By the way dini inaweza isiwe suala la kubwa kwangu.
Lakini ni kwamba, nikisoma nadharia zingine hasa sayansi ya AUSTRONOMY inanifanya mimi kwa mawazo yangu mwenyewe ni conclude tu kusema Mungu yupo.
Mfano : katika sayansi ya anga za juu (Austronomy) ni kwamba kila kitu kilichoko angani kinazunguka (every object in the universe is moving or is in motion).
Ni kama na maana kwamba Dunia inazunguka,Mwezi unazunguka,Sayari zote zinazunguka,Jua linazunguka,Galaxy (mkusanyiko wa nyota) zinazunguka,Black holes zina zunguka n.k
Yaani kifupi ni kwamba hakuna kitu hata kimoja ambacho kimo hewani kimesimama wima tu hakizunguki,every object is in motion.
Lakini sasa kinachonishangaza, kwenye hii tasnia ni kwamba "ulimwengu unazunguka kwa kufata kanuni maalum".
Yaani unavyoviona angani vyote vinazunguka kwa kufata system/formula ama mfumo maalum na ndiyo maana huoni vikigongana hovyo wakati ukiangalia ni kama viko shaghala paghala (bila mpangailio).
Isingekuwa hivi vitu viko kwenye mfumo maalum basi dunia yetu hii ingeshagogwa na vitu vingine vikubwa sana angani na ingeshasambaratika muda tu.
Coz kwenye anga kuna vitu vikubwa sