Mzee Warioba: Siyo lazima Mbunge aitwe Mheshimiwa

Mbona viongozi wa dini anaitwa kwa Cheo Chao kisha jina.
Mf: Mchungaji D, Askofu D, shehe D nk.
Kwani Hawa wabunge tusiwaite Mb. K na sio kulazimisha tuanze na Mheshimiwa wakati wengine hawana hiyo heshima
Hakika hawa watu wanataka kujikweza bila kuwa na sifa hizo.

Wengi wao wana sifa ambazo wengi wetu mitaani tunawazidi kwa sifa mzuri .

Wanalichafua bunge letu hao wataka sifa.
 
Mtukufu aliyeshuhudia Yesu wanavishana Pete. Spika aandikiwe kitabu cha uongozi wake.Eti anakaa ofisini na fimbo halafu KATIBA anakanyaga kama zulia.
Huyu naye ndiye sababu ya watu kukosa imani na bunge lenyewe
 
Uko sahihi. Miaka ya 1990s Waryoba alikuwa alikuwa mbunge wa jimbo la Bunda kabla ya kuenguliwa mahakamani na Stephene Wasira wa NCCR wakati huo. Kipindi hicho wabunge walikuwa wameshaanza kuitwa waheshimiwa. Wasira alimunyang'anya uheshimiwa Waryoba baada ya kushinda mahakamani kesi ya uchaguzi mkuu kwenye jimbi la Bunda.
 
Unapomuita mtu"MHESHIMIWA" unakuwa umejiridhisha kuwa anastahili heshima kwa jinsi anavyoendesha maisha yake katika jamii anayoishi!! Heshima haiombwi bali hutengenezwa na muhusika.

Leo hii kumuita Ndugai "MUHESHIMIWA ni kumkejeri kwani hastahili heshima kwa jinsi jamii inavyo muona!!
 
Si kweli kuwa hapa Tanzania Rais alikuwa akiitwa Mtukufu! Ni Kenya Rais Mzee Kenyatta alikuwa akiitwa Mtukufu lakini hapa Tanzania tulimwita Ndugu Rais Nyerere.
Mwinyi aliitwa Mtukufu Rais, Mkapa ndio akakataa hiyo title.
 
Warioba ndiyo kundi la Nyerere ambao walipinga but walishindwa na hilo kundi la wengi..
Sikumbuki Waryoba kulipinga hilo. Waryoba alikuwa na madaraka angeweza kuyatumia kulizuia. Hata Mwalimu nadhani aliacha tu, angetaka angelizuia. Kumbuka aliweza kuzuia G55 ya akina Njelu Kassaka asingeshindwa kuzuia huu uheshimiwa japo kwa muda.

Neno Ndugu lilikuwa likinasibishwa na siasa za Ujamaa wa Ulaya Mashariki. Ndugu ilikuwa kama opposite ya Kabaila, Beberu, Kupe, Bepari, Bwanyenye, Mnyonyaji, Kaburu, nk.
Baada ya Azimuo la Zanzibar maneno kama Beberu, Kabaila, Kupe, nk yalipoteza umaarufu hivyo na mwenza wake yaani Ndugu nalo likayeyuka. Tukaingia kwenye msamiati wa maneno yanayoendana na Uchumi wa Kibepari wa nchi za Ulaya Magharibi ambapo maneno kama HE, Hon, Bar, Lord, nk ndiyo yanatumika.
 
Hiyo vita yao haijawahi kuisha!
 
Yaani mtu/mbunge umwajiri wewe mwananchi kupitia kura yako halafu umwite mheshimiwa? Khaa
Wivu upo wapi hapo
Halafu mbaya zaidi ni pale ambapo wala hujamuajiri (hujampigia kura) kaingia zake kimagumashi then anakomaa umuite muheshimiwaaa khaaa...
 
Naona unapenda kuabudu binadamu wenzako
 
Na wake zao pia ni waheshimiwa. Niliwasikia wakisema "Karibu Sana Mheshimiwa Mama Mwenyekiti wa Kijiji".
 
Walazimishe kuitwa mazuzu mimi nitakuwa no 1 kuwaita[emoji1787]ila kumuita mbunge au raisi muheshimiwa ni ngumu kwelikweli labda awe na akili na utendaji wa hali ya juu sana
 
Walazimishe kuitwa mazuzu mimi nitakuwa no 1 kuwaita[emoji1787]ila kumuita mbunge au raisi muheshimiwa ni ngumu kwelikweli labda awe na akili na utendaji wa hali ya juu sana
Nitakuunga mkono
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…