Mzee Yusuph aamua kuachana na muziki na kumrudia Mungu wake

Mzee Yusuph aamua kuachana na muziki na kumrudia Mungu wake

asije tu akawa mpiga ramli.
tatizo la hawa wenzetu, akiwa mcha mungu sana huwa na nafasi kubwa ya kufuga majini au kuwa mganga wa kienyeji.

wakristo wao... akiwa mcha mungu sana kwa maana ya ulokole wa kupitiliza, anakuwa mjinga mjinga... hawana tofauti na mazombi.
 
Nani alimwambia kuimba in dhambi, analia kwa sababu amefanya sana ushirikina Wa kuwaua wenzake, agawe Mali zake kwa yatima ili tuamini anachosema otherwise hizo ni cinema tu, investment zote zimetokana na kuimba taarabu, that is to say, na hizo investment zote ni haramu.
 
Dah....kapata kazi mpya? Sasa hizo CD/ DVD tuzifanye nini?? Angetangaza kununua CD/DVD zake zote ambazo ziko mikono ni mwa watu ili wasizipige tena...
 
Aombe Na radhi nyimbo zake zenye matusi Na kujaza mashoga kwenye show zake otherwise atakuwa mnafiki
 
Kha ametajirika anaona taarabu haina deal,akifilisika asirudi tena kwenye gemu,tatizo ili nyimbo zao ziheat wanashinda kwanza kwa waganga ,ndo maana analia,i thank God huwa sisikilizi ma nyimbo yao ambayo mpaka wakazindikwe kwanza ndo watoe
Umejuaje?
 
Assalaamu alaykum warahmatullahi wabarakaatuh

BREAKING NEWS

Aliyekuwa Mfalme na gwiji wa muziki wa taarabu Afrika mashariki MZEE YUSUF ameamua kuachana na mziki na kumrudia Allah.

Mzee Yusuf ametangaza Nia yake hiyo leo ijumaa tarehe 12-08-2016 Muda mfupi baada ya kumaliza kuswali swala ya ijumaa ktk msikiti wa ilala bungoni (Masjid Taqwa)

Alizungumza huku akibubujikwa na machozi mengi Mzee Yusuf amemuomba Allah amsamehe madhambi yake yote pamoja na kuwaomba waumini wote wamuombee msamaha kwa Allah. Kadhalika amewaomba wanamuziki wengine ambao ni waislamu kuachana na muziki na kuzitumia fani zao walizonazo ktk kutangaza na kusifia Shamaail za bwana mtume muhammad (s.a.w).

Gwiji huyo wa zamani wa taarabu amewaomba watu wote waliokuwa na Cd zake majumbani mwao kuacha kupiga nyimbo zake na wakikaidi wafahamu madhambi yote yatakuwa juu yao kwani yeye hivi sasa anafanya toba kwa Allah.

Pia amevitaka vituo vyote vya televisheni na redio kuacha kupiga nyimbo zake kwani yeye Hana dhimma hiyo Tena. Ikumbukwe hali kama hii ilishawahi kutokea kwa aliyekuwa msanii wa bongo fleva SUMA LEE kuamua kuachana na mziki na sasa ni mpenzi mkubwa wa mtume muhammad (s.a.w)

Yaa rabbi awape tawfiiq wanamuziki wote wa kiislamu waachane na muziki pamoja kutupa mwisho mwema wao pamoja nasi in shaa Allah.

Hakuweza kuendelea kuongea zaidi ya maneno hayo na kuangua kilio kilichomsababishia maneno kutoweza kutoka mdomoni mwake.
Iwe ni wito wa kiimani au soko limegomba lakini vipi aamuuru watu wasi sikilize CD zake na mpaka kuapiza ili hali aliziweka sokoni na akachuma fedha? nadhani ingekuwa busara kama amedhamiria hayo angeita kila mwenye CD yake aipeleke mahali atakapo teua yeye arejeshe fedha kwa kila CD vinginevyo itakuwa si haki bali dhuluma kesha vuna hela za watu halafu awanyanganye haki yao nakuanza kujiliza hilo sijapata kulisikia,na kila alicho kipata kupitia chumo lile ambalo sasa analiona haramu basi akiweke wakfu au akitoe kwa Yatima ndipo tutamuelewa.
 
