Mzigo Mkubwa wa Madaftari kwa Wanafunzi Je, Hii Haileti Madhara ya Kiafya Kwenye matatizo ya mgongo

Ile Elimu ya zamani watu walistukia mnakuwa waelewa sana mnaanza kuhoji sasa hii nayo ninjia yakuwavilingisha siunajua wasokotaji niwajanja
 
Wadau wote wa Wajamvini habari za muda huu

Mara nyingi nikiwa kwenye daladala, hukutana na wanafunzi wadogo wa shule za msingi na sekondari wakiwa wamebeba mabegi mazito sana yenye madaftari na vitabu vingi. Hali hii hunisikitisha hasa nikifikiria umri wao mdogo na namna wanavyobeba mizigo hiyo kwenye mabega yao.

Nauliza:

1. Kwa kawaida, hawa wanafunzi huwa na vipindi vingapi kwa siku hadi kulazimika kubeba madaftari mengi kiasi hiki?

2. Je, mzigo huu mkubwa wa kila siku hauwezi kusababisha matatizo ya mgongo au athari nyingine za kiafya kwa muda mrefu?

3. Kuna suluhisho lolote ambalo shule, wazazi, au serikali wangeweza kulifanyia kazi ili kupunguza mzigo huu kwa wanafunzi?

Na kama kuna walimu humu Jamvini, naomba mtupatie mwanga kidogo:

Kwa siku huwa mnafudisha vipindi vingapi?

Kuna nini kinachowazuia kuwaruhusu watoto kubeba madaftari ya vipindi vya siku hiyo tu?

Na kama ratiba hubadilika, kwa nini wanafunzi wasipewe taarifa mapema ili wasibebe mzigo mkubwa usio wa lazima?

Ni jambo dogo lakini linaweza kuwa na athari kubwa kwa maisha ya watoto wetu hapo baadae.
Nimesoma heading tu, uko sahihi kabisa na hiyo Hali ulishawahi nikuta mm mwenyewe binafsi

Kuna haja ya wazazi kupata ratiba ya masomo shuleni na kuamua mwanafunzi abebe madaftari yepi kwenda nayo shule Kwa siku husika
 
Ile Elimu ya zamani watu walistukia mnakuwa waelewa sana mnaanza kuhoji sasa hII nayo ninjia yakuwavilingisha siunajua wasokotaji niwajanja
Elimu ya zamani na saiv imekua nivitu viwili tofauti kabsa, tukiendelea kwa style hii ya kubeba madaftari kama gunia la viazi watoto wetu watakuja kupata shida ya mgongo sana huko mbeleni
 
English medium zilikuja kwajili yakutenganisha matabaka mkajidai wabishi nanyie mnapoleka watoto wenu
 
Inapaswa watoto wabebe daftari za homework ya siku hiyo tu. Madaftari mengine yawe yanabaki shuleni mpaka ikikaribia mitihani. Kikubwa shule iwe na sehemu maalumu ya kutunza madaftari ya watoto.
Sio kwa mazingira ya Tanzania hii, hasahasa shule za umma.
 
94 hakukuwa na masomo mengi ya kuchosha mwili kiasi hiki
Hakuna ulicho elewa, matoto ya siku hizi hata yanalima kweli shule ? Au yanalia lia tu.. kubeba madaftari inakuja na michozi humu shensi kabisa
 
Nimesoma heading tu, uko sahihi kabisa na hiyo Hali ulishawahi nikuta mm mwenyewe binafsi

Kuna haja ya wazazi kupata ratiba ya masomo shuleni na kuamua mwanafunzi abebe madaftari yepi kwenda nayo shule Kwa siku husika
Na kingine pia waalimu wazingatia ratiba ya vipindi kwenye ufundishaji sio unakuta leo ni vipindi vinne labda , Historia , kiswahili, Uraia na Hisabati
Tuseme lambda mwalimu wa Historia amepata dharura ajaje ndo anatokea mwalimu wa Kingereza anaingia darasani hii haijakaa sawa kabsa kama mwalimu ajafika wanafunzi wajisomee ilo somo
 
