Na Hii shahada yangu, niuze matikiti? This is not fair.

Na Hii shahada yangu, niuze matikiti? This is not fair.

Mwenzio ana shahada ya uzamili (masters) toka Marekani, mtoto wa familia bora, mrembo Sana, mtoto wa kike ana option ya kuolewa na nafasi ya upendeleo kwenye ajira.
Lakini anauza makande. Kaza mtoto wa kiume. Fruit stand hiyo unayo idharau inaweza kukupa utajiri, hapo ubunifu tu.
Papai la kisasa shambani kwangu nauza 300 wakati muuzaji kwenye deli (fruit stand) anauza zaidi ya 3000.
Kwanini usiajiri watu ukafungua vijiwe 4? Posta, Sinza, Goba, Ilala Boma na Kariakoo?


View: https://youtu.be/aIv_5i5ruCk?si=zd2FFsFXUx_ENdIw
 
Toka geto.Sogea Njombe viwand a vya wachina.Ikifika miezi 3 mbona utakuwa bonge la mpambanaji.

Ikifika mwezi Wa 12 Njombe dili za parachichi hukosi 10000-20000

Sogea huku Njombe

Nb
Ukifika kiwandani ficha degree na wenzamo tunazo
 
Kuna mwingine na shahada yake alijiajiri kuuza kahawa Stand ya mikoani enzi za Ubungo.
Akaajiri warembo. Usidharau kazi.
Aibu yako umasikini wako.
Mimi na shahada yangu nalima, nafuga nguruwe na kuku kijijini huku. Nina maisha Dar. Namaanisha nyumba n.k.
Niliamua kuajiriwa sasa basi.
 
Ishu sii shahada, ishu ni unapataje pesa. Mbona umesoma alaf sii msomi
 
Toka geto.Sogea Njombe viwand a vya wachina.Ikifika miezi 3 mbona utakuwa bonge la mpambanaji.

Ikifika mwezi Wa 12 Njombe dili za parachichi hukosi 10000-20000

Sogea huku Njombe

Nb
Ukifika kiwandani ficha degree na wenzamo tunazo
nipe connection mkuu.
 
Weka pembeni hiyo degree upambane mkuu, yaani jifanye kama hujasoma kbsa afu uone jinsi utakvyofanikinikiwa.
 
nipe connection mkuu.
Ukifika mwezi 12.Njombe viwanda vya parachichi unaenda moja kwa moja unapata kazi.Sio kama Dar huku unaweza ukapata sehemu hata tano unachaua wewe.
Ukifika mwezi 12 toka Dar unachelewa.Dar nimekaa najua ugumu Wa Dar
 
C Bora nisingesoma kabisa
How come na shahada yangu niuze matikiti kwenye deli...

Hii sio haki
Ni bora usingesoma kweli
Kwa sababu elimu uliyopata bado haijakufaa kwa lolote yani haijafanikiwa kuondoa hata ujinga kichwani
kwa karne hii kusoma ukitarajia ajira ni upuuzi pia kuuza matikiti ni upumbavu zaidi
 
Back
Top Bottom