Naamini Mungu yupo ila nashindwa kuuelewa ukamilifu wake, labda muendelee kunifunza

MUNGU YUPI SASA ALIWEKA HIZI SHERIA??????? MAANA KILA MUNGU WA KILA DINI ANA SHERIA ZAKE MKUU...
Hizi sheria, ni Designer Mkuu wa Universe ndo ameziweka, Kwa wanadamu ndo maana kwa Kila dini unaona sheria za maadili zinafanana maana Kila mtu amewekewa utashi wa kujua jema na mabaya.
Kuna kitu ukifanya unahisi msuto Fulani hivi ila ukizidi kufanya na kurudia ile aibu inakutoka sasa ile aibu ndo Muumba ameweka.
 
Ndo sio Sasa sheria za mtu. Haya Mimi Nina miaka 22 na demu wangu ana miaka 20. Tunafanya Mapenzi bila kucheat na tunatumia uzazi wa mpango. Haya kosa langu hapo Mimi Ni Nini.
Kosa lako litakuwa kumuacha.
Ukisoma vile vitabu vya Mwanzo vya Musa, mwanaume akifanya mapenzi na mwanamke bikra na akagundulika, anapaswa amuoe mwanamke huyo .
Pili kosa lako lingine ni kutumia uzazi wa Mpango, Designer Mkuu aliumba shahawa kwa ajili ya kupass genes from generation to generation Ili kizazi kisipotee, kufanya mapenzi kupitia condom unazuia mipango ya nature ya kuzaliana ,hilo ni kosa.
 
Kipimo cha kutumia Ili kujua kitabu gani kimesema kweli ni akili yako tu., Yani ukivisoma vitabu hivyo viwili utagundua kipi kimesema kweli na kipi kimeongea uongo na kwenye hivyo vitabu viwili ukiona kitu hakiingii akiilini mfano concept ya utatu ukiona haiingii akilini basi ujue ni Uongo huo.

Injili(Biblia) ilianza kabla ya Qur'an na Qur'an yenyewe inatambua na kuheshimu hilo,..lakini hiyo hiyo Qur'an inasema kwamba Kuna baadhi ya watu waliamua kuuza Maneno ya Mungu kwa thamani ndogo ya maslahi yao kwenye Dunia, wakabadilisha baadhi ya mambo kwenye Hivyo vitabu vya mwanzo(Biblia) kabla ya Qur'an .... Mfano jiulize tu, Je concept ya Utatu mtakatifu imetoka kwa Mungu au watu wamejitungia?
 
ila shida yangu kubwa ni sifa za Mungu ambazo anapewa na wanadamu naona kama zinashindwa kujidhihirisha kwenye baadhi ya mambo.
Kwa maelezo yako ni kuwa hujaridhishwa na sifa anazopewa na wanadamu, ila wewe ni mwanadamu pia, una nafasi kwa kadri ulivyomjua Mungu kuumpa sifa unazoona zinamfaa.
 
Siyo Hawa alikuwa dhaifu, ila binadamu wote ni dhaifu, hata Mungu aliyewaumba nadhani wanamjua kwa asilimia ndogo sana, kwahiyo usitegemee majibu makamilifu. Kwakuwa umeamini uwepo wake rekebisha matendo yako uendane naye kukwepa jehanamu. Ni yeye pekee anayejua kwanini aliumba viumbe dhaifu. Kingine jihadhari sana na shetani, alishuka na nguvu za kutosha, asikutumie kwa malengo yake.
 
Na ujumbe wa huyo Mungu mmoja huujui, hujui yupoje. Hujui anataka Nini, hujui atafanyaje, so usimpe sifa na sheria ambazo watu wa kale walimbunia.
So, umekubali na kuamini kwamba Kuna Mungu Mmoja Muumbaji?
 
Hakuna ushahidi wala uthibitishobwowote kwamba kuna Mungu aliyewaumba watu.

Tena, huyo Mungu anayesemwa kawaumbwa Adam na Hawa, anaweza kuthibitishwa kimantiki kwamba hayupo.

Zaidi, wasomi wa Biblia walioisoma kwenye ma seminary na kuifundisha mpaka vyuo kama Harvard wanasema mnavyoisoma na ilivyo kiuhalisia ni vitu tofauti kabisa, huyo Adam hakuwahi kuwepo, huyo Hawa hakuwepo, hizo ni stories za mafumbo ya utamaduni wa Wayahudi tu watu wasioielewa Biblia wanazichukulia kama habari za kweli.
 
