Scorpio Me
JF-Expert Member
- Aug 2, 2016
- 6,119
- 7,934
Sa unataka kujua ili iweje ka c mshabiki[emoji53]Hawa kina Kijoti kulikoni? Maana mimi kwenye taarabu sina ninalolijuwa na si mshabiki hata chembe wa muziki huu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sa unataka kujua ili iweje ka c mshabiki[emoji53]Hawa kina Kijoti kulikoni? Maana mimi kwenye taarabu sina ninalolijuwa na si mshabiki hata chembe wa muziki huu.
Na hela alizochuma, nyumba alizojenga kwa ajili ya mziki??Kwetu sie.
Hapo chacha, sijui na wake zake wataacha kuimbaKishakusanya za kutosha kwa miaka mingi, sasa ndiyo anagundua kama ni dhambi. Arudishe basi na pesa zote alizopata alipokuwa akitenda dhambi ya kuimba nyimbo mbali mbali za taarab.
HahahaaaaaaAliyekuwa Mfalme na gwiji wa muziki wa taarabu Afrika mashariki MZEE YUSUF ameamua kuachana na mziki na kumrudia Allah.
Mzee Yusuf ametangaza Nia yake hiyo leo ijumaa tarehe 12-08-2016 Muda mfupi baada ya kumaliza kuswali swala ya ijumaa ktk msikiti wa ilala bungoni (Masjid Taqwa)
Alizungumza huku akibubujikwa na machozi mengi Mzee Yusuf amemuomba Allah amsamehe madhambi yake yote pamoja na kuwaomba waumini wote wamuombee msamaha kwa Allah. Kadhalika amewaomba wanamuziki wengine ambao ni waislamu kuachana na muziki na kuzitumia fani zao walizonazo ktk kutangaza na kusifia Shamaail za bwana mtume muhammad (s.a.w).
Gwiji huyo wa zamani wa taarabu amewaomba watu wote waliokuwa na Cd zake majumbani mwao kuacha kupiga nyimbo zake na wakikaidi wafahamu madhambi yote yatakuwa juu yao kwani yeye hivi sasa anafanya toba kwa Allah.
Pia amevitaka vituo vyote vya televisheni na redio kuacha kupiga nyimbo zake kwani yeye Hana dhimma hiyo Tena. Ikumbukwe hali kama hii ilishawahi kutokea kwa aliyekuwa msanii wa bongo fleva SUMA LEE kuamua kuachana na mziki na sasa ni mpenzi mkubwa wa mtume muhammad (s.a.w)
Yaa rabbi awape tawfiiq wanamuziki wote wa kiislamu waachane na muziki pamoja kutupa mwisho mwema wao pamoja nasi in shaa Allah.
Hakuweza kuendelea kuongea zaidi ya maneno hayo na kuangua kilio kilichomsababishia maneno kutoweza kutoka mdomoni mwake.
NB: ukitaka kujua ibliis huwa hapendi kuona watu wakiwa kwenye njia sahihi subiri comments hapa chini za ibilisi waliobaki ambao jambo hili limewakera na litawakera sana
Amiiim mkuuAcha atubu akhera pazito mkuu..kaona mbali sana huyu jamaa..Allah atupe mwisho mwema sote.
Mziki wa taarabu umeharibiwa sana siku hizi. Ulikua miongoni mwa aina za mziki zenye maadili ya hali ya juu.
Hawa wanaojiita waimba modern taarabu wakaharibu sifa ya taarabu. Taarabu sasa inatia aibu, huwezi kwenda kwenye show kama unaijua asili hasa ya taarabu ya enzi zile.
Kuna yule anajiita mashauzi, anakoipeleka taarabu ni hatari sana.
Kwa muimba taarabu halisi kama akina Patricia Hilal hawawezi kusimama na kulia kujutia kazi zao, walifanya mziki wenye maadili sana.
Ukisoma Quran hata kula na kijiko ni haram."..... Hakika mziki ni shetani...."
Iwe Qaswida au Dufu vyote ni kharamu.
Tunaposema Mungu ni muumba wa vyote ina maana vipaji vya mziki havihusiki?Hujaambiwa muziki ni haramu ila kile ukitoacho kwa kupitia muziki ndicho haramu,Je una uhakika Mungu alitoa vipaji vya mziki,unasoma wapi au umepata wapi hili
Mkuu ilisemekana ile ajali ya five star miaka ile iliyoua wasanii wengi yeye ndio aliitengeneza kwa hofu ya kufunikwa na marehemu ISSA KIJOTI aliefariki kwenye ajali hiyo maana marehemu alikuwa anakuja juu sana kisanii. Na hili lilipelekea Mzee kukataa kushiriki wimbo uliotungwa na wasnii wa taarab wa kumuenzi marehemu Issa.Niulize mara ngapi?
Kasoma nyakati, kupiga shoo moja 2,000,000 sasa hivi atapata wapi wakati FM Academia wanapiga bonanza la bure Toroka uje?
Hakuumba mziki ila alitoa maarifa ya kutengeneza vyombo vya muziki,ktk utumiaji ndio tatizoTunaposema Mungu ni muumba wa vyote ina maana vipaji vya mziki havihusiki?
mi naona kastaafu, maana kashalamba vitamu vyote
Bwana weeeee, unapomkataa shetani yakatae na mambo yake. Huwezi kuendelea kulamba fedha za trade mark ya shetani huku unajifanya ni wa Mungu.Kama Imani yake ina Mungu wa kweli,Huyo Mungu huondoa magugu taratibu shambani asije haribu na ngano pamoja hivyo vyote vilivyochumwa katika anasa/haramu vitaisha na vya halali vitabaki,tusubiri tutashuhudia hapa,Mungu sio dikteta kwamba hakupi muda wa toba kamili na malipizi
Tunaacha taratiiiibuBwana weeeee, unapomkataa shetani yakatae na mambo yake. Huwezi kuendelea kulamba fedha za trade mark ya shetani huku unajifanya ni wa Mungu.
Labda tu Mzee Yusufu angetoa angalizo kwa wafuasi wake kwamba 'alikuwa akifanya dhambi kwa hiyo nao waache'
Hainaga ushemejiMan Fongo atawastaafisha wengi