ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 83,659
- 90,151
My Take
Safi sana Wasira unajua sana kuwakera 😂😂👇👇
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira, leo Juni 11, akizungumza na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Nyasa, mkoani Ruvuma, ametumia jukwaa hilo kuwakumbusha wanachama wa CCM nchini kuwa kwa sasa mgombea pekee mwenye ridhaa ya kupewa kipindi kingine cha uongozi wa miaka mitano ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mhe. Wasira alisisitiza kuwa wagombea wengine wanaotafuta nafasi za Ubunge na Udiwani bado wanapaswa kusubiri mchakato rasmi wa mchujo, ambao utaanzia katika ngazi ya Kata hadi Taifa, kama taratibu za chama zinavyoelekeza.
Aidha, aliwakumbusha wajumbe wa CCM kujiepusha na vitendo vya rushwa katika mchakato wa uchaguzi ndani ya chama, akieleza kuwa tabia ya kuchagua wagombea kwa misingi ya rushwa ni sawa na kupora haki za wale wanaostahili na wanaokubalika na wananchi.