Naona wafia dini hapo juu wananiattack sana, naomba nitoe kauli yangu.
1.Hakuna sehemu niliyosema kuwa uislam uendeshwe kwa matakwa yangu
2. Hakuna nilipodeclare kwamba mimi ni msomi.
3. Hakuna mahali nilipozuia wafu kuzikwa haraka.
Ila nilitoa maoni yangu kulingana na Uislam na utamaduni wa Kiarabu kwamba hili jambo la kuwahisha kuzika nadhani ni kutokana na ukosefu wa teknolojia wakati huo kama mawasiliano, uhifadhi wa maiti na pia uchukuzi, ndio maana ikashauriwa kuwa maiti azikwe haraka, nimeandika neno imeshauriwa kwa sababu hakuna sehemu iliyoweka amri katika jambo hili.
Kuhusu uharaka wa kuzika hiyo ni perceptions za watu, kwa mfano mimi naweza kusema kuzika haraka ni ndani ya masaa mawili baada ya mtu kufa, mwingine akasema kuzika haraka ni baada ya masaa 24 ndugu wakishafika, mwingine anawesa kusema watoto wa marehemu wapo Marekani wanataka kushiriki ibada ya mazishi hivyo tutasubiri kwa siku tatu ili wafike, hiyo pia ni haraka kwa sababu hakuna maiti inayowekwa tu ndani halafu watu wakae nayo bila sababu.
Hayo yalikuwa ni maoni yangu, ssa tuje kwenu wafua dini mnijibu maswali haya mawili.
1. Tafsiri ya neno haraka nyinyi ni muda gani?
2. Mtume (S.a.w) alipofariki hakuzikwa siku hiyo hiyo, nini kilifanya wacheleweshe kuzika na je hapo hakukuwa na ulazima wa kufuata hiyo haraka mnayoipigia kelele.
NB:
Raha ya dini uamini kwa tafakuri sio kukaririshwa bila kufanya reasoning.
Kuna Uislam na kuna utamaduni wa kiarabu.