Naamini Mungu yupo ila nashindwa kuuelewa ukamilifu wake, labda muendelee kunifunza

Nimekwambiaje NASA hawawezi kusema ni gharama ili halu pesa ni white house inatoa siyo wao.

White house ndiyo ikisema bajeti haitoshi ni haitoshi.

Nimekwambia hapa kuwa Marekani wameanza kufanya mpnago kumrudisha binadamu mwezini since 2018 chini Rais TRUMP.

Na trump alikadiria kuwa 2022 tayari NASA watakuwa washapeleka watu mwezini lakini bado walisogeza mbele kwa sababu vifaa (rocket na mavazi) bado hayajakamilika.

But wamesema saivi wanatazamia kwenda 2024 na tayari timu ya kwenda majina yao yashatajwa na mzabuni aliyeingia ubia na NASA ni kampuni ya Elon Mask (space X) ndiyo inayo tengezea rocket itakayowabeba wanasayansi hao ambayo inaitwa Artems -1 na sasahivi tayari inafanyiwa majaribio ili ikae sawa kwa ajili ya safari hiyo ya mwakani.

Sasa wewe unabisha endelea kushikilia data zako sijui za mwaka gani
 
 

Attachments

  • Screenshot_20230501_125854_Chrome.jpg
    83.9 KB · Views: 7
 

Attachments

  • Screenshot_20230501_130109_Chrome.jpg
    103.2 KB · Views: 7
Ndugu. Hio iko kwenye schedule, na inaweza isitokee pia. Ndio kauli yao NASA waliotoa.

Schedule ilikua 2024 wapeleke watu orbit ya mwezini na 2025 watue mwezini. Hio ya majina wanakaa wanabadili kila siku... mara waseme watapeleka mwanamke mwezini mara waseme watapeleka watu weusi wa kwanza... kiufupi hakuna tarehe maalumu waliopanga kutua mwezini.

Na sababu ya kutokwenda mwezini kwa zaidi ya miaka 50 inabaki ileile; cost!

Mwanzon ulikua unabisha kua NASA hawajatua mwezini..? [emoji848]
 
MImi sijakwambia kuna tarehe specific ya kwenda.

Ndiyo maana nimekwambia mpango huo waliuzindua 2018 wakitegemea utafanikiwa 2022, lakini wakafeli na sasahivi wamepeleka 2024.

Na hata 2024 bado wanaweza kufeli wakaenda 2030 mimi hilo sina shida nalo cha msingi tunasubiri mipango yao kama itatimia.

Mimi ninachokukatalia ni wewe kusema kuwa NASA hawana mpango wa kwenda mwezini kwasasa, mara useme pesa hamna, mara useme hakuna umuhimu wa kwenda mwezini kwa sasa, kama wewe umeona hakuna umuhimu basi wao wameona kuna umuhimu ndiyo maana sasahivi wanapanga mipango kazi ya kurudi huko
 
Hizo ni statement zao wao wenyewe. Walisema kua kupeleka binadamu ni less efficient kwasababu ina require alot of resources kupeleka wakat hakuna faida ya kupeleka binadamu. Walisema wao wenyewe sio mm.

Na sijasema hawana pesa. Bali walisema inagharimu pesa nyingi zaidi in excess.
 
Kwahiyo mkuu nawewe unaamini kuwa Pyramid zilijengwa na wayahudi?

Anyway let's say walijenga wao, kama walijenga wao nini kinazuia hadi leo hii kusiwe na pyramid mpya?

Technology waga haipotei bali watu wanachange matumizi kulingana na Zama zilizopo, Zama zilizopo bado zinahitaji technology iliyotumika kujenga pyramid kwa nini ipotee?

Kama pyramid zilijengwa na wayahudi inakuaje hadi leo hii watu wanaendelea kufanya tafiti yalijengwa na nani? Ata kama utasema wazungu wanaficha kwani hao wayahudi hawapo kuprove kwa Dunia kuwa wajenzi ni wao?

