Na wao hulipwa posho za per diem?

Mama ameamua kuvunja Rekodi ya Mkwere.

Rekodi ya mama Kwa Sasa haishikiki baada ya kuipiku ya Mobutu See Seko!!

Nchi imepata ikapatikana
 
Unaambiwa Mama anaifungua Nchi!!

Naisubiri Sinema NYINGINE anayorekodi.... Nadhani tujiandae Tena kuzificha sura zetu Kwa aibu
 
Mimi naamini Rais angewaachia hao waigizaji wafanye huo mkutano na hao waigizaji wenzao.

Sioni kabisa tija wala ulazima wa mkuu wa nchi kuwepo hapo.
Upo sahihi kabisa!! Yule ni WA level ya mijadala na Rais mwenzake!!

Anyway Kama alikosa muda wa kuwasikiliza Wafanyakazi Mei mosi lakini akapata muda wa kwenda Mlimani City kuburudika na Harmonizer, inabidi tumuachie tu Mungu ainusuru Tanganyika yetu
 
Sipati picha eti Julius Nyerere au Benjamin Mkapa ashiriki kikao nje ya nchi na waigizaji wa filamu za bongo movie na Korean soap operas.
 
Mimi bado hata sijui ambacho Wakorea wanakijua kuhusu uigizaji na ambacho sisi hatukijui mpaka kumlazimu rais aende na rundo la waigizaji wa Kitanzania huko Korea!

Wanachokijua wao na ambacho sisi hatukijui ni kipi hasa?
Watatufundisha kuweka subtitles nzuri kwenye muvi na tamthilia zetu na bonus ya kutuletea ujuzi wa kupata ngozi nyororo wenyewe wanaita glass skin 🫠
 
Kwanini wasilipwe?
 
Mkuu ebu fafanua vzr kwenye waigizaji walioenda inamaana ata muhogo mchungu yumo?πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Hao waigizaji wamejilipia wenyewe hizo gharama au ni pesa za walipa kodi ndo zinatumika?
Mimi nitajibu hili:
Utaambiwa hizo pesa hakuna hata senti moja toka kwa walipa kodi.
Sasa uliza swali jingine, je, hizo pesa zinatoka wapi?
Mimi nitajibu--ni toka kwa wajomba, wanaotaka kuhakikisha kwamba mpwa wao ananunua ngwe mpya ili waweze kujinasibu zaidi hapa nyumbani.
Hawa wajomba wanazo hela wasizojuwa wazifanyie kazi gani, kwa nini wasitafute mahala pa kwenda kuchezea michezo yao michafu.
Hivi unajuwa maana halisi ya "Banana Republic" ni nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…