Sio kwa mazingira ya Tanzania hii, hasahasa shule za umma.
Umenikumbusha kitu pia inakuaje shule za private ndo zinafanya vizuri uki,compare na za government hata kimazingira pia private ndo iko vizuri swali. Je private wana,ela kuwazidi Gvmnt au ni vipi 🤔
 
Wanapata madhara makubwa sana na wengine huwa vilema kabisa.
Dr Gwajima angekuja humu aliongelee hili jambo.

Watoto wanateseka sana
Mbona nchi zingine wanaacha shule? Kasoro homework tu?

Huu ni unyanyasaji na kuwapa ulemavu tu watoto dhaifu
 
Shida sana kwakweli na wanavyobeba ivyo sidhani kama wakifika darasani wanaweza kufundishwa kitu na kuelewa watakua wamechoka hoi nikusinzia tu darasani hili jambo ni lakua serious kabsa wizara na yenyewe itilie mkazo
 
Matatizo kama haya huwa hawayaoni kwa sababu hata waliopo Bungeni hawana Habari
Wanaomba kura kwa unyenyekevu ila mambo ya msingi wako kimya

Wahusika kimya
 
Wadau wote wa Wajamvini habari za muda huu

Mara nyingi nikiwa kwenye daladala, hukutana na wanafunzi wadogo wa shule za msingi na sekondari wakiwa wamebeba mabegi mazito sana yenye madaftari na vitabu vingi. Hali hii hunisikitisha hasa nikifikiria umri wao mdogo na namna wanavyobeba mizigo hiyo kwenye mabega yao.

Nauliza:

1. Kwa kawaida, hawa wanafunzi huwa na vipindi vingapi kwa siku hadi kulazimika kubeba madaftari mengi kiasi hiki?

2. Je, mzigo huu mkubwa wa kila siku hauwezi kusababisha matatizo ya mgongo au athari nyingine za kiafya kwa muda mrefu?

3. Kuna suluhisho lolote ambalo shule, wazazi, au serikali wangeweza kulifanyia kazi ili kupunguza mzigo huu kwa wanafunzi?

Na kama kuna walimu humu Jamvini, naomba mtupatie mwanga kidogo:

Kwa siku huwa mnafudisha vipindi vingapi?

Kuna nini kinachowazuia kuwaruhusu watoto kubeba madaftari ya vipindi vya siku hiyo tu?

Na kama ratiba hubadilika, kwa nini wanafunzi wasipewe taarifa mapema ili wasibebe mzigo mkubwa usio wa lazima?

Ni jambo dogo lakini linaweza kuwa na athari kubwa kwa maisha ya watoto wetu hapo baadae.
Hili swali nimejiuliza sana!
Wakati mwingine inanifikirisha sana hata kuanza kujudge uwezo wa kufikiri wa waalimu wetu, mdogo angu kila siku anabeba daftari zaidi ya 10 pamoja na vitabu nikimuuliza kwanini anasema Mwalimu x kasema madaftari yake yote kuanzia form 1 tuwe tunabeba (sasa yuko form 2). Anasema pia kuna waalimu wanataka madafyari yao yabebwe kila siku plus vitabu
Hii nchi sijuwi inashida gani kwa kweli, walimu wanapaswa kubadilika waanze kufikiria kama watu wazima na kama professionals wa taaluma zao.
Nawasilisha!
 
Matatizo kama haya huwa hawayaoni kwa sababu hata waliopo Bungeni hawana Habari
Wanaomba kura kwa unyenyekevu ila mambo ya msingi wako kimya

Wahusika kimya
Kazi yao nikupiga piga makofi tu huko bungeni na pia watoto wao hawasomi izi shule
 
Back
Top Bottom