Naamini Mungu yupo ila nashindwa kuuelewa ukamilifu wake, labda muendelee kunifunza

Naamini Mungu yupo ila nashindwa kuuelewa ukamilifu wake, labda muendelee kunifunza

A
Kama Mungu anapenda tumtii bila shuruti kwa nini alitupa uwezo wa kufanya mabaya na kutenda uovu ambao yeye unamchukiza?

Alishindwaje kutuumba tuwe tunafanya mema na mazuri tu kama atakavyo yeye??

Ana uwezo wa vyote kweli huyo Mungu??
Angeweza kutuumba kama robots lakini nahisi asingejivunia uumbaji wake lakini pia alituacha tuamue kwa hiari yetu tunachopenda kufanya ndio maana akatupa utambuzi wa mema na mabaya, yaani kwa lugha rahisi yeye sio dictator ila utavuna ulichopanda.
 
Mi naona adhabu ziko wazi ivo ni maamuzi yako kuchagua ukosee au ufanye yanayompendeza sababu ukifanya mazuri kuna zawadi na ukifanya mabaya kuna adhabu. Na pia kuna option ya kutubu sababu hakuna mkamilifu ila yeye tu.

So it's your choice and you must pay the price for your selection
it's said that kabla ya mtu kuumbwa mungu mwenyewe anakuwa anajua hatima ya kila mtu kuwa ni wa peponi au lah hata kabla hajaumbwa, si ndio?
 
A

Angeweza kutuumba kama robots lakini nahisi asingejivunia uumbaji wake lakini pia alituacha tuamue kwa hiari yetu tunachopenda kufanya ndio maana akatupa utambuzi wa mema na mabaya, yaani kwa lugha rahisi yeye sio dictator ila utavuna ulichopanda.
Ukisema anajivunia hata kwa mabaya pia anajivunia coz they are all from within
 
Ukisema anajivunia hata kwa mabaya pia anajivunia coz they are all from within
😂😂😂 duh labda, lakini sidhani kama anajivunia sababu amekupa uwezo wa kuchanganua mambo sio ufanye tu sababu unaweza kufanya.
Ni kama sasa ivi una uwezo kabisa wa kuvua nguo hadharani lakini sababu ufahamu wako unakwambia ili sio jema huwezi kufanya ivyo na hata ukifanya huwezi jivunia au familia yako haiwezi jivunia wewe kwa ulilofanya.
 
inatokana na sifa ya kujua kila kitu. So ukisema hauna uhakika that means huyo mungu huwa hajui kila kitu.
Point of correction, mi sio Mungu am trying to defend what I think I know

Mimi ndio sina uhakika, na siwezi kubali kitu ambacho sija experience au kuona mtu ka experience, ni maneno ya kusadikika.
 
Point of correction, mi sio Mungu am trying to defend what I think I know

Mimi ndio sina uhakika, na siwezi kubali kitu ambacho sija experience au kuona mtu ka experience, ni maneno ya kusadikika.
kwenye biblia na nahisi pia quran japo sina uhakika huko wametaja hiko kitu kuwa huyo mungu ni mjuaji wa yote hata kabla hayajatokea
 
A

Angeweza kutuumba kama robots lakini nahisi asingejivunia uumbaji wake lakini pia alituacha tuamue kwa hiari yetu tunachopenda kufanya ndio maana akatupa utambuzi wa mema na mabaya, yaani kwa lugha rahisi yeye sio dictator ila utavuna ulichopanda.
Sasa kwa nini hapendi wanaofanya mabaya?

Na uwezo wa kuyaondoa hayo mabaya alikua nao,

Utambuzi wa sisi kujua mema na mabaya ni dhahiri kwamba Mungu alipanga tufanye yote mema na mabaya.

Kama hapendi sisi tufanye mabaya asinge tupa utambuzi na ufahamu wa kutenda mabaya.

Labda useme kwamba anapenda mema na mabaya..
 
