Mzee Yusuph aamua kuachana na muziki na kumrudia Mungu wake

Mzee Yusuph aamua kuachana na muziki na kumrudia Mungu wake

Mungu pia alimuumba shetani, ina maana shetani ni rafiki yako kisa nyote mmeumbwa na Mungu???
Shetani aliumbwa kama malaika lkn baadae alikuja kumuasi Mungu, akirudi kuwa mwema atakuwa rafiki
 
Mombasa, Kenya
Mzee Yusuf almaaruf kama Daktari wa Mapenzi aliyejulikana kama ''Mfalme'' wa Modern Taarab, habari za ''kustaafu'' kwake zimewatatiza sana na kuwatia simanzi wapenzi wake wa Mombasa, Kenya. Hakika wapenzi wake ndani na nje ya Tanzania watamkosa katika burudani waipendayo.

Pengine Mzee Yusuf anaweza kubadilisha ''maamuzi yake magumu'' na katika siku chache zijazo baada ya kutafakari kwa kina maombi kedekede ya mashabiki wake bila kusahau ufadhili wa mamilioni ya shillingi anaweza kurudi kuendelea kusuuza nyoyo za wapenzi wa modern Taarab.

Taarab: Nitadumu nae : Mapenzi yawe ya Daima : Yarabi yawe Salama

Source: Swahili Taarab
 
Mkuu ilisemekana ile ajali ya five star miaka ile iliyoua wasanii wengi yeye ndio aliitengeneza kwa hofu ya kufunikwa na marehemu ISSA KIJOTI aliefariki kwenye ajali hiyo maana marehemu alikuwa anakuja juu sana kisanii. Na hili lilipelekea Mzee kukataa kushiriki wimbo uliotungwa na wasnii wa taarab wa kumuenzi marehemu Issa.
hauwezi ukawa serious wewe, yaan issa kijoti amfunike mzee yusuph dah umemdharirisha sana mzee yusuph,kabla hujamfikia mzee kuna vigingi kama amigo, mohamedi ally mtu pori ndio ukutane na fundi mwenyewe mzee yusuph
 
Kwa hakika ukitazama kufuru ya matendo yaliyo katika hiyo video ya Mkuki live na pia mengine anayoyajua Mzee Yusuph mwenyewe aidha kwa kuyafanya mwenyewe au kuyashuhudia yakifanyika katika kumbi alipokuwa akipiga muziki wake basi ana kila sababu ya kulia kwa jinsi kipaji chake kilivyotumika vibaya na kuwafanya wengi kumkosea Mungu wao. Mungu amsimamie katika huo uamuzi wake wa kumrejea Mungu.
Ni kweli kabisa amepoteza kundi la watu wengi sana, na mimi huu msemo nilikuwa nasema kila siku kila nikiangalia show zake
 
Nadhani dini zetu za kikristo na kiislam zinasema kwamba tukifanya toba ya kweli mungu anatusamehe dhambi zetu..katika biblia tunafundishwa pia dhambi zetu zijapokua nyekundu kama damu mungu atazifanya nyeupe kama theluji..sasa nyie mnaomhukumu mzee mwacheni kama kufanya toba ya kweli mungu wake wala hawezi kukumbuka tena yale aliyokua akiyafanya cha msingi ni yeye mzee kurudi kwa mungu kiukweli ukweli na asiwe anatafutia kiki tu
 
Mkumbuke Mungu wako siku za ujana amefanya uamuzi sahihi sana kwa muda muafaka .
 
hauwezi ukawa serious wewe, yaan issa kijoti amfunike mzee yusuph dah umemdharirisha sana mzee yusuph,kabla hujamfikia mzee kuna vigingi kama amigo, mohamedi ally mtu pori ndio ukutane na fundi mwenyewe mzee yusuph
Anamtia hasira ili arudi kwenye gem
 
Anataka watu wenye CD zake waache kusikiliza, lakni hasemi kama atawafidia maana hizo CD walinunua kwa hela zao!
 
Kha ametajirika anaona taarabu haina deal,akifilisika asirudi tena kwenye gemu,tatizo ili nyimbo zao ziheat wanashinda kwanza kwa waganga ,ndo maana analia,i thank God huwa sisikilizi ma nyimbo yao ambayo mpaka wakazindikwe kwanza ndo watoe
Unasikiliza zipi.?!
 
Kuwaambia watu walionunua CD zake kwa pesa kuacha kupiga na kusikiliza nyimbo zake,ni changamoto.Ama sivyo na yeye apeleke utajiri wake kuendeleza misikiti na pia kugawa kwa maskini.Vinginevyo auchune tu hadi watu wenyewe wataacha kuzisikiliza nyimbo zake!
 
hauwezi ukawa serious wewe, yaan issa kijoti amfunike mzee yusuph dah umemdharirisha sana mzee yusuph,kabla hujamfikia mzee kuna vigingi kama amigo, mohamedi ally mtu pori ndio ukutane na fundi mwenyewe mzee yusuph
Unaelewa maana ya neno "ilisemekana" siku maanisha kuwa "alifunikwa" maana hata hiyo ajali sijui kama ni kweli ilitengenezwa na mzee Yusuph. Halafu huwezi kuusemea moyo wa mtu, huwezi kujua nani atiaye hofu mtu mwingine bali mtu mwenyewe ndie ajuaye hofu yake inasababishwa na nini/nani.
 
Back
Top Bottom