Mzozo wa Mpaka Kati ya Thailand na Cambodia Uendelea kwa Siku ya Tatu

Mzozo wa Mpaka Kati ya Thailand na Cambodia Uendelea kwa Siku ya Tatu

Fascinating

Senior Member
Joined
May 14, 2025
Posts
146
Reaction score
351
Mzozo wa mpaka kati ya Thailand na Cambodia umeingia siku ya tatu, huku pande zote mbili zikiendelea kurushiana risasi na silaha za moto. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa wito wa kwanchi hizo kujizuia kulipa mashumbulizi. Cambodia imeitaka Thailand “kusitisha mapigano mara moja” bila masharti, kama alivyosema balozi wao wa Umoja wa Mataifa, Chhea Keo, baada ya mkutano wa faragha wa Baraza hilo Ijumaa, uliohudhuriwa na wawakilishi wa Cambodia na Thailand.
1753509950540.jpeg


Mapigano makali yalianza Alhamisi, yakihusisha ndege za kivita, mizinga, vifaru, na wanajeshi wa ardhini, yanayosababishwa na mzozo wa muda mrefu wa mpaka. Hadi sasa, Cambodia imeripoti raia mmoja, mzee wa miaka 70, ameuawa, na wengine watano wamejeruhiwa katika mkoa wa Oddar Meanchey. Thailand pia imesema zaidi ya watu 138,000 wamehamishwa kutoka maeneo ya mpaka, huku wameripoti vifo 15, raia 14 na askari mmoja, pamoja na majeruhi 46, wakiwemo askari 15.
IMG_2429.jpeg


Jeshi la Thailand lilisema mapigano yalianza tena katika maeneo matatu asubuhi ya Ijumaa saa kumi jioni (2100 GMT Alhamisi), huku wanajeshi wa Cambodia wakitumia silaha nzito, mizinga ya ardhini, na mifumo ya roketi za BM-21 maarufu kama Sabasaba hapa Tanzania. Thailand ilijibu kwa kushambulia maeneo ndani ya mpaka wa Cambodia kwa kutumia moja ya ndege 6 za aina ya F16 ilizozirusha katokana na mzozo huo huku ikidai kuwa ni inafanya “mashambulizi yanayofaa kusaidia,” kulingana na uhitaji wa jeshi lao.

1753510003725.jpeg


Kabla ya mkutano wa Umoja wa Mataifa, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Thailand, Nikorndej Balankura, alisema mapigano yalikuwa yameanza kupungua hadi alasiri ya Ijumaa, akiongeza kuwa Bangkok iko tayari kwa mazungumzo, lakini kwa msaada wa Malaysia.

Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kupatikana suluhu kwa amani, huku dunia ikiangalia kwa karibu mzozo huu unaoweza kuathiri zaidi usalama wa eneo hilo. Pande zote mbili zimeonyesha nia ya kuzungumza, lakini hali bado ni tete huku mapigano yakiendelea.

New York Times
Reuters
CGNT
 

Attachments

  • 1753509875424.jpeg
    1753509875424.jpeg
    119 KB · Views: 40
Hapa tanzania wapo kusifu mama naona kuna dalili ya malawi na upande rwanda hipo siku
 
Uzi huu hauna wafia dini 😃😃😃
 
Ukiona mwenzako ananyolewa zako.......
Jiandae kisaikolojia kabla ya yote mengine utaongezea......
 
Back
Top Bottom