Mzee wa miaka 75 auwa kwa mapanga kwenye kikao cha familia

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Mzee Thomas Filipi Silayo (75), mkazi wa Kijiji cha Mbomai Juu, Tarakea wilayani Rombo, amefariki dunia baada ya kushambuliwa kwa mapanga wakati wa kikao cha kifamilia kilichokuwa kikijadili mgogoro wa ardhi kati yake na ndugu zake.

Tukio hilo lilitokea Mei 8, 2026 katika Kijiji cha Wama, Kata ya Ubetu Kahe, ambapo marehemu alijeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo tumboni, mguuni na mkononi hali iliyosababisha kupoteza damu nyingi.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa, amesema marehemu alipelekwa kwanza katika Hospitali ya Karume Wilaya ya Rombo kwa matibabu ya dharura kabla ya kuhamishiwa Hospital ya rufaa ya Kanda KCMC ambako alifariki dunia Mei 9 akiwa anaendelea na matibabu.

Kamanda Maigwa anasema mtuhumiwa mkuu wa tukio hilo ni John Anselim Silayo, ambaye ni mtoto wa mdogo wa marehemu na alitoroka baada ya kutekeleza tukio hilo.

“Tunamtafuta mtuhumiwa ili akamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria,” amesema Kamanda Maigwa.

Soma Pia: Mwalimu Afariki Dunia baada ya kushambuliwa shambani Masasi - Mtwara kisa mgogoro wa ardhi

Binti wa marehemu, Elizabeth Silayo, anasema baba yake aliitwa kwenye kikao cha familia kwa lengo la kutafuta suluhu ya mgogoro wa mipaka ya shamba uliodumu kwa muda mrefu.
 
Watu wanakufa sana aisee
B729B2AF-C68C-4D81-8344-1447BA689505.jpeg
 
Ndugu ni umbwa!
 
Moshi na Arusha kaa mbali sana na Mali za Urithi, kule vijana waliobaki sio kama hawa wachapakazi unaona hapa Mjini na mikoani, kule kumejaa mambululazi yanayosubiri wazee wafe wauze Mali na ardhi
 
Back
Top Bottom