Mzee Yusuph aamua kuachana na muziki na kumrudia Mungu wake

Mzee Yusuph aamua kuachana na muziki na kumrudia Mungu wake

Ni kweli kabisa amepoteza kundi la watu wengi sana, na mimi huu msemo nilikuwa nasema kila siku kila nikiangalia show zake
Amepoteza kwa vipi? Kwa kuwafanya watu wafanye dhambi zipi?

Mkuu naomba ubainishe dhambi anazojutia Mzee Yusufu.
 
Huyu aache unafiki Allah hadhiakiwi..kama kweli kaacha mziki agawe na Mali zote alizochuma kwenye huo mziki kwa masikini...mziki umemfanya aoe wanawake wanne Leo anaketa nyodo!?mziki sio mbaya ila tabia zake tu..!!
 
Mungu wako kibao wengine hadi wanatia shaka.Yusuph kafanya kazi halali iliobarikiwa na Mola hadi kupata mafanikio makubwa kiutajiri.Leo huyo huyo Mungu aliyempa mafanikio hayo yeye na wenzake wanadai ni mafanikio haramu.Mzee Yusuph anapaswa kuzitupilia mbali mali zake zote alizochuma kiharamu.Yaani kuimba tu na kuburudisha watu Mungu wa Mzee Yusuph hapendi!!!.
 
Kimempata kipi Mzee? Mbona kawa kama wale wakristu waliotenda dhambi mpaka shetani akawafukuza kisha ndio kwenda kanisani na kutangaza kuokoka? Anawaasa Waislam waache mziki?? Dooh! Sasa wabaki akina nani tena na wakati wanamziki zaidi ya 90% ni waislam, alafu hivi kumbe kuimba mziki ni dhambi?
 
Analia nini sasa???

IMG_3139.JPG
Ndio na mimi najiuliza
 
Imeandikwa kwenye Surat ipi katika qur'an?

Ni mtume ama swahaba yupi alipinga muziki?

Tarawe unaizungumziaje?
Hahahaha lazima utakua wa upande wa pili wewe maana si kwa maswali haya ya kijahili,
Na kama ni muislam hlf hujui kama mziki ni haram basi una matatizo.

anyway, waislam wenyewe wanajua na kuelewa so wewe potezea.

Kuhusu taraweh nimeshindwa kuelewa unataka niizungumzie kwa mantiki ipi?
Maana Taraweh ni katika swala za sunna ziswaliwazo kipindi cha Ramadhan tukufu,
Sasa sijui ulitaka kufaham nini.
 
Tatizo ni kwamba,ukimkimbia shetani na yeye hua anaenda kwa MUNGU kudai vyake,kama ni pesa magari na majumba atayadai then amuache atafute kivingine huko alikoelekea
 
Ndio, muziki ni haramu kwa waislam
Kwani kaswida sio muziki? Ni vizuri tusijivue ufahamu kwa sababu ya ushabiki tukatupa akili pembeni. Mimi sio mshabi wa taarabu wala bongo fleva. Ila ni vizuri kujua maana ya muziki kuwa ni sauti zilizopangiliwa zenye kuleta vionjo. Hili tumejifunza darasa la pili. Hivyo ni vizuri kusema ameachana na uovu ambao bila shaka alikuwa anaufanya kupitia taarabu. Pia ni vizuri kusema wanamuziki wengi wanaingia katika mtego wa uovu kutokana na umaarufu wao. Kwa hiyo alichokifanya mzee Yusufu ni kutupa jongoo na mti wake jambo ambalo ni jema bila kuleta vitisho kwa washabiki wake aliowauzia santuri. Hekima zaidi ilipaswa.
 
Umenena vema mkuu, ila ndio mambo ya iman hayo kama ni katazo ni katazo tu hata kama halina mantiki
 
Back
Top Bottom