Mzungu anawaambia wahamiaji wa kiafrika msije Uingereza "Don't come to England"

Hata sisi wenyewe hatutaki wenzetu waje ,sema tu tunaogopa kusema,mwisho tunabaki kupigana vijembe tu mitandaoni,binadamu bhana
 
Inaposemwa kama kaharibu Demokrasia ni hivi, odds zote ziko kwake, kwa sababu Mihimili miwili ambayo inatakiwa imsimamie yeye ndio anateua wakuu wa hiyo Mihimili + Tume ya Uchaguzi + Wasimamizi wa Uchaguzi + Watangaza matokeo ya Uchaguzi.

Hizi advantages zilikuwepo tangu enzi ya Mwalimu ili havikuwa amplified kama sasa. Mzee baba kaamua kutumia hizi advantages kwa faida yake kwa sababu kwa asili na kama binadamu mwingine hapendi ushindani.
 
Kwa asili ya mwafrika sio mtu wa kukaa mezani, anahitaji shuruti ili msonge, bahati mbaya tukaletewa mifumo ya kisiasa kama demokrasia inayoweka uwepo wa bunge, aliyeleta mfumo huo alizingatia asili ya watu husika akajua ukiwawekea huu mfumo hawataweza hawatafika kwahiyo watakwama, lakini pia itakuwa rahisi kwao kupenyeza mamluki halafu kuna mambo wapinzani watapinga tu kwa kuwa watapigwa bao, mfano mkitaka mambo ya ndege moja mkajadili bungeni Chadema watahujumu tu maana ilikuwa ajenda yao, ukizitekeleza wao watakuja na ajenda gani tena, mnakwama.

Msomi anafelisha taifa kizembe kabisa bila kujua, hapo tu nimeshadiss mifumo miwili kwa pamoja, wa elimu na wa kiutawala
 
British man tells African migrants to "Don't come to England"

Katika video hapo chini mzungu anawaambia wahamiaji wa kiafrika kuwa wasiende Uingereza kwa kuwa wana wahamijai wa kutosha na watu wao ambao inabidi wawatumikie
View attachment 1563148
Waingereza walivyokuja Afrika nani aliwakataza?

Kuna video moja comedian Trevor Noah alikuwa anatania na kusema wakoloni sasa hivi ni zamu yao kupokea watu kutoka makoloni yao ya zamani.

Mkuki mtamu kwa nguruwe, kwa binadamu mchungu.
 

Kuambia wakoloni warudishe walichoiba sio utumwa.

Hio misaada yao ya kutufumba macha wakitulawiti hatuja waomba. Ni wanasiasa ndio wanakula hiyo misaada.

Bila shaka tuaneza kujenga kwetu Afrika tukituma wachache huko kulinda maslahi yetu kutoka inje.
 
Paragraph ya kwanza ulikuwa ushauri mzuri kabisa, baadaye ukaona haitoshi ukaamua kuingiza na siasa.
Unaambiwa hata ROMA haikujengwa kwa siku moja.
 
Paragraph ya kwanza ulikuwa ushauri mzuri kabisa, baadaye ukaona haitoshi ukaamua kuingiza na siasa.
Unaambiwa hata ROMA haikujengwa kwa siku moja.
Hakuna siasa ila ndio ukweli. Mtaishia kusema hivyo hivyo kwa kutoa mfano wa Roma, mkishituka ni kiama kimewadia.
 
Maendeleo Ya Unyang'anyi Hii Planeti haiwezi himili.
 
British man tells African migrants to "Don't come to England"

Katika video hapo chini mzungu anawaambia wahamiaji wa kiafrika kuwa wasiende Uingereza kwa kuwa wana wahamijai wa kutosha na watu wao ambao inabidi wawatumikie
View attachment 1563148
enheee, na wenyewe wamejibu nini

endelea kutuhadithia
 
Waafrika matatizo tunayatafta wenyewe. Tunasshindwa kutengeneza nchi zetu tunakimbilia za wazungu, kwani tuliwasaidia kutengeneza nchi zao?
Anayejaribu kutengeneza nchi anapigwa vita na akina Tundu Lissu
 
Muafrika anakitu gani hasa cha kuibiwa chenye maana kwa dunia?
Chuma hana,almasi mrusi anayo tele Dhahabu mkanada anayo,gesi ulaya ipo, ananini muafrika zaidi ya chuki, maradhi ,kuminya Uhuru wa wenzie ili yeye atawale hata kwa mkono wa chuma, elimu yenyewe ya ubabaishaji, bado rushwa, nepotism na nk, muafrika hajiamini na hatuaminiki popote si kielimu,kitabia hata kiuchumi
 
Wazungu wengi wana mawazo kama ya huyu sema tu hawayasemi live.
Sana sana nearly 90% ila wanaogopa kuitwa wabaguzi. Mwingereza yuko tofauti kidogo na wazungu wenzao. Ni mnafiki 100%. Hatakuambia usoni maneno ya kibaguzi, ila mate matendo yake yatazungumza alivyo, mfano, kazi hutapata kama jina la mwisho ni la kiafrika. Kazini utakoma kwa kutokupata cheo na kufuatiliwa kila kona, madukani nq supermarket utakoma, michezoni hupati nafasi kama wazungu, uongozini ndio kabisa hasa kwenye siasa. Ni shida kwa kweli, ila ataongea swala la kupinga ubaguzi kama vile ana upend nawe kumbe gelesha tu, bure kabisa wale...
 
Tena hao hao mabeberu tunaowatukana kila uchao wakipiga pini misaada ya ARV na soksi za kiume hapa afrika mbona ndani ya miezi sita tu nusu ya nchi zetu zitakuwa ni makaburi, yaani vilio kila nyumba tutapukutika kama nyasi kavu zilizoshika moto na ndio utakuwa mwisho wa bara hili sababu nguvu kazi asilimia kubwa ipo kwenye red zone.
 
Kama kuna taifa ambalo halipaswi kulalamika kabisa kuhusu immigrants ni Great Britain.... They have introduced us to them
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…