Mie Nitammisi Kweli!Naipenda Ile Nyimbo yake anayoimba:"helua,helua,helua.."sijui huwa anamanisha nini?
 
Binafsi huwa sisikilizi,labda zikiwa zinapigwa mitaani.Masikio hayana pazia,fally sijawahi sikia nyimbo yake hata moja,Koffi nilisikia shamkwale na ile prends la photo sijui selfie.

Mnafiki mkubwa wewe
 
Iwe ni wito wa kiimani au soko limegomba lakini vipi aamuuru watu wasi sikilize CD zake na mpaka kuapiza ili hali aliziweka sokoni na akachuma fedha? nadhani ingekuwa busara kama amedhamiria hayo angeita kila mwenye CD yake aipeleke mahali atakapo teua yeye arejeshe fedha kwa kila CD vinginevyo itakuwa si haki bali dhuluma kesha vuna hela za watu halafu awa nyanganye haki yao nakuanza kujiliza hilo sijapata kulisikia,na kila alicho kipata kupitia chumo lile ambalo sasa analiona haramu basi akiweke wakfu au akitoe kwa Yatima ndipo tutamuelewa.
Ni ajabu sana. Kwamba anawaamuru mashabiki wake waliojinyima vihela vyao kiduchu na kununua cd na DVD zake zilizojaa shombo la muziki wake huku yeye hazungumzii atakachofanya juu ya mali zote alizochuma kwa kutumia mamilioni ya fedha zilizotokana na hizo hizo CD na DVD zenye shombo lile lile la muziki wake. Na bora hiyo safari yake aliyoianza iende vizuri kwani yakimshinda na kurudi tena kwenye muziki itakuwa aibu sana kwake.
 
Habari za jioni wanajamvi.
Taarifa nilizozipata punde zinasema mfalme huyo wa taarabu anaacha rasmi mziki huo na kumrudia mungu.
Mungu amjaalie wepesi afanikiwe katika dhamira yake

UPDATES;

Mzee Yusuph ameamua kuachana ma Muziki na kumrudia Mungu wake na amewataka watu wote wamsamehe ili apate msamaha kwa Mola wake.

Mzee Yusuph Ameapa kuto kujihusisha na Muziki na kutaka Nyimbo zake zisipigwe tena kwenye Media zote. Mzee Yusuph alionekana analia kwa uchungu katika msikiti wa Bongoni Ilala na kujutia yale aliyokuwa akiyafanya enzi za Ujahili wake.

Hongera zake kwa kuachana na huu muziki wa kike.
 
Hizi nyingine zinaitwa Paranoia na watu wengi wanaomwamini Mungu wa Saudi Arabia wana hii kitu. Ukiwasikiliza Sana waarabu utakufa masikini, yaani aache kupiga pesa kwasababu za kipuuzi. Subiri awe Shehe Ubwabwa wa Bungoni huko.
Hapana atakuwa Mchungaji feki mpenda wake za watu,mzee wa misukule .....ma
 
Ndiyo sababu mimi na bolingo tu nyimbo zenyewe zinapendwa na mashoga tu, bora umeacha na mungu akusamehe.
 
Dah, sasa tutapata jembe kama Mzee kweli? Utunzi yumo, uimbaji usiseme, vyombo ndo kabisaaaaaaaaaaaaa ukianza na kinanda!! Mungu alimtunuku sana ndugu yetu huyu ingawa hatujui yamemsibu yepi! Allah Akbar...!! God is Great..!!
Alah akbar!!! huwa naogopa sana kila nikisikia mtu anatamka, sijui sababu ya kuwa kafr!!!?
 
Back
Top Bottom