Na wao hulipwa posho za per diem?

Aibu kubwa! Na hapo wanasema liwalo na liwe! Lisemwalo na lisemwe,tumeshika mpini wao wameshika kwenye makali!
 
Viongozi wa nchi zilizoendelea huwa wanawaona viongozi wenzao kutoka Africa ni ngedere zilizochangamka, ukiwa hujielewi zile tabasamu na hospitality unapokaribishwa unaweza kujihisi wanamaanisha.
 
Inachekesha sana hii picha, kibaya zaidi wakorea hata bendera ya kwao hawajaweka, yaani sijui hata walikuwa wanajadiliana nini, aibu sana πŸ˜ƒ
Mimi naamini Rais angewaachia hao waigizaji wafanye huo mkutano na hao waigizaji wenzao.

Sioni kabisa tija wala ulazima wa mkuu wa nchi kuwepo hapo.
 
Wageni 100 wenyeji 3!
Safari yetu ni ndefu mno, mpaka mapambazuko yatufikie sijui tutakuwa hali gani !
 

..Watanganyika?

..inawezekana Wazanzibari ndio wengi ktk hiyo delegation.

..lakini rasilimali za Tanganyika ndio zinapigwa mnada, ila za Zanzibar haziguswi.
 
Tunawmbiwa hao waigizaji wameenda kujifunza huko Korea.

Sina hakika wameenda kujifunza nini.

Ni kitu gani ambacho hawakijui na ambacho hao Wakorea wanakijua?

Hao Wakorea wao waliendaga wapi kujifunza hayo wanayoyajua kwenye huo uigizaji?
Swala lakujifunza kwa waliofanikiwa ni sahihi,Lakini naona aliyemshauri mama kuambatana na hao wasanii kwamba ndani za ziara ndio kuna kujifunza naona ni upuuzi.Alitakiwa akifika Kule aombe kupatiwa wataalamu waje hata DSJ pale hata miezi 3 wawanoe wasanii wote sio hao mala..ya waliokwenda. WATU VIAZI NDIO WAMEKUWA WASHAURI WA SEREKALI.
 
Sawa.

Lakini hao waliofanikiwa, wao walijifunza toka kwa nani?
 
Dalili za wivu,mi nimetangulia kurudi korea ni sehemu nzuri na wakarimu sana
wenye wivu mtapata nafasi mwakani
 
Huku ni kuhujumu uchumi wa nchi. Dreamliner imepaki Korea siku ya tano leo bila kufanya ratiba yake ya China kisa inangojea kijiji cha wasanii na machawa walioko kwenye mkutano na wakorea wachache ukumbini....Hii aibu gani hii?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…