Naamini kwa dhati kabisa nguvu ya Makonda haitokani na kuwa kwake katibu mwenezi wa CCM, lazima kuna chanzo kingine kinampa kujiamini kiasi hiki

Eti amkebehi Mwanasheria Mkuu wa Serikali!! Huyo Mwanasheria Mkuu wako ni Mungu? Hanyi? Hakosei?

Mwanasheria ambaye hana wanasheria wa kuitetea nchi? Hata juzi tumepigwa 300bil, Mtu huyu kwako ndo Mungu asiyekosolewa?

Acha uzabizabina. Makonda ni Level nyingine kabisa kwa sasa
 
NI wazi wewe huna ufahamu wa kutosha kuhusu majukumu ya chama na serikali katika utaratibu wa uongozi wa nchi. Msikilize Fatma Karume labda kuna jambo utaambulia pale.
Fatuma Karume huyu huyu Mlevi wa Dawa? Usitupotezee muda hapa
 
Ni sawa lakini so long as wapigakura wanaona ni poa that is right.

Kuna tofauti ya kumtumia PM au Watendaji wengine kwenye Hilo Kwa sababu litaonekana ni Kushindwa Kwa Serikali tofauti na kumtumia mtu wa Chama kuwasulubu Watendaji itaonekana Chama kinafanya kazi.

Hiyo strategy ndio alikuwa anatumia Mwendazake na maigizo kama hayo.

Mpaka hapo shida Iko wapi? Ccm Kwa Sasa inatafuta kura at any cost na Makonda kapewa jukumu Hilo nothing else.
 
Swala sio kufikia Kila maskini swala hapa ni kutuma ujumbe kwamba chama Kiko kazini,kufikiwa ni mpaka itokee ila inatafutwa Imani kwamba akija yule na Mimi nitasiaidiwa so kwenye siasa hicho ndio kinatafutwa.

Sasa mtu ataamini Chadema itamsadidia wakati nao Chadema ni walalamikaji?
 
Kwa hiyo yeye atakosa wa kumlinda? Kwamba ni mjinga wa kiasi hicho? Kwamba huko ccm woote wanamchukia au siyo? Hakuna kitu kama hicho.

Uchaguzi ukipita Samia anaweza mpa cheo kizuri tuu Cha kiserikali na hiyo njama ya harassment ikayeyuka ghafla.
 
Hata kama hayuko sahihi ila kama amewekwa kimkakati Kwa maslahi ya chama Kuna ubaya gani? Kwanza ana deal na Watendaji na sio Wanasiasa wenzie japo Kuna mambo kama binadamu Huwa anakwazika nayo ila generally hii strategy ni karata dume Kwa Samia na ccm yenyewe.

Shida ni kwamba wale Wanasiasa ambao walikuwa na malengo ya urasi ndio Hawapendi Kwa sababu wanaona anafifisha Nyota zao
 

Bashite ni mtu ambaye hata mzee Baba msepa zake alikuwa akimhanya!!
 
NI wazi wewe huna ufahamu wa kutosha kuhusu majukumu ya chama na serikali katika utaratibu wa uongozi wa nchi. Msikilize Fatma Karume labda kuna jambo utaambulia pale.
Naungana na jamaa, sisi wananchi wa kawaida kabisa hatutaki kujua hayo mambo yenu ya protocol za uongozi, tunahitaji mtu wa kusikiliza matatizo yetu na kutatua.
 
Kwanza naunga mkono hoja, kuwa Mwenezi ni very powerful extra ordinarily, hiyo power anaipata kutoka kwa YEYE!. Mafanikio ya Makonda ni Uthibitisho Wa Jiwe walilolikataa Waashi litafanywa kuwa Jiwe Kuu la Pembeni

Kuhusu anguko la CCM, naomba kutofautiana na wewe, badala ya CCM kuanguka, Makonda ameifanya CCM iamke, CCM sasa inapata!. Pongezi Paul Makonda kuifufua CCM kwa amsha amsha. Twende mdogomdogo ngoma ikivuma sana inakaribia kupasuka!
P
 
Sasa ulitaka makonda aje nyumbani kwako?au ni chuki na wivu umekujaa

Tarizo hamkutegemea makonda atapewa tena cheo ,Mlikuwa mnatembea na hukumu zenu mfukoni
 
ni katibu wa nec, katibu uenezi na itifaki, katibu wa mafunzo. tambueni hapo anamajukumu 3. anaiwakilisha ccm nec, anaiwakilisha ccm chama na anatoa darasa kwa vitengo vya serikali.
 
Mheshimiwa nakukumbusha tu urudi nyuma, walikuwepo kina nape, pole pole, badhiru na Kinana mwenyewe tena walikuwa wa moto balaa!!! Wako wapi???

Waelewa wanajua kwenye mtori huu nyama zipo chini!!!
 
Ccm ni ile ile utasubiri sana ianguke tazama utaanguka wewe.


Makonda woyeeeee
 
Sasa umeanza kujipendekeza kwa Makonda ukitegemea kwamba labda kuna siku atapitishwa kuwa Raisi? Tuombe uhai, maana nachelea unaweza kufa kwa kuvunjika moyo. Samia anaweza kuwa alilazimisha Makonda kuwa katibu mwenezi japo alipingwa sana na viongozi wa CCM na wengine kutaka hata kumziria chama, lakini Samia akitaka kujua Watanzania bara wakoje aje ajaribu kulazimisha eti Makonda awe mteule wa CCM kugombea uraisi baada ya kipindi chake. Utaona mambo yatakayoanikwa hadharani.
 
Mawaziri na watendaji wanaolalamikiwa ni wateule/waajiriwa wa serikali ya CCM. Chama kimejaza mawaziri na bureaucracy kubwa serikalini. Hiyo ndiyo maana sahihi ya chama kuwa kazini; ndivyo chama kinavyodhibiti na kusimamia serikali. Kawaida, si sahihi kwa viongozi wa chama (except Rais) kuwa na mawasiliano ya moja kwa moja ya kikazi na watendaji wa serikali bali kupitia wateule wake wa kisiasa serikalini (mawaziri, RCs, DCs, etc.) nje ya ofisi za umma.

May seem complicated to many lakini huo ndio usahihi wenyewe.

Sasa hii ya Katibu Mwenezi wa CCM kutembea na misafara mikubwa na kuitisha mikutano ya hadhara yenye gharama kubwa kusikiliza malalamiko ya individuals dhidi ya viongozi na watendaji wa serikali ya CCM, ni ufujaji mkubwa wa hazina ya taifa usiokuwa na tija yoyote zaidi ya kupeana faraja ya kisaikolojia kwa watu wenye uwezo mdogo sana wa kufikiri.
 
Hao voingozi wavivu, wazembe, wajinga wanafanya kazi chini ya uongozi wa chama gani? Waliteuliwa katika nafasi zao na uongozi wa chama gani?

Aaah, waliteuliwa na Mbowe. Samahani nilisahau!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…