Mzee Warioba na hoja fikirishi ya Mwalimu Nyerere kutohutubia Kanisani

Kiranga, siku hizi hii lugha unayoandika ni lugha gani inatupa shida sisi wengine?
Vidole vyangu vina allergy na hewa chafu ya baadhi ya watu humu.

Ukiona hivyo karibu nitaondoka.

Nimekusawazishia usihitaji algorithms za Claude Shannon kunisoma.
 
Nadhani huu uhuni wa kutumia mimbari za nyumba za Mungu kutoa matamko ya kisiasa tumeanza kuuona kwa JK,kwa Mwendazake ilizidi! Yaani akipewa Mic ilikuwa ni kufoka mpaka kukashifu Watumishi wa Mungu!
Hayati Magufuli alitumia kanisa kuwaunganisha Watanzania na sio kutugawa! Kama hofu ya Mwalimu Kutumia Dini ilikuwa kuwagawa Watanzania basi Magufuli aliitumia dini kutuunganisha!

Nenda kamsikilize Shekhe Kishki ambae alitokwa ma Machozi juu ya upendo wa Rais Magufuli kwa Waislamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilimsikiliza vyema Waziri Mkuu mstaafu Mzee Joseph Sinde Warioba pale alipopewa nafasi ya kuhutubia nyumbani kwa Mwalimu Nyerere pale Msasani kama sehemu ya sherehe ya kufikisha miaka 100 ya hayati Mwalimu.

Aliongea kwa lugha nzuri kama mwanasheria na mtu muungwana. Akamuelezea Mwalimu Nyerere jinsi alivyokuwa akimfahamu tangu alipokuwa kijana kabisa. Tukumbuke kuwa mwaka 1961 Mzee Warioba alikuwa ni mmoja wa vijana waliokuwepo pale uwanja wa Uhuru siku ya tarehe 9 mwezi Desemba. Hivyo anamfahamu vyema hayati Mwalimu.

Akiwa anaendelea kujenga hoja ya unyenyekevu(humility) wa hayati Baba wa Taifa akaongelea suala moja lililoniacha nikiwa nimezama katika fikra nyingi aple aliposema kuwa Mwalimu Nyerere hakuwahi hata mara moja kuhutubia kanisani.

Nikaona kamera ikizungushwa na akaonyeshwa Amani Karume mdogo wake na rais wa zamani wa Zanzibar, macho yake yakawa yanatazama juu hewani kama alikuwa na mawazo fulani yaliyomjia kichwani muda huo.

Kwamba Mwalimu Nyerere alipenda mno kujishusha na hakulewa na madaraka.Siku zote alikuwa tayari kujiweka katika nafasi ya mtu wa kawaida pasipo uwepo wa dalili wala viashiria vya makuu, ni kama Mzee Warioba aliamua kusisitiza kwa viongozi wa sasa waendelee kujishusha wawe ni watu wa kawaida wasiwe ni Miungu watu.

Nikakumbuka miaka ile ya 1980 pale kanisani Saint Joseph Hayati Baba wa Taifa alikuwa siku moja moja akipenda kusali. Kilichokuwa kikituonyesha kwamba yeye ni rais ni kwamba kile kiti chake kirefu kilikuwa kikikaliwa na watu watatu tu. Yeye mwenyewe katikati kushoto mlinzi mmoja na kulia mlinzi mwingine. Hakuwa na mbwembwe za kutaka kupewa kipaza sauti wakati misa ikiwa inaendelea ili eti aanze kutoa maagizo mle mle kanisani.

Hoja kama hii ya Warioba ni nzito na pengine katika utu uzima wake alionao kwa sasa ni wakati muafaka kufikisha ujumbe kama ule ule aliousema Askofu Niwemugizi kwa Samia kule Kagera. Kwamba cheo chako kipo leo na kesho kinakwenda kwa mtu mwingine, hivyo tumia busara siku zote katika maamuzi yako.

Nakumbuka JK katika kumuongelea akasema kitu alichojifunza kwake ni kauli yake kwamba hoja hujibiwa kwa hoja na siku zote haipigwi bunduki. Kutoipiga bunduki hoja ni pamoja na kuwa na uwezo wa kujifanya wewe ni wa kawaida tu hata kama yanayosemwa dhidi yako yanaiumiza nafsi yako.