Acha uwongo Sheria hazifanani. Wengine wanakula nguruwe wengine hawali, wengine wake wanne wengine mmoja, wengine wavae magunia wengine wasivae. Hizi Ni sheria za watu. We unaweza ukakuta mchwa kwenye kichuguu ukawaambia wakuabudu na wafuate sheria zako au utawaunguza. Jua jinsi ulimwengu ulivyokuwa mkubwa sisi Ni Kama bacteria katika ulimwengu... Huyo muumbaji kwani ajali kuhusu bacteria wanajamianaje au wanavaaje.. Ina msaidia Nini yeye
 
Turudi hapa.. Kama sex bila lengo la kuzaa Ni kuzini au kuuwa. Nieleze kwanini nature hiyo hiyo imempa mwanamke siku salama na zisizosalama, na nature hio hio imempa mwanamke tabia ya kuua yai kila mwezi. Hii inaonyesha kuwa vitabu hivi vimeandikwa na jamii isiyo na ujuzi wa Mambo ya kidunia. Na hizi sheria zimetungwa na watu wajinga wa kale.
 
Sheria unazoziiita za watu wa kale ndiyo zilikua Bora compared na sheria zilizopo zama hizi... Sheria za siku hizi ndiyo zinaleta upuuzi wa haki za ushoga & Transgender na ujinga kama huo.
 
Mstari
Mstari
Hujanielewa vizuri kama ulivyohisi kwenye mstari wako wa mwisho. Soma swali la mtoa mada Kisha soma jibu langu. Kiufupi shetani hayuko na malaika mbinguni, huko alishafukuzwa na hana nguvu mbele ya Mungu kama mtoa mada anavyodhani. Nguvu ya shetani iko duniani anakojaribu kushawishi watu, nguvu yake ndio mtihani wa binadamu katika kumtukuza na kumjuwa Mungu. God doesn't control everything but He is capable of and can do that at His own will and convenience. Sasa nilitoa disclaimer kwamba we can't discuss God empirically but logically.
 
Zaidi, wasomi wa Biblia walioisoma kwenye ma seminary na kuifundisha mpaka vyuo kama Harvard wanasema mnavyoisoma na ilivyo kiuhalisia ni vitu tofauti kabisa, huyo Adam hakuwahi kuwepo, huyo Hawa hakuwepo
Hao wasomi wa Biblia toka seminary na kufundisha Havard walijuaje hayo? kutoka source ipi? kama unaweza share please?!
 
Hivi vyote Ni visingizio vya dini ili tusiulize maswali. Ni Bora kuwa na maswali ambayo Sina majibu kuliko majibu ambao siruhusiwi kuuliza maswali.
Twende taratibu ndugu SimbaMpole123 kama kweli umedhamilia kujifunza na kuelimika.
Kabla sijaendelea kukufafanulia naomba nkuulize swali dogo,

Unafahamu kuwa only jambo ambalo umeli experience via mind ndilo pekee unaweza kulielezea? You cannot explain something beyond your mind experience. Hilo jambo aidha uliliona kupitia macho,ama ulisikia kupitia masikio,ama ulionja kupitia ulimi ama uliguswa kupitia ngozi ama Kupitia pua.

Our mind experience, depends on our only five Senses ambazo nimezitaja hapo juu(Masikio,pua,ulimi,ngozi na Macho)

Tunapo sema our mind is limited,maana yake ni kwamba tunategemea experience kutoka kwenye Five senses ili ku develop our experience of life and perception of life..

Hivyo basi,kuna vitu hatuwezi kuviona kwa kutumia macho yetu ya kawaida kwa kutambua kuwa we are limited. tunajikuta tunatumia microscope kuangalia.

Kuna harufu hatuwezi kuzinusa kwa kutumia pua zetu, then tunamtumia mbwa kuwinda.. mifano ni mingi.
Ndipo tukasema kuwa our mind is limited.

Ili uwe na ufahamu wa hayo mambo, unahitaji kwenda beyond your five senses of human experience. Hapo ndipo kazi inaanzia.
 


Iwafikie wale wote wanaopinga uwepo wa THE BEST DESIGNER/THE BEST CREATOR!.,
Human being is a work of art& engineering.... Yani Mtu alivyo tu inaonyesha kuna ufundi ambao umefanya mpaka ukaona mifumo yote kwenye mwili wa binadamu kuanzia:-
1. Respiratory system
2. Digestive system,
3. Circulatory System
4. Nervous System
5. Endocrine system
6. Muscular system
7. Skeletal system
8. Immune system
9. Urinary system
10. Reproductive system.


Yani, Ingetosha kabisa kuangalia mwili wako na jinsi unavyofanya kazi kujua kwamba kuna DESIGNER aliyeweka mifumo yote hiyo., Au kama unahisi mwili wa binadamu na jinsi unavyofanya kazi umejitokeza tu from nowhere, let's conclude that hata robots tunazoziona zimejitokeza tu from nowhere..... Does it make sense?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…