Naachana na harakati za kisiasa Tanzania, hazina faida yoyote

Mkuu umesahau kitu kimoja kikubwa sana ambacho ukikifanyia kazi nina uhakika hutofikiria kwenda nchi nyingine... Kwakuwa umeshatambua kuwa sisi watanzania ni 'waoga' na 'wanafiki' wa kutupwa basi we pambana kupata 'chance' kwenye huo 'mfumo tawala' ili ule mema ya nchi.

Trust me ukiwa kwenye huo 'mfumo' we tunyooshe tu watz, kwasababu mwisho wa siku hata utufanye nini tutaishia 'kuongea' tu, maana ndio tunachokiweza.
 
Mbaya zaidi siasa ndiyo hatma ya jambo lolote ulifanyalo maishani kwako. Wanao, wajukuu na hata kizazi chako kijacho siasa hii inawahusu - nakushauri komaa tu hadi hapo nchi itakapokuwa inaamulikuwa kwa kura za almost fifty fifty kwenye maamuzi ya mustakabali wa nchi yako.

Leo hii watu wasiozidi 6 tu wanajifungia na wanaamua hatima ya taifa lako - hii ni mbaya saana... simama uhesabiwe - siasa haikwepeki ni kukomaa nayo hadi hapo Bunge litakapokuwa la kidemokrasia - na Rais wa nchi apatikane ki-demokrasia na mahakama kuwa chombo huru ambacho hakitariport kwa mtu mmoja.
 
Hapana usijitoe kijana wa Bavicha ila kinachotakiwa usitolee macho siasa za Bongo mpaka kukubali kufa ama kwenda jela,kwasababu wananchi bado wamelala na viongozi wa upinzani wanafika bei pia,fanya siasa za upinzani ili kuishtua chama tawala ili isijisahau sana.
 
Kamanda Pole sana! Sisi tulinyang'anywa Ushindi wa John Mnyika Mwaka 2005 kwa Charles Keenja kutangazwa kwa Nguvu na hakuna aliyeandamana. Toka muda huo nikaachana na hayo mambo! Shida hayo yote uliyoyasema yanavishwa Nguo ya AMANI.
 
kuandamana, kuandamana, kuandamana. kwa uono wako maandamano ndio suluhisho la matatizo yote uliyoorodhesha.
 
Mkuu kwa muda nilikuwa nataka kuandika mada kama hii lakini umeniandikia kabisa
TATIZO SIO CCM WALA VIONGOZI
TATIZO NI WATANZANIA AMBAO NADIRIKI KUWAITA WAPUMBAVU
NAAM WATANZANIA NI WAPUMBAVU
 
Tatizo ni mwenge ...unaharibu fahamu za watanzania wengi hawaelewi hili
Ni jambo la kiroho
CCM itatawala sana
Inatoa elimu mbovu Kwa Wananchi wake huku ikijua kabisa haiwezi kuwakwamua
kwenye karne hii na Wananchi wanaangalia tu
Wameharibiwa fahamu zao
 
Ongezea na kuwaongezea followers akina Shangazi ili wapige hela zaidi kutoka kwa hao wanaowafadhili! Leo hii Sarungi na Karume ndiyo waongoza harakati za CDM na watu wanawaamini!!!! Lolote likitokea hao watu mfumo huu huu wanaoutukana utawalinda
 
Mkuu sikushauli ufanye ulicho kiandika kumbuka weledi ni wachache wajinga ni wengi kumbuka haya yanayotupata sasa hata mwalim yalimkuta kipindi hicho anausaka UHURU wajinga walimbeza nahata kumlaan wakisema wewe mzanaki unatuhalibia maisha hakukata tamaa alisonga mbere hata sisi tusikate tamaa watanzania wengi hawazijui haki zao hata ukiwaambia habari ya katiba hawajui wengine mpaka Leo wanajua nyerere yupo hajafa Tusikate tamaa Tusonge Mbere Mbowe watamuachia hawana kesi ya kumfunga tukaze mwendo kamanda Tunataka KATIBA MPYA NA TUME HURU,
 
Nimecheka baada ya Heading.

Karibu.. MMU
 
Kidogo kidogo tutaelewana! Hongera kwa kujitambua, bado Tundu Lissu
 
Nyerere aliiacha Tanzania yenye wafu wanaotembea so usijisumbue na ninamshangaa sana Mbowe sijui anamtesekea nani…. Bora awe mtukanaji wa mitandaoni Kama sisi tu.
Kiukweli Mbowe angeachana tu na Siasa za Tz,
 
ukome kiranga,swine!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…