Pia ni kama ile picha maarufu ya Bilionea Bill Gates aliyoipiga akiwa kapanga foleni huko USA kavaa jeans yake kama vile ni mtu wa kawaida tu.

Anajishusha na kutojikweza siku zote, jaribu kumuweka Gates na pesa zake na ushawishi wake katika nafasi ya hawa matajiri wanaomiliki mabasi ya mikoani na vituo kadhaa vya kuuza petroli, namna wanavyotaka wanyenyekewe kama vile wao ndio wanaowapa binadamu wengine uhai na kuuondoa!.

Tutamkumbuka sana Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alikuwa ni mtu wa kawaida mwenye ucheshi mwingi na busara nyingi. Lakini ndani kabisa ya nafsi yake akiwa mtu wa kawaida kabisa.

Ukikutana nae pale ikulu katika zile koridoo karibu na yule Simba aliyekaushwa miaka ile anakuwekea mkono kichwani na kukuuliza hujambo mwanangu!?. Ni kama jana tu lakini inakaribia miaka 40 sasa.
'Phillipo Bukililo', sijkumbuki kama huwa ninakusoma hivi. Najua huwa ninakusoma mara nyingi tu hapa jukwaani, na pengine tuliwahi kuzozana juu ya jambo wakati fulani, (sikumbuki)! Itakuwa ni kuhusu JPM? Sijui.
Nakumbuka JK katika kumuongelea akasema kitu alichojifunza kwake ni kauli yake kwamba hoja hujibiwa kwa hoja na siku zote haipigwi bunduki. Kutoipiga bunduki hoja ni pamoja na kuwa na uwezo wa kujifanya wewe ni wa kawaida tu hata kama yanayosemwa dhidi yako yanaiumiza nafsi yako.
Hii hapa JK aliisema wakati gani mkuu 'Phillipo', unakumbuka?
Hili ndilo shina la heshima kuu aliyokuwa nayo Mwalimu, lakini nyakati hizi kuna watu wanalazimisha kuwa alikuwa "haambiliki."

Nikukumbushe pia na sifa nyingine ambayo siku hizi viongozi wetu hawataki isahaulike kwamba wanayo na kulazimisha watu wawatambue hivyo. Wao ni ma'Amiri Jeshi' wanaotaka watambuliwe hivyo, hata kama hakuna sababu kabisa ya kutaka watambuliwe kwa sifa hiyo.
Kuna sababu ya kujitangaza hivyo.

Ni nadra sana kumpata kiongozi mwenye haiba ile ya Mwalimu Nyerere popote duniani.
 
kila mwanadamu hakosi mazuri yake na kila mwanadamu hakosi mabaya yake..

Ukiamua kuelezea mazuri tu ya Adolph hittler basi naye unaweza kumuita mtakatifu....
 
Ukiamua kuelezea mazuri tu ya Iddi Amin basi naye anaweza kuwa malaika...kuna wakati nilikuwa na rafiki yangu kutoka Uganda, kila tukizungumzia siasa basi alikuwa akimsifia sana Iddi Amin..
 
Nyerere alihudumu kipindi cha mfumo wa chama kimoja.

Na hata kura alikuwa hashindanishwi na yoyote ndani ya CCM

Hata mzee Malecela pale St Alban Upanga utaratibu ulikuwa ni huo huo.

Mfumo wa vyama vingi unahitaji mambo mengi pia.

Huyo huyo Nyerere alimwingiza Mandela Ikulu wakati ameshastaafu, ingekuwa leo maneno yangekuwa mengi sana!
Hoja hapa hasa ni ipi inayohusiana na mada moja kwa moja?

Naona umeamua kukusanya mambo kadhaa yasiyohusiana na mjadala wa tabia ya Mwalimu Nyerere kama kiongozi ambaye hakutaka kuonyesha ukuu wa nafasi aliyokuwa anaishikilia kama rais.

Kuwa na siasa za vyama vingi kuna uhusiano gani na tabia ya uongozi wa mtu!
 
