Naamini Mungu yupo ila nashindwa kuuelewa ukamilifu wake, labda muendelee kunifunza

Iko hv mungu aliwaumba hao na kisha akawapa akili na utambuzi wa mema na mabaya yaani uhuru was kuchagua na si kuwanga ufahamu ili wamtii yeye tu

Basi baada ya kuwapa utashi Mungu mwenyewe kwa matakwa yake akaona kwenye utashi huo aliowapa basi watakao ishi mapenzi yake watakua wake na watao enda kinyume wataadhibiwa.


Mwisho nikukumbushe Kuna kitu kinaitwa madaraka yaan mtawala anakuwa na pawa ya kufanya chochote kimpendezacho yeye kwenye himaya yake

Kama ataamua mchinjane na watakao pona ndio raia wake it's ok pia

Kama ataamua watoto wote chini ya miaka mitano wauwawe it's ok pia rejea heroda na kuzaliwa kwa yesu.

Namaanisha tupige ibada tu mengine Ni ya Mungu mwenyewe!
 
Huko vitabuni ni utata mtupu vinahadaa tu hivyo vitabu hamna ukweli
 
Huko vitabuni ni utata mtupu vinahadaa tu hivyo vitabu hamna ukweli

Hakuna kitabu chenye utata kukielewa kama Biblia.

Kuna baadhi hadithi mule ukizisoma hazieleweki yaani kama zinaenda mbele au zinarudi nyuma.

Alafu kinachonichoshaga zaidi kina mafumbo kibao na hayo mafumbo unakuta kila kukundi wanatafsiri tofauti na kikundi kingine kwenye kitu kile kule.

MFANO : Kitabu cha ufunuo wa Yohana ni mafumbo matupu.


Sijajua kuhusu Quran kama nayo hadithi zake zinazikanyaga kanyaga kama za kwenye Biblia, na mafumbo pia sijui kwenye Quran kama yapo
 
Zote ni zilezile hadithi za hekaya
 
Cha kwanza inabidi ujue kuwa dini zimetengenezwa na binadamu ili waweze kujibu haya maswali unayouliza na pia ili kuendesha maisha ya watu
Cha Pili kuhusu Lucifer sijui na Eva hizi Ni story tu katika dini za ki Abraham ambazo zimetungwa kuelezea jinsi matatizo duniani yalivyoanza. Na yamemtumia mwanamke Kama chanzo Cha maovu duniani kwa sababu jamii zilizotunga hizi story zilikuwa zinachukulia wanawake Kama viumbe duni na nyoka pia walichukuliwa wanyama wabaya Sana ndo maana wakapewa hii story. Nadhani wagiriki na wamesapotamia Wana story Kama hii Tena za kwao Ni za zamani zaidi na pia dini zao ziliamini kuwa mwanamke alisababisha vyote.
Dini haiwezi kukupa majibu unayotaka Ila Sayansi imetoa majibu mengi na tumeweza jua kuhusu vitu vingine ulimwenguni na Kama unaona maswali yako yatajibiwa na kitabu kilichoandikwa kipindi ambacho watu hawakujua jua linaenda wapi usiku na watu walijua nyota zinaweza anguka duniani siku ya mwisho, Sawa Ni maamuzi yako pia
 
umekaribia kuchanganyikiwa kwa kujifanya great thinker. Kafanye shughuli zitakazokuletea mkate
 
Kwa Nini kuwe na designer? Na kwa Nini awe mtu.. na ukiulizwa aliyemdesign huyo mtu.. utajibuje
 
Huwezi kutumia mind kuelezea ukuu wa Mungu,since iko limited mnoo. Kitu pekee unacho weza kuelezea ni kile ulicho experience. You have to go beyond the Egoic Mind ili umtambue Mungu.
Hivi Ni visingizio vya dini... Kama kitu hakieleweki hakieleweki tu..hamna Cha kusema huwezi elewa, mbona vingine vinaeleweka. Walioandika hivyo vitabu wameandika hisia zao ndo maana kwa elimu na Sayansi ya saa hivi unaona mapungufu.
 
Ndo maana nakuambia kwamba zote Ni story. Hukumu ya motoni haipo kwenye agano la kale. Imeanzishwa kwenye agano jipya, kwa Nini. Ili kutishia watu katika kuamini dini ya kikristo. We kwanini aumbe viumbe ambavyo anajua hatima Yao Ni kuungua milele, hizi Ni mbinu tu za kudaka akili za watu ndo maana kila dini duniani Ina mbingu na Moto jiulize kwa Nini.
 
