawataki kufanya reasoning.

Zaidi ya yote hizi dini zote mbili tumeletewa tu Leo hii mimi Hassan nimchukie Jose wakati tunafanana rangi ya mwili mpaka nywele halafu nimpende Ali mpemba mwenye nywele za kiarabu na ngozi nyeupe kisa dini. usitokwe na mishipa ya shingo kwa jambo lisilo lako. Mungu hashindwi kitu angetaka angekuletea dini yako hapohapo kwa lugha yako na utamaduni wako.

Mimi ni muislam mwenye fikra huru ninayejua kutofautisha Uislam na Uarab.
 
Juzi hapa kulikuwa kuna mjadala kuhusu adhabu ya mtu aliye convert kutoka kwenye uislamu kwenda dini nyingine.

Maoni ya waislamu wengi waliyotoa kupitia Quran yalisema ni hukumu ya kifo kwa mtu huyo

Quran imesema atayetoka kwenye uislamu achinjwe, lakini naamini jambo hilo huwezi kulitekeleza kwa ndugu yako kipenzi eti kwakua tu Quran imesema.

Hiyo ndio sababu ya mdau kuweka opinions zake kuwa kuna muda anakuwa freethinker, anafanya kitu kulingana na utashi wake na sio kila muda ni kuifata Quran kwasababu kuna errors kama hizo.
Hata hizo hukumu zinatekelezwa basi kaka, waislam wangapi leo hii wanaenda kwa Mwamposa wanaconvert lakini hawa waarabu pori wapo kimya, wajaribu waone serikali itakachowafanya.
 
Mimi ni muislam lakini katika suala la kuwahisha mazishi niko kinyume na wengi.

Kuzika haraka mtu anapofariki sio muongozo wa quran bali ni maelekezo ya mtume wetu kutokana na wakati wao hakukuwa na teknolojia ya kuhifadhi maiti ili ikae muda mrefu.

Pia kutokana na joto la huko jangwani ikawa ni rahisi maiti kuharibika upesi, lakini pia kutokana na kukosa mawasiliano ya simu wakati huo ikawa sio rahisi kuwapelekea taarifa watu waliopo mbali ili wawahi mazishi, kwa hiyo mtume kwa hekima akasema kati ya mambo yanayotakiwa kufanywa haraka basi mazishi ni mojawapo.

Sasa kwa kuwa nyakati zimebadilika, teknolojia imekua kwa maana maiti inaweza kuhifadhiwa muda mrefu na pia wafiwa pengine wapo mbali na taarifa wamepata kupitia simu au whatsapp, je kuna ubaya gani kuchelewesha mazishi kwa sababu mazishi pia ni ibada mtu akihudhuria anapata thawabu.

Haya ni maoni yangu binafsi kwa sababu kuna Uislam na Uarabu, kun mambo inabidi kuyafuata kama Uislam unavyosema lakini pia kuna masuala ya utamaduni wa kiarabu ambao huku kwetu hauko applicable sio mbaya kama tutaacha huo utamaduni bila kuathiri dhima ya Uislam.
Mkuu kwa mujibu wa uislam mtu anapokata roho huwa anapata maumivu makali sana, na Yale maumivu hayakomi mpaka azikwe
Nadhani hii ni sababu kuu mtume wetu akatuasa swala hili liwe miongoni mwa Mambo ya haraka zaidi
 
Hekima ya jambo hilo tofauti na ulivyofikiri ,hata watu kuomboleza baada ya msiba nayo haitakiwi kisheria baada ya msiba inatakiwa watu wamwagikane wasiweke kiwingu kwa marehemu siku kibao, sasa fikiria kuhusu hekima ya jambo hilo unaweza kupata baadhi ya sababu zinazopelekea mtu kuwahishwa kuzikwa.
 
Hapo sasa nimekupata mkuu sio hawa wengine wanaishia kutoa tu lugha mbovu, kama suala la kuwahisha kuzika ni hekima ili kuzuia kuomboleza hapo nimekubali mkuu.
 