Nakumbuka JK katika kumuongelea akasema kitu alichojifunza kwake ni kauli yake kwamba hoja hujibiwa kwa hoja na siku zote haipigwi bunduki. Kutoipiga bunduki hoja ni pamoja na kuwa na uwezo wa kujifanya wewe ni wa kawaida tu hata kama yanayosemwa dhidi yako yanaiumiza nafsi yako.
Watanzania wanafiki sana. JK huyuhuyu aliyeona njia sahihi ya kupinga hoja ya Dr Uli ni kumng'oa kucha!
 
ni kweli Nyerere alikuwa ni mtu wa tofauti sana we fikiria miaka yote aliyokaa Ikulu alifanikiwa kuzaa mtoto wa nje ya ndoa mmoja tu

#mbowe sio gaidi
 
kila mwanadamu hakosi mazuri yake na kila mwanadamu hakosi mabaya yake..

Ukiamua kuelezea mazuri tu ya Adolph hittler basi naye unaweza kumuita mtakatifu....
Hata wewe ukiambiwa baba yako ni mchawi hukubali, lakini hilo halitoi mwonekano wa baba yako la kiujumla katika jamii katika mazuri yake na mabaya yake. Kama wingi wa jamii unaona baba yako kweli ni mchawi, wewe hata ungekataa vipi, jamii itamtambua hkwa sifa hiyo mzee wako. Siyo lazima kila mtu katika jamii akubali uzuri au ubaya wa mtu/kiongozi.
 
Mwalimu aliyaelewa na kuyaishi maandiko haya; kwamba; (Yesu) hakujiona kuwa Mungu ni kitu cha kushikamana nacho; akatwaa namna ya mtumwa akakaa kwetu. Pili, aliye mkubwa kwenu na awe mtumwa wa wote.

Pia kwenye dhehebu lake la Katoliki title rasmi ya Pope ni; the Servant of the servants of God. Hayo maeneo matatu (na mengine) aliyaishi sana Mwalimu.

... kwamba kama wakubwa hao including Jesus, his Lord and savior, walijishusha kwa kiwango hicho kwa wanaowaongoza, yeye (Nyerere) ni nani ajikweze? Pamoja na kuwa mkuu wa nchi, Nyerere alijishusha akaishi maisha ya mwananchi wa kawaida no matter wakati mwingine itifaki zilitaka vinginevyo. Sio leo, mijitu mingine inalazimisha kupewa mike madhabahuni itoe maelekezo simply ni RC, DC, au wana madaraka fulani!
 
K U J I P E N D E K E Z A

Wanasiasa wanatumia Dini kama kivuli ili kuficha madhaifu yao.
 
Nilimsikiliza vyema Waziri Mkuu mstaafu Mzee Joseph Sinde Warioba pale alipopewa nafasi ya kuhutubia nyumbani kwa Mwalimu Nyerere pale Msasani kama sehemu ya sherehe ya kufikisha miaka 100 ya hayati Mwalimu.

Aliongea kwa lugha nzuri kama mwanasheria na mtu muungwana. Akamuelezea Mwalimu Nyerere jinsi alivyokuwa akimfahamu tangu alipokuwa kijana kabisa. Tukumbuke kuwa mwaka 1961 Mzee Warioba alikuwa ni mmoja wa vijana waliokuwepo pale uwanja wa Uhuru siku ya tarehe 9 mwezi Desemba. Hivyo anamfahamu vyema hayati Mwalimu.

Akiwa anaendelea kujenga hoja ya unyenyekevu(humility) wa hayati Baba wa Taifa akaongelea suala moja lililoniacha nikiwa nimezama katika fikra nyingi aple aliposema kuwa Mwalimu Nyerere hakuwahi hata mara moja kuhutubia kanisani.

Nikaona kamera ikizungushwa na akaonyeshwa Amani Karume mdogo wake na rais wa zamani wa Zanzibar, macho yake yakawa yanatazama juu hewani kama alikuwa na mawazo fulani yaliyomjia kichwani muda huo.

