Nadhani nitumie fursa hii kujibu hii hoja kwa faida yako
BIN NUN na jamaa yangu
kavulata na wengine ambao ni ukweli usiopingika hawajui dhana ya mgombea huru.
Mfumo wa
Mgombea Huru (Private/Independent Candidate) ni mfumo wa kidemokrasia unaotumika katika nchi nyingi duniani, ikiwemo barani Afrika na mataifa makubwa yenye demokrasia komavu.
Kama nilivyotakiwa nijaribu kuorodhesha nchi zinazoruhusu Mgombea huru kwa ufupi:
- Afrika: South Africa, Kenya, Uganda, Ghana, Zambia, na Malawi.
- Mataifa Mengine: Marekani (USA), Uingereza (UK), Ufaransa, India, na Canada.
Ndugu yangu
BIN NUN , hivi unafahamu kuwa Kikatiba na kisheria, Tanzania ilishapewa uamuzi wa kimataifa kuhusu swala hili:
- Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR): Mwaka 2013, katika kesi iliyofunguliwa na marehemu Mchungaji Christopher Mtikila dhidi ya Serikali ya Tanzania, mahakama iliamua kuwa marufuku ya mgombea binafsi inavunja Haki za Binadamu na Mikataba ya Kimataifa ambayo Tanzania imesaini.
- Mahakama iliamuru Tanzania iruhusu wagombea binafsi, lakini mchakato wa kisheria na mabadiliko ya Katiba umekuwa ukipigwa danadana na serikali.
Faida Kuu za Kuruhusu Mgombea Huru
Kuna faida lukuki za Serikali kuruhusu Mgombea huru, ikiwa ni pamoja na:-
- Uhuru wa Mawazo na Uuwajibikaji: Kiongozi anakuwa anawajibika kwa wananchi waliommchagua na siyo kwa "Uvungoni mwa Chama" au msimamo wa Mwenyekiti wa Chama.
- Kudhibiti Nidhamu ya Woga (Party Whip): Inawaondolea wanasiasa hofu ya kufukuzwa vyama pale wanaposimamia ukweli au kuwasilisha kero za wananchi dhidi ya serikali iliyopo madarakani.
- Haki ya Kikatiba ya Kuchagua na Kuchaguliwa: Kila raia anapaswa kuwa na haki ya kugombea nafasi ya uongozi bila kulazimika kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa.
- Kuchechemua Uwajibikaji Bungeni: Hata kama bunge litakuwa na wabunge wengi wa chama kimoja, presence ya wagombea binafsi inaleta changamoto halisi ya kisiasa inayokilazimisha chama tawala kuwajibika.
- Fursa kwa Wataalamu na Wazalendo: Inatoa nafasi kwa watu wenye uwezo mkubwa (wataalamu, wanaharakati, viongozi wa kijamii) kuwatumikia wananchi bila kuingia kwenye siasa za majitaka za vyama.
Muhashimiwa (siyo Mheshimiwa)
BIN NUN na
kavulata niendelee au nisiendelee... au ngoja nilale