Naachana na harakati za kisiasa Tanzania, hazina faida yoyote

Tuliwaambia msimfananishe magufuli na vitu vya kijinga mkabisha sasa mafisadi yameingia tena ikulu tuone kama watawasikiliza ,Kile ninacho kiona ni hali zenu za mwisho zitakuwa mbaya kuliko za mwanzo
 
Were mwenyewe hujawahi kuandandamana halafu unalaumu wengine kwanini hawaandamani! Pumbavu! Nenda unakoenda. Tanzania itabaki!
 
Safari njema boss wangu!
 
technically Usichukulie Siasa za Tz kwa nguvu zako zote na kujilipua kwa kujitoa mhanga...utaumia sana kwa maana hata wanaoitwa viongozi hawako serious na hizi siasa pia.

Asilimia kubwa ya wanasiasa bila kujali chama, wako kilingeni kwa ajili ya kutafuta maslahi yao.
Anayefanya siasa za kweli ni mwananchi wa kawaida ambaye naye anategemea maslahi bora kutoka kwa mwasiasa feki.

Hivyo mkuu relax ziangalie hizi siasa kwa mtizamo tofauti.
 
😎😎😎 umesahau kuwa tumerithi nizamu ya woga Toka kwa wazazi wetu tangu enzi za mwalimu, tuna nyanyaswa na kivuli Cha aman, thus why people fear to organize maandamano,
 
Pole sana kawasalimie
 

Unasomeka mkuu. Yaonesha ulidhani njia hii ni nyepesi.

Kwamba kama wewe hukuandamana katika lolote moja kati ya hayo, haiyumkiniki ulitegemea wengine wafanye hivyo wala si wewe.

Njia hii ni ngumu yenye mateso mengi. Mbowe angekuwa nyumbani kwake na wanawe leo kwa kuchukua uamuzi kama wako tu, wa kuachana na hii mambo.


Heri kuwa baridi kuliko kuwa vuguvugu. Kama ni urahisi tu, kujiuzulu au hata kuunga mkono juhudi inaweza kuwa muafaka zaidi kwako.

Safari hii tumedhamiria kuwa na wenye nia tu kuliko kuwa na marefu ya wasiokuwa na guts.

Pumzika kwa amani Mkuu tutaonana baadaye.
 
Siasa inamuhusu kila mtu, naifanye kwa uzalendo wa nchi yako bila kuisababishia matatizo, hivyo usikate tamaa, na ukiacha wajinga watachukua nafasi ya kukuongoza mambo yatakuwa mabaya zaidi.....
 
mie nafikiri ungeanza kuandamana na wengine wangekufuata.
 
Tuna matatizo makubwa mkuu.Ukiona taasisi kubwa kama za dini,taasisi za kiraia na wasomi wapo kimya haswa hata kwenye suala la Katiba basi ujuwe siyo Mbowe tu aliyeko gerezani bali watanzania tulio wengi ukiachana na wanufaika wa mfumo.

 
Ukitaka kufurahia siasa za Tanzania usiwe na chama. Epuka kuwa msukule wa mtu yeyote!!!
 
Pole. Walau sasa unaanza kuelewa maana halisi ya kauli ya JPM ya maendeleo hayana vyama.

We unadhani maendeleo yako binafsi atakuletea mwanasiasa? Wa CCM au Chadema? Wao wenyewe wanafight kwa ajili ya matumbo yao na watoto wao wenyewe.

Ila kitu kitakachokuweka huru na ukawa huru kweli kweli ni kuijua Kweli. Na kweli ni kwamba kama kila mmoja wetu angefanya bidii kujielimisha mwenyewe, kujiletea maendeleo yake mwenyewe usingekubali kudanganywa na mwanasiasa yeyote kutoka chama chochote kwamba ukimchagua yeye atakuletea maendeleo.

Pia Kweli nyingine ni kwamba usipoijenga nchi yako kwa mikono yako mwenyewe hakuna mjomba atakayekuja kukujengea nchi yako ikiwemo na nyumba yako.

Tungeifahamu Kweli hiyo tusingetumia muda mwingi kugombana sisi kwa sisi au kushtakiana kwa wamarekani.

Tungeijua Kweli hiyo tungefanya mambo kitofauti na tungewajibishana kitofauti.

Kwa kupitia Kweli hiyo tungeshangaa kuona kwamba maana halisi ya Demokrasia ni kujadiliana namna gani bora ya kujenga nyumba yetu ya pamoja iwe imara na bora zaidi.

Hata namna ya uwasilishaji wa hoja kinzani, ikiwemo kukubaliana kutokubaliana, ingekuwa tofauti kabisa.

Umechelewa sana kuitambua hiyo Kweli lakini karibu sasa tuijenge nchi yetu bila makandokando ya siasa na wanasiasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…