Kwamba Mwalimu Nyerere alipenda mno kujishusha na hakulewa na madaraka.Siku zote alikuwa tayari kujiweka katika nafasi ya mtu wa kawaida pasipo uwepo wa dalili wala viashiria vya makuu, ni kama Mzee Warioba aliamua kusisitiza kwa viongozi wa sasa waendelee kujishusha wawe ni watu wa kawaida wasiwe ni Miungu watu.

Nikakumbuka miaka ile ya 1980 pale kanisani Saint Joseph Hayati Baba wa Taifa alikuwa siku moja moja akipenda kusali. Kilichokuwa kikituonyesha kwamba yeye ni rais ni kwamba kile kiti chake kirefu kilikuwa kikikaliwa na watu watatu tu. Yeye mwenyewe katikati kushoto mlinzi mmoja na kulia mlinzi mwingine. Hakuwa na mbwembwe za kutaka kupewa kipaza sauti wakati misa ikiwa inaendelea ili eti aanze kutoa maagizo mle mle kanisani.

Hoja kama hii ya Warioba ni nzito na pengine katika utu uzima wake alionao kwa sasa ni wakati muafaka kufikisha ujumbe kama ule ule aliousema Askofu Niwemugizi kwa Samia kule Kagera. Kwamba cheo chako kipo leo na kesho kinakwenda kwa mtu mwingine, hivyo tumia busara siku zote katika maamuzi yako.

Nakumbuka JK katika kumuongelea akasema kitu alichojifunza kwake ni kauli yake kwamba hoja hujibiwa kwa hoja na siku zote haipigwi bunduki. Kutoipiga bunduki hoja ni pamoja na kuwa na uwezo wa kujifanya wewe ni wa kawaida tu hata kama yanayosemwa dhidi yako yanaiumiza nafsi yako.

Pia ni kama ile picha maarufu ya Bilionea Bill Gates aliyoipiga akiwa kapanga foleni huko USA kavaa jeans yake kama vile ni mtu wa kawaida tu.

Anajishusha na kutojikweza siku zote, jaribu kumuweka Gates na pesa zake na ushawishi wake katika nafasi ya hawa matajiri wanaomiliki mabasi ya mikoani na vituo kadhaa vya kuuza petroli, namna wanavyotaka wanyenyekewe kama vile wao ndio wanaowapa binadamu wengine uhai na kuuondoa!.

Tutamkumbuka sana Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alikuwa ni mtu wa kawaida mwenye ucheshi mwingi na busara nyingi. Lakini ndani kabisa ya nafsi yake akiwa mtu wa kawaida kabisa.

Ukikutana nae pale ikulu katika zile koridoo karibu na yule Simba aliyekaushwa miaka ile anakuwekea mkono kichwani na kukuuliza hujambo mwanangu!?. Ni kama jana tu lakini inakaribia miaka 40 sasa.
Sawa tunakushukuru i kwa porojo zako
Lakini wenye akili tunataka kwa nguvu katiba mpya
 
Nyerere halikuwa haambiliki mfano ni wakati wa Azimio LA Arusha. Alipingwa na kina Kambona, bibi titi na wenzake he walifanywa nini wakati huo mpaka sasa hawaaminishwi kwa watanzania kama no mashujaa waliondelea baada ya Uhuru.

Si kweli nyerere hakuwahi kuhutubia Kanisani isipokuwa alikuwa hatanabaishi mambo ya serikali wakati wa ibada za kawaida lkn alifanya hivyo kwenye ibada za kualikwa kama mgeni Rasmi.

Warioba was trying to portray something behind the reality.
 
Ni pengo kubwa nyerere,mkapa na magufuli hawapo
Nchi imebaki kutafunwa
Magufuli na Lukuvi walikuwa wanahutubia kanisani, na inawezekana kabisa mzee Walioba alikuwa anamzungumzia Magufuli.
 
Nadhani huu uhuni wa kutumia mimbari za nyumba za Mungu kutoa matamko ya kisiasa tumeanza kuuona kwa JK,kwa Mwendazake ilizidi! Yaani akipewa Mic ilikuwa ni kufoka mpaka kukashifu Watumishi wa Mungu!
Usimsahau na Lowasa
 
Back
Top Bottom