Mzee wa Bwax ni msanii namba moja wa Singeli nchini. Msanii gani wa Bongo fleva wa kupambana naye jukwaani?

Mzee wa Bwax ni msanii namba moja wa Singeli nchini. Msanii gani wa Bongo fleva wa kupambana naye jukwaani?

Mkuu man fongo anajua sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwenye kupiga show za kibabe Shollo Mwamba na Mzee wa Bwax hakuna anayewafikia iwe bongo fleva ama hiphop hakuna anayewafikia, hapa nazungumzia kwenye kuamsha raia.
Shollo Mwamba akiwa jukwaani piga ua garagaza ni lazima uruke tu.

Ila msanii mkali kwa sasa kwenye game ya singeli ni Meja. Man Fongo ni mkali ila sio mkali kuliko wote.
 
Man fongo ndo baba lao monopoly inc,

Sent using Jamii Forums mobile app
Man Fongo mistari yake ni adimu sana.

"We tia mguu uzame ,mi ni kama mgema tulia sasa nikugeme ,usipime peme hizi ryhmes kama sime, tulia nikufinye nikubusu au nikusonye au nikutekenye ukicheka tuone mwanya

Huu ni mguu wa neema, Mc mchovu ninukuu upate vina ,zing mpaka ding hizi bifu za kiaina, dunia sio tamu kila siku watu wanazidi saga sumu, eti gemu ngumu? Au kichwa chako mpumbavu ndo kigumu kila nyimbo zako unawaimbia mademu zangu za kiarabu ona ninavyowahukumu .......,.........


Nani bado sijamtaja wahuni wangu, njoo kati nikuone jeshi langu........
 
princess ariana, Sholo mwamba kaanza kutoka kabla ya Man Fongo.

Fongo alikuwa DJ wa Sholo kabla na yeye kuamua kuanza kuimba.

Kuhusu Bwax na Dulla Makabila ,Makabila ana hits nyingi kuliko Bwax.

Hits za Makabila
1)Demu wako namba ngapi
2)Motoni kumedamshi
3)Dua
4)Hujaulamba
5)Sitaki kuoa mpaka nijue manila
6)Kuingizwa
7)Nikilewa nitakuwaje?



Hits za Bwax
1)Kisimu changu

2)Unaringa nini

3)Kisuli suli

4)Nyota yangu
 
ulioa mwanaume anapenda singeli ana vinasaba vya kula tigo ni mtazamo tu
 
princess ariana, Wasanii wa singeli hawapendani full kurogana .

Huyo huyo Bwax unayemtetea katoa nyimbo anamponda Dulla Makabila anachota nyayo zake, Sholo Mwamba anamuongelea vibaya, kamponda pia Man Fongo humo.
 
Sholo mwamba
Mczo morfan
Lajini
Pk
Kidene
Ha ha ha, Genero Taya a.k.a Kono La Jini sio [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Tatizo la PK Mr Konki na Kidene nyimbo zao zimejaa uvunjifu wa amani.

Sikiliza ngoma kama kimaskani ya Pk Sela Mr Konki mistari yake uone.

Baadhi ya mistari yake
"Manyungu wakija kwetu tunawatoboa, na zaga zao mfukoni tunafokoa .

Na panya road hawaelewi kwa Sana, na panya road wanawaza kukanda kumbe wanajulikana, sio poa lile jalamba la leo ,kila tunapopita kwa raia ni vilio, sio poa lile jalamba tuling'ata hadi utumbo mchana kinoma noma , silitaki lile jalamba la juzi watoto wamekimbizana kule wanaleta makuzi".

Huyo kidene naye nyimbo zake zote ni za maasi ,vurugu.

Sikiliza ngoma ya Zuna, mule anahamasisha vurugu kwa asilimia mia.
 
[emoji23][emoji23]Asa mkuu bongo unashangaa kurogana.
btw wanatuonyesha ushirikiano mzuri hata kama nyuma ya pazia yapo mengi
Wasanii wa singeli hawapendani full kurogana .

Huyo huyo Bwax unayemtetea katoa nyimbo anamponda Dulla Makabila anachota nyayo zake, Sholo Mwamba anamuongelea vibaya, kamponda pia Man Fongo humo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hance Mtanashati, Manfongo upepo ulimbeba sana Alivyotoa hauna na haina ushemeji. na vile wabongo wanapenda kukuza jambo inakua balaa.
Sholo yupo siku nyingi na nahisi ni miongoni mwa waimba singeli walioanzisha usafi.
Dula makabila nazikubali nyimbo zake 3 tu ile style yake ya kupause ilibamba sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Manfongo upepo ulimbeba sana Alivyotoa hauna na haina ushemeji. na vile wabongo wanapenda kukuza jambo inakua balaa.
Sholo yupo siku nyingi na nahisi ni miongoni mwa waimba singeli walioanzisha usafi.
Dula makabila nazikubali nyimbo zake 3 tu ile style yake ya kupause ilibamba sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa katika nyimbo za Man fongo ambazo ni mbaya Hauna na Hainaga Ushemeji ni mojawapo.

Tafuta nyimbo za Man Fongo kama vile.

1)Vijimambo

2)Twista

3)Watu Kibao

4)Taarifa Maalum

5)Disco Dancer

6)Nani bado sijamtaja

7)Namuamini Mungu
 
Wasanii walionifanya niipende singeli ni manfongo (hainaga ushemegi) na mzee wa bwax (nyimbo zote)...mzee wa bwax kwa sasa ni fire....

Ila kuna muhuni mmoja hajatajwa humu S.KIDE toto la mama Shamte, mdogo wake na Simbaaa...hahahaaa huyu muhuni nyimbo zake nikisikiliza naishia kucheka tu maana kutwa kazi kuimba watu tu..juzi kati alitoa moja kumuhusu harmonize. Baadaya ya kujitoa wasafi...😂
 
kwenye show hapa bongo hamna wakumfikia Sholo mwamba narudia tena hakunaaa

tujaribu kotofautisha mwenye hit song na anae amsha jukwaan

narudia tena hakuna wakumfikia sholo mwamba jukwaan

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukisema jukwaani Kuna madogo wengi wanaofanya vizuru sana mfano yule anaewapigisha magoti na kuwanyanyua(Pk Mr Konki) pia wapo wengine km mczo na kidene jaribu kufatilia matamasha ya mziki mnene.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee wa bwax ameachwa mbali sana meja kunta ukiangalia meja kunta mziki wake unapendwa na watu wote wake kwa waume watoto kwa wazee wadada kwa vijana...dogo amekuja na fleva ya tofauti sana taarabu+qaswida+bongo fleva+singeli pia dogo anaonekana alikuwa mtu wa kupenda sana kusoma vitabu tukufu vya dini ya kiislamu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom