Mzee Yusuph aamua kuachana na muziki na kumrudia Mungu wake

Mzee Yusuph aamua kuachana na muziki na kumrudia Mungu wake

Naaam!mungu ampe wepesi ktk njia njema aliyoichagua!,mi pia nataman kuachana na maov nifanyayo hivo nanyi tamanin kulejea kundini"NAIHUSIA NAFSI YANGU NA YAKO PIA"
Maa shaa Allah, weka nia ya dhati na Allah mwingi wa rehma atakuongoza katika njia iliyonyooka.
 
Naona umevaa umungu kwa kutoa mashart ya kumsamehe
Astaghafirullah!! usinibabatize mambo nisiyo na uwezo nayo, maneno hayo sijayatunga mimi bali ni maamrisho kutoka kwa Mtume wetu Muhammad (s.a.w), nami nimefanya kutoa elimu kwa ndugu zangu walioghafilika.
 
Kwa hakika ukitazama kufuru ya matendo yaliyo katika hiyo video ya Mkuki live na pia mengine anayoyajua Mzee Yusuph mwenyewe aidha kwa kuyafanya mwenyewe au kuyashuhudia yakifanyika katika kumbi alipokuwa akipiga muziki wake basi ana kila sababu ya kulia kwa jinsi kipaji chake kilivyotumika vibaya na kuwafanya wengi kumkosea Mungu wao. Mungu amsimamie katika huo uamuzi wake wa kumrejea Mungu.
 
"..... Hakika mziki ni shetani...."
Iwe Qaswida au Dufu vyote ni kharamu.
Inawezekana ni kweli usemayo, maana nilikuwa nina rafiki yangu ustaadh mmoja hivi chuoni, yeye alikuwa haudhurii sherehe zote za waisilamu wenzake kwa sababu zilikuwa zina kangoma kanapigwa. Hii kitu bado ina ubishani miongoni mwa waisilamu, huku kingine kinacholeta ubishi kikiwa ni kusherehekea Maulid ya mtume
 
Kuna mijitu minafiki sana kama hiki kizee! Umesha shiba hela haramu halafu leo uje useme unamrudia Mungu? arudishe na hzo hela basi haramu alizo kuwa anazi chikicha
 
Inawezekana ni kweli usemayo, maana nilikuwa nina rafiki yangu ustaadh mmoja hivi chuoni, yeye alikuwa haudhurii sherehe zote za waisilamu wenzake kwa sababu zilikuwa zina kangoma kanapigwa. Hii kitu bado ina ubishani miongoni mwa waisilamu, huku kingine kinacholeta ubishi kikiwa ni kusherehekea Maulid ya mtume
Kuna Muislam na Muumini,
Muumini sharti afate aliyoyaamrisha Allah (s.w) na kuacha aliyoyakataza,
Pia sharti afate muenendo mzima wa maisha ya mtume wetu Muhammad (s.a.w)

Sasa Allah ametukataza mziki, Mtume pia hakuwahi kucheza wala kuimba mziki, hapo mtabishana nini tena jamani, hilo lipo wazi wala halina shaka ndani yake.

Mtu akifanya atafanya kwa matamanio ya nafsi yake ila sio kwa maamrisho ya dini yake.
 
Mziki wa taarabu umeharibiwa sana siku hizi. Ulikua miongoni mwa aina za mziki zenye maadili ya hali ya juu.

Hawa wanaojiita waimba modern taarabu wakaharibu sifa ya taarabu. Taarabu sasa inatia aibu, huwezi kwenda kwenye show kama unaijua asili hasa ya taarabu ya enzi zile.

Kuna yule anajiita mashauzi, anakoipeleka taarabu ni hatari sana.

Kwa muimba taarabu halisi kama akina Patricia Hilal hawawezi kusimama na kulia kujutia kazi zao, walifanya mziki wenye maadili sana.
 
Back
Top Bottom