Mzee Warioba: Siyo lazima Mbunge aitwe Mheshimiwa

Mzee wetu Waziri Mkuu Mstaafu Joseph Sinde Warioba amesema kulazimisha watu wakuite wewe kuwa ni mheshimiwa mbunge, mheshimiwa waziri ,mheshimiwa diwani huko ni kuweka matabaka kwenye jamii ya watanzania.

Hii inapingana na Naibu Spika alivyogombana na Mbunge wa Mbeya Mjini Mbilinyi. Tulia alilazimisha kuitwa Mheshimiwa Naibu Spika

Hakika mzee Warioba ni tegemeo la watanzania kwa busara.

Chanzo dakika 45 itv.
Kama hawa wabunge ww Mwendazale nao ni waheshimiwa?
 
Acha uwongo. Nyerere hakuwa anaitwa mtukufu Rais. Alikuwa akiitwa Ndugu Rais. Kenya walikuwa wanamwita mtukufu Rais Arap Moi, wote watanzania tulikuwa tunashangaa. Wakati huo nikiwa chipukizi, nilimvisha Mwalimu skafu mara 2, mara zote nilimwita Ndugu Rais ..... Mwinyi ndiye kwa mara ya kwanza aliitwa Mtukufu Rais, na wabunge wakajiita waheshimiwa.
Wakati Mzee Waryoba akiwa PM, au? Kwa hiyo Utukufu na Uheshimiwa umeasisiwa yeye akiwa PM?
 
Mzee wetu Waziri Mkuu Mstaafu Joseph Sinde Warioba amesema kulazimisha watu wakuite wewe kuwa ni mheshimiwa mbunge, mheshimiwa waziri ,mheshimiwa diwani huko ni kuweka matabaka kwenye jamii ya watanzania.

Hii inapingana na Naibu Spika alivyogombana na Mbunge wa Mbeya Mjini Mbilinyi. Tulia alilazimisha kuitwa Mheshimiwa Naibu Spika

Hakika mzee Warioba ni tegemeo la watanzania kwa busara.

Chanzo dakika 45 itv.
Hahahahahahaha wanavyopenda kuabudiwa sasa hawawezi kukubali kabisa.
 
sahihi kwa 100%, wanasiasa akishaitwa mheshimiwa tayari anajiona yeye ni mtu maalum sana wakati kiuhalisia ni tofauti.

kuna watu kibao huku kitaa wapo smart sana kichwani kuliko hako kakikundi kanakoongozwa na Ndugai pale Dodoma!
 
Siku moja Tulia akawa anamlazimisha Sugu amuite mh naibu spika nilidhani ni sheria kumbe wapi ni vapour tu.

Leo mzee kawavua nguo sijui kama Ndugaye hatompiga mkwara mbuzi
 
Ni uqendawazimu mtu kutaka uotwe mheshimiwa. Sasa mtunkama Ndugai, ambaye kika mwenye akili anamdhaharau kutokana na unafiki wake, hata akiitwa mheshimiwa ndiyo ataheshimiwa? Si atabakia zuzu tu kama alivyo?
Hajitambui lkn tayari alishasema kuwa ana faili mirembe.
 
Nakumbuka wakati wa Mwalimu hakukuwa na neno Mheshimiwa kwa mtu yeyote, viongozi wote walikuwa wakiitwa Ndugu kasoro Rais ambaye alikuwa pia akiitwa Mtukufu Rais! Baada ya Mwalimu Nyerere kutoka madarakani, ukaibuka mjadala Bungeni Wabunge wakitaka waitwe Waheshimiwa (Honorable). Mwalimu alipinga lakini wakamwambia mbona Uingereza wanaitwa Honorable. Wakapitisha sheria wakaanza kuitana Waheshimiwa. Siyo wakati wa akina Waryoba kweli?? Tafuta wazee watukumbushe. Ila wakati Waryoba ni PM Rais wake alikuwa akiitwa Mtukufu Rais, na Mzee sikumsikia akisema kitu kwa kuwa labda alikuwa na kitu.
Unataka kusema kuwa mzee Warioba leo anayaongea haya kwakuwa hana kitu?
 
Nakumbuka wakati wa Mwalimu hakukuwa na neno Mheshimiwa kwa mtu yeyote, viongozi wote walikuwa wakiitwa Ndugu kasoro Rais ambaye alikuwa pia akiitwa Mtukufu Rais! Baada ya Mwalimu Nyerere kutoka madarakani, ukaibuka mjadala Bungeni Wabunge wakitaka waitwe Waheshimiwa (Honorable). Mwalimu alipinga lakini wakamwambia mbona Uingereza wanaitwa Honorable. Wakapitisha sheria wakaanza kuitana Waheshimiwa. Siyo wakati wa akina Waryoba kweli?? Tafuta wazee watukumbushe. Ila wakati Waryoba ni PM Rais wake alikuwa akiitwa Mtukufu Rais, na Mzee sikumsikia akisema kitu kwa kuwa labda alikuwa na kitu.
Mtukufu ilikuwa ni enzi za Mzee Ruksa. Nyerere hakuwa akitumia title ya Mtukufu
 
Nakumbuka wakati wa Mwalimu hakukuwa na neno Mheshimiwa kwa mtu yeyote, viongozi wote walikuwa wakiitwa Ndugu kasoro Rais ambaye alikuwa pia akiitwa Mtukufu Rais! Baada ya Mwalimu Nyerere kutoka madarakani, ukaibuka mjadala Bungeni Wabunge wakitaka waitwe Waheshimiwa (Honorable). Mwalimu alipinga lakini wakamwambia mbona Uingereza wanaitwa Honorable. Wakapitisha sheria wakaanza kuitana Waheshimiwa. Siyo wakati wa akina Waryoba kweli?? Tafuta wazee watukumbushe. Ila wakati Waryoba ni PM Rais wake alikuwa akiitwa Mtukufu Rais, na Mzee sikumsikia akisema kitu kwa kuwa labda alikuwa na kitu.
Nyerere hakuwahi kuitwa 'mtukufu rais', hiyo ya kuitana 'mtukufu' ilianzishwa wakati wa awamu ya pili.
 
Back
Top Bottom