Katika harakati zako za kutaka kumfahamu Mungu muumba wa vyote najua umesoma vitu vingi ikiwemo baadhi ya dini na science Je Umewahi kuwasoma Annunaki?

Je Umewahi kufatilia vitabu/maandiko ya Sumerians wanaongeleaje kuhusu Annunaki na kuumbwa Kwa homo sapiens duniani?
 
You should be one of those conspiracy theorists. Lol

Pyramids zilijengwa na wamisri wenyewe. Bado hatuna uhakika kama walijenga ni watumwa au ilikua ndio ajira yao. Ila Pyramids zilijengwa kwa kusudio la kuzika mapharao na mali zao. Unamaanisha nn kusema kua hatujui Pyramids zilijengwaje?
 
Sidhani kama kuna mahali nimesema kuwa nakubali piramidi zilijengwa na wayahudi, bali nimeelezea ni kina nani huwa wana dhana hiyo ya piramidi kujengwa na wayahudi au Aliens.

Na nikasema kwa mujibu wa Afro-centric ni kwamba wamisiri wenyewe ndiyo walihusika na ujenzi wa piramids
 
Hueleweki unachokitaka
 
Zamani za upumbavu Mungu alijifanya kama hajui au asikii ila sasa anataka ujue na usikie ili ukiukumiwa usijesema umeonewa
 
Mkuu Pyramid zimekuwepo ata kabla ya uwepo wa Pharaohs na kitu kingine unatakiwa kujua kuwa Pyramid hazipo Egypt tu, kuna zingine zipo North America kwahiyo na huko walikuwa wanazikwa kina nani?

Unaniita mie mtu wa conspiracy ilhali wewe mwenyewe huna ushahidi kuwa pyramid zimejengwa na wamisri wenyewe

Na kama zilijengwa na wamisri hao wamisri wote pamoja na vizazi vyao wamekufa? ili wawe wamekufa na ujuzi wao

Technology iliyotumika kujenga pyramid katika miaka ya 2780 BCE Hadi kufikia Karne hii ya 21 bado hatuna hiyo technology alafu tukae tunaambiana kuwa zilijengwa Kwa lengo la kuweka pharaoh

Kwa Akili ya kuvukia barabara tu ni impossible kuwa wamisri ndio walijenga pyramid na kama walijenga nini kinawafanya wasijenge tena?

Wamisri walishiriki tu kwenye ujenzi kama saidia fundi ndomana hakuna wanachokijua, kitu walichonufaika nacho ni kujifunza vitu ambavyo vilikuwa ndani ya uwezo wao kutoka kwa Annunaki ikiwemo science ya madawa na ujenzi
 
Duh... inabidi uende walau sikumoja kutembelea Pyramids of giza. Watu wanatunza historia. Izo mambo ya kwamba Pyramids zmekengwa na aliens walianzisha conspiracy theorists. Wamisri wao wanajua kila kitu... ni mahesabu makali tu. Pyramids zilichukua miaka zaidi ya 20 kujenga Pyramid moja. Na watu 20,000-100,000.



Kuhusu Pyramids za North America nenda Wikipedia uangalie kuhusu mesoamerican Pyramids... hakuna miujiza.
Na swala la kwann hawajengi Pyramids tena ni sawa na kuuliza kwanini hatuui albino tena na kuabudu makaburi? Jibu ni hawafuati tena hizo desturi.

Na sio kila mtu alizikwa kwenye Pyramids, ni mapharao tu sanasana. Na matajiri. Walikua mummified na kutunzwa humo pamoja na mali zao. Ww unafkir kwann wanahusisha sana mummies na Egypt, hata kwenye movies nyingi?
 