Kitabu Cha ufunuo, wakristo wanakiita mafumbo kwa sababu hawataki kuamini kimeandikwa vitu vya uongo kuhusu nyota kuangushwa angani na mkia wa Dragon, viumbe vya ajabu na hivyo. Ndo maana wakristo wanakikimbia kile kitabu. We Nani kakuambia aliyeandika alisema Ni mafumbo. Basi mi nasema kitabu kizima mafumbo. Wakristo wanachagua wanachoamini na wasichoamini wanaita mafumbo ili watered dini Yao
 
Hahaha yaani we unatetea kwamba madaraka ndo mtu aue watu, aunguze miji, afurike dunia. We kamtese mtoto wako Kama hufungwi. Hata viongozi wanashtakiwa wakiua, zile Ni story tu zisiwachanganye.
 
Mkuu kuna vitu vinne muhimu nime-notice kwako ambavyo ni :

1. Akili/utashi (ufahamu wa kutambua zuri na baya)

2. Uhuru wa kufata unachotaka (yaani umepewa demokrasia).

3. Madaraka(Mungu ana mamlaka ya kuamua mwenyewe awafanye nini watu wake hata kama vitawaumiza watu hao).

4. Mungu anajua mwenyewe kwanini aliamua/ameamua iwe hivyo ilivyokuwa/kutendeka, kwa hiyo kuhoji kupata sababu ni sawa na kupoteza muda maana huwezi kupata majibu ya kuridhisha.

Lakini kati ya hayo mambo manne niliyo-notice kwako, jambo la kwanza na la pili (utashi na uhuru wa kufata ninachotaka) siyo mara ya kwanza kuyaskia.

Ila 3 na 4 (madaraka na siri za Mungu mwenyewe) ndiyo ni mara ya kwanza nayaskia kwako, na nakushukuru sana kwa kunipa knowledge mpya.

Lakini mkuu bado maswali yangu hayawezi kuisha hata kama Mungu ametupa UTASHI na DEMOKRASIA ya kuchagua ninachotaka.

Kwenye maandiko ya Biblia, kuna mstari unasema kuwa "Binadamu ni wa thamani sana mbele za Mungu".

That means,pamoja na kwamba sisi ni mojawapo ya asset tu za Mungu, lakini inaonekana Mungu hatuchukulii kama hatuna thamani maana ameshasema kuwa binadamu ni wa thamani mbele zake.

Sasa kama ni wa thamani kwanini aruhusu wengi kupotea kuliko wale wanaofata sheria zake ?

Kwanini amlete kiumbe duniani(shetani) mwenye nguvu kuliko sisi ambaye anajua kabisa lazima atafanikiwa kutupotisha wengi ? Kama kweli Mungu anatupenda na hataki tupotee kwanini amshushe shetani kwetu wakati anajua kabisa yule alikuwa ni malaika lazima ana nguvu kutuzidi ? Upendo wa Mungu uko wapi hapa ? Je, kutuletea shetani ndiyo upendo ? Kwanini asingemtupa kwenye sayari nyingine baada ya kuasi na badala yake kamtupa duniani ? Unawezaje kusema unatupenda wakati umetutupia adui anetuongoza kwenda motoni ?

Na Je, kama kweli Mungu hapendi na kuchukia MAOVU/DHAMBI, kwanini sasa aruhusu yatokee ?

Hivi wewe kitu usichokipenda utaruhusu kitokee ?
 
Bro, ndo maana nakuambia hizi zote Ni story tu za kujaribu kuelewa dunia. Zimeandikwa na makabila miaka elfu 3 iliyopita ambayo hata haikujua kwamba dunia Ni ndogo kuliko jua. So usitegemee watu Hawa ndo wawe na majibu ya maswali yako wakati hata we saa hivi umewazidi akili wote walioandika hizi story.
 
Watakatifu wetu wanawaita mizimu/mashetani wakati huo huo wakaja na mizimu/mashetani yao wakatuambia ni watakatifu wakina yesu,,, mtume Mohamed,,,wakina petro,,paulo,,yakobo nk nk hao wote ni mizimu tu tunayoiomba kwa kuwa ni wafu tuu kama mababu zetu!!
 
Heeewalaaa
 
Kaa kimya kama huelewi acha hearsay zama deep utakuja na experience Tofauti
 
Kaa kimya kama huelewi logic ya haya mambo achana na hearsay zama deep utarudi n experience Tofauti!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…