Hatujui kwamba Mungu yupo. Kwa sababu zamani watu walisema upinde wa mvua Ni msamaha wa Mungu Ila Leo hii hata wewe unaweza tengeneza upinde wa mvua. Walisema mvua Ni maji yanayomwajika kutoka madirisha ya mbinguni. Lakini hata wewe ukipika unaweza una process ya condensation. In short kitu usichokijua ndo unampa Mungu. Inaitwa God of the Gaps. Na hizi gaps zinaendelewa kuwa filled kila siku na wanasayansi mwishowe utakosa pa kumficha huyo Mungu wako. Na jicho kuwa complex hainiambii kwamba Mungu Ni Allah na anataka nisali nikiangalia mji wa waarabu. Kusema Mungu yupo na Mungu Ni Allah au yahweh Ni vitu 26 tofauti.
Kina nani wanasema upinde wa mvua ni msamaha wa Mungu,... Na kina nani wanasema mvua inamwagika kutoka madirisha ya Mbinguni?
Ukisoma Sayansi juu juu utasema hakuna Mungu Muumbaji..., Lakini ukiiingia deep zaidi Utajua kuna Mungu Muumbaji.
FuZ54rKWIAEZDVn.jpeg
 
Mkuu wahindu na wabudha wamekuepo hata kabla ya huyo ibrahim na walikua na dini zao au hujui mkuu???? Na unajuaje mungu aliumba wakati haukua nae umesimuliwa tu??????? UNATAKA KUMJUA MUNGU ILA KILA IMANI DUNIANI INA MUNGU WAKE NA NDIO MAANA TARATIBU ZA KUSALI ZIPO TOFAUTI.Mungu wa waislamu sio Mungu wa wakrsto na wayahudi na Mungu wa wahindu sio Mungu wa Wabudha.Mungu wa makabila yote ya kibantu sio Mungu wa dini za wakoloni wa kiarabu na kizungu waliovamia afrika.........!!!!!WEWE UNATAKA KUMJUA MUNGU YUPI MAANA KILA IMANI DUNIANI INASEMA MUNGU WAKE NI SUPER GOD?????
Kila Imani inamungu wao waliijitengenezea wenyewe

Lakini waumini wote wa hizo Imani ambao ni binaadam Mungu wao ni mmoja tu ambae ndio aliyewaumba wao , na vyakula vyao wanavyokula na hi Dunia wanayoishi

Jibu ni kwamba Mungu ni mmoja tu ila Kuna watu wengine hawamjui huyo Mungu wao ambaye ni mmoja tu

Na hawamjui Kwa sababu hawataki kumjua Kwa sababu Mungu alishaa jifunua kupitia manabii na vitabu
 
Sasa kwa nini hapendi wanaofanya mabaya?

Na uwezo wa kuyaondoa hayo mabaya alikua nao,

Utambuzi wa sisi kujua mema na mabaya ni dhahiri kwamba Mungu alipanga tufanye yote mema na mabaya.

Kama hapendi sisi tufanye mabaya asinge tupa utambuzi na ufahamu wa kutenda mabaya.

Labda useme kwamba anapenda mema na mabaya..
NAKAZIA
 
Nimekwambia designer wa vyote aliyeumba vyote kwa wakati mmoja Hayupo..

Ila kuna ma designer tofauti kwa wakati tofauti.

Ndio maana designer aliye gundua na kuumba Simu sie aliye gundua na kuunda Ndege au Meli...
Okay, swali langu ni hili.... Mtu pamoja na designed systems zote zilizopo kwenye mwili wake kwa ufahamu wako, zina Designer au hazina?
 
Sasa kwa nini hapendi wanaofanya mabaya?

Na uwezo wa kuyaondoa hayo mabaya alikua nao,

Utambuzi wa sisi kujua mema na mabaya ni dhahiri kwamba Mungu alipanga tufanye yote mema na mabaya.

Kama hapendi sisi tufanye mabaya asinge tupa utambuzi na ufahamu wa kutenda mabaya.

Labda useme kwamba anapenda mema na mabaya..
Hapendi mabaya sio wanaofanya mabaya ndio maana tukitubu tunaamini tunasamehewa angekua hatupendi asingetusamehe na asingepatikana asiye na mabaya sababu hatuna ukamilifu ndio maana tumepewa nafasi ya kujutia mabaya na kutubu.
 
Back
Top Bottom