G TARIMO
Member
- Jul 23, 2025
- 30
- 22
Wadau wote wa Wajamvini habari za muda huu
Mara nyingi nikiwa kwenye daladala, hukutana na wanafunzi wadogo wa shule za msingi na sekondari wakiwa wamebeba mabegi mazito sana yenye madaftari na vitabu vingi. Hali hii hunisikitisha hasa nikifikiria umri wao mdogo na namna wanavyobeba mizigo hiyo kwenye mabega yao.
Nauliza:
1. Kwa kawaida, hawa wanafunzi huwa na vipindi vingapi kwa siku hadi kulazimika kubeba madaftari mengi kiasi hiki?
2. Je, mzigo huu mkubwa wa kila siku hauwezi kusababisha matatizo ya mgongo au athari nyingine za kiafya kwa muda mrefu?
3. Kuna suluhisho lolote ambalo shule, wazazi, au serikali wangeweza kulifanyia kazi ili kupunguza mzigo huu kwa wanafunzi?
Na kama kuna walimu humu Jamvini, naomba mtupatie mwanga kidogo:
Kwa siku huwa mnafudisha vipindi vingapi?
Kuna nini kinachowazuia kuwaruhusu watoto kubeba madaftari ya vipindi vya siku hiyo tu?
Na kama ratiba hubadilika, kwa nini wanafunzi wasipewe taarifa mapema ili wasibebe mzigo mkubwa usio wa lazima?
Ni jambo dogo lakini linaweza kuwa na athari kubwa kwa maisha ya watoto wetu hapo baadae.