Shida hizo nchi unazoita shitholes zilikuwa masikini hata kabla ya dini. Hivi wewe kwa akili yako unadhani wazungu walianza kusali na waafrica kanisa moja walivofika tu. Haya tuambie nyinyi maatheist taifa mmelifanyia nini mpaka watu wawafuate tuanzie hapo. Unazungumzia amani japan amani za mapanga na mapigano ndo amani kwako. Masamurai wanafanya nini kule maninja wanafanya nini kule kwanini wanatengeneza misilaha mizito? Sababu wanajua amani yao sio ya milele sababu kuna kipindi walitandikwa na wenzao tofauti na ukisali kweli unapata amani ya milele.
 
Sasa wale jamaa walifundishwa upendo upole amani na babu zao na ndo maan walikuwa hawafanyi maafa makubwa duniani. Na watu walikuwa wanawatawala sababu ni wasikivu na ni mabrave sana kwa watawala wao na Mungu aliwatoa ile roho ya ubaya wa kutisha kutokana na ujuzi wao wangetesa dunia sana. Na pia yale yote yalitabiriwa katika bible kuwa watatawaliwa na watapoteana kabisa kwahyo matukio hayo ya kihistoria unayoyaona hata kibiblia yaliandikwa hivo hivo. Na ndo maan walivokuja katika modern world kuna baadhi wakaungana na wanatoa kipigo kikali sana kwa yoyote atakaewachokoza ila wao hawachokozi mtu na bado sio wote walioungana kupiga watu hata hivi karibuni. Ila wale wakiingia sehem wanaweza fanya chochote kile hujui kuwa watu wenye power zaidi duniani na hasa pale marekani ni hao hao jmaa pamoja na kwamba walichukuliwa utumwa marekani. We unajua kwanini mpaka mwanamuziki Kanye West aliwachukia sana wanavowapiga na kuwanyanyasa watu weusi hasa kwenye media wao nd wanapanga nani awe star nani ashuke. Unaijua familia ya kiyahudi ya Ku klax klan wabaguzi wa rangi wa kutisha wenye power za juu pale U.S. Bro myahudi akiruhusiwa evil things ni mtu wa kutisha kuliko ukoma.
 
Hukumu ya mababu zetu wa kale Mola ndie ajuaye
 
Karibu uone tofauti Quran haina migongano hata kidogo na Quran imeruhusu kuhoji yaliyomo kwa kadri yako
 
Sasa mkuu misri ndo alimtawala myahudi kwahiyo kwa haraka haraka misri alikuwa ana uchumi imara zaidi yao na pia ilikuwa ni nchi yenye maendeleo makubwa hata ya kisilaha na vitu kama hivyo na biblia inaweka wazi kuwa hata kabla ya kutawaliwa waisrael walisaidiwa sana na misri kipindi cha shida na njaa katika taifa lao. Kwahyo biblia inavoonesha kuwa wayahudi walitawaliwa na kuwasaidia katika baadhi ya technlogy haiwadowngrade misri lakini ndo inawakuza zaidi. Kumbuka biblia inasema kuwa mkombozi wa wana wa israel wamekombolewa na mtoto alielelewa kwenye mikono ya farao mwenyewe so utaona hapo kuwa hakuna kudharau historia ya africa wala nini. Bible imeelezea vizuri taifa la ethiopia kwa uzuri tu na kuna wayahudi wengi wameishi ethiopia na katika historia ya africa utaona hayo mataifa hayajatawaliwa na mtu yoyote. Ila huku kwingine ni kweli africa ilikuwa giza tupu na hakuna ustaarabu kabisa. Nakupa uthibitisho mdogo tu ukienda vijijini maswala ya kuamini uchawi na pia aina ya maisha mpak leo vijijini vyoo tu ni shida nyumba za kuishi ni duni elimu duni mavazi duni em fikiria vijiji maji safi tu ni changamoto chakula cha ajabu ajabu tu sasa unawezaje kubisha. Hapo pa mkwawa Iringa unapopasema ni pa hovyo ajabu maisha duni so sometimes kutawaliwa ni kweli lilikuwa kosa regardless tulikuwa tuna hali gani ila kuukataa uhalisia kuwa hatkuwa na hali mbaya naona ni kuukata uafrica wenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…