Dini ni itamaduni wa jamii na kila jamii ina tamaduni zake ambazo ndiyo msingi wa maisha yao ya kila siku. Kamwe taratibu za A haziwezi kuwa za B. Waislamu wabaki kwenye utamaduni wao na wakristo vivyo hivyo. Ni mbaya kuchelewesha maiti kwa mwislamu(ndiyo utamaduni na imani yao) ila siyo mbaya kwa wakristo (ndiyo utamaduni na maisha yao). Tusipangiane wala kulazimishana kila mtu abaki kwenye njia yake
Hajampangia wala kumlazimisha mtu.
 
Mimi ni muislam lakini katika suala la kuwahisha mazishi niko kinyume na wengi.

Kuzika haraka mtu anapofariki sio muongozo wa quran bali ni maelekezo ya mtume wetu kutokana na wakati wao hakukuwa na teknolojia ya kuhifadhi maiti ili ikae muda mrefu.

Pia kutokana na joto la huko jangwani ikawa ni rahisi maiti kuharibika upesi, lakini pia kutokana na kukosa mawasiliano ya simu wakati huo ikawa sio rahisi kuwapelekea taarifa watu waliopo mbali ili wawahi mazishi, kwa hiyo mtume kwa hekima akasema kati ya mambo yanayotakiwa kufanywa haraka basi mazishi ni mojawapo.

Sasa kwa kuwa nyakati zimebadilika, teknolojia imekua kwa maana maiti inaweza kuhifadhiwa muda mrefu na pia wafiwa pengine wapo mbali na taarifa wamepata kupitia simu au whatsapp, je kuna ubaya gani kuchelewesha mazishi kwa sababu mazishi pia ni ibada mtu akihudhuria anapata thawabu.

Haya ni maoni yangu binafsi kwa sababu kuna Uislam na Uarabu, kun mambo inabidi kuyafuata kama Uislam unavyosema lakini pia kuna masuala ya utamaduni wa kiarabu ambao huku kwetu hauko applicable sio mbaya kama tutaacha huo utamaduni bila kuathiri dhima ya Uislam.
Kwahiyo hizo sababu ulizosema wewe mtume naye aliainisha vile vile au niwewe tu unaleta.
 
Mkuu kwa mujibu wa uislam mtu anapokata roho huwa anapata maumivu makali sana, na Yale maumivu hayakomi mpaka azikwe
Nadhani hii ni sababu kuu mtume wetu akatuasa swala hili liwe miongoni mwa Mambo ya haraka zaidi
Vipi ukilipuka na bomu kama la Hiroshima na Nagasaki ukatoka vipande vipande

Sent from my SM-A035F using JamiiForums mobile app
 
Kwahiyo hizo sababu ulizosema wewe mtume naye aliainisha vile vile au niwewe tu unaleta.
Ni mimi tu nimeleta kutokana na kufanya reasoning, sio maneno ya mtume na hangeweza kuyasema wakati huo hayo niliyoyasema kwa kuwa hizo technology nilozosema hazikuwepo.
 
Hapana kulazimisha katika dini. Kwani Uongofu umekwisha pambanuka na upotofu. Basi anaye mkataa Shet'ani na akamuamini Mwenyezi Mungu bila ya shaka amekamata kishikio madhubuti, kisicho vunjika. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.
Al_baqarah 256
 
Hapana kulazimisha katika dinui. Kwani Uongofu umekwisha pambanuka na upotofu. Basi anaye mkataa Shet'ani na akamuamini Mwenyezi Mungu bila ya shaka amekamata kishikio madhubuti, kisicho vunjika. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.
Al_baqarah 256
Ila punguza ujuaji Mkuu,.... Unakosea unaposema wenzako hawafanyi reasoning, wakati kiuhalisia wewe ndiyo upo wrong.
Kwa mfano, Baljurashi amekuwekea hadithi inayotoa reasons za maiti kutocheleweshwa kuzikwa, ambapo hizo reasons hazihusiani na teknolojia wala Uarabu.

Sababu ishatolewa,.. lakini wewe unaendelea kuita wenzako eti hawafanyi reasoning..,

Sasa hapo, wewe na wao nani,... Asiyetumia reasoning?

Kuwa humble,.. na siku zote fahamu kwamba kwenye Mjuzi basi kuna Mjuzi zaidi.
 
Back
Top Bottom