Naamini kwa dhati kabisa nguvu ya Makonda haitokani na kuwa kwake katibu mwenezi wa CCM, lazima kuna chanzo kingine kinampa kujiamini kiasi hiki

Nikuambie tu Paul Makonda siyo mtu wa kawaida. Nafasi ya sasa ni ndogo kuliko yeye. Muda utaongea! Hata alipokuwa mkuu wa mkoa Dar ilikuwa kama yeye ndiyo prime minister. Jamaa ni hatari.
 
Ccm bwana ww si ulikuwa unamponda sanq
 
Unafrahisha sana kujiita mlokole!
Na kutabili uongo kiasi hicho
Inawezekana nafasi IPO ila watu hawakujua /kupenda kuitumia ipasavyo!!
Baba huyo ndo msemaji wa CCM!!!
MAKONDA Baba lao endelea kusafisha mapito !!
 
Rais awapige chini watendaji wote wabovu. Haingii akilini mtu anaharibu wizara ya nishati badala kufukuzwa anapewa wizara ya nje. Mara aseme mitambo chakavu, ukarabati, mvua, watu kuchepusha maji greda.

Lukuvi, kalemani walizimudu wizara zao. Uhuni ulipungua huko. Unawatoa kisa woga, fitina, majungu.

Inatakiwa watendaji wote wapige kazi zao na kuwajibishwa. Rais awe mfano.
 
Tatizo linaanzia hapo juu kabisa. Uwezo mdogo wa kiuongozi. Unafikiri wateule wakisikia kauli zake wanajali. Wakiiba wanajua watahamishwa au kupewa kazi nyingine, hakuna uwajibikaji.

Watu wanamsikiliza zaidi Majaliwa na Makonda kuliko Rais. Mifano, teuzi na vitendo vyake vinaonyesha hajali maisha na shida za watu wa chini.

Unawaita wengi wajinga, elimu, afya, ajira, umeme, maji, mazingira wezeshi wanyanyuke watoe ujinga.

Weka mifumo, viongozi, taasisi imara zitakazolinda usalama na mali zao.
 
"If wishes were horses, beggars would ride".
 
Ametatua tatizo gani la msingi kwenye kuzunguka kwake kimaigizo!!??
 
Nimekuelewa Sana, na kwa upeo wangu na pia kwa historia iliyokuwepo kwa muheshimiwa pamoj na hizi chaguzi zijazo ni wazi kabisa zote hizi huenda zikawa siasa.
 
Mpaka sasa amefanya nini Makonda? Ila watu mna muda wa kupoteza, alikopita kote ni wapi umesikia kuna tume iko kazini kwa madudu aliyoyaibua Makonda? ni wapi umesikia watumishi wamewekwa ndani kwa upotevu wa mabilion, maigizo ni maigizo tu hayajawahi kuwa kitu halisi.
 
Kikubwa Watanzania wamepata sehemu ya kuongelea shida zao na zinatatuliwa hayo mengine hayajalishi.
 

Wewe ungekuwa Mkurugenzi mwizi, afisa ardhi mwizi mkubwa umedhulumu wengi ukisikia anakuja mwezi ujao ana ziara eneo lako ungeendelea na wizi ungekuwa kwenye hali gani? Utafanya kazi yako vipi?

Ukijua hadi Rais, mawaziri, wakubwa zako, Tanzania nzima itaona wizi wako? Utaitwa jukwaani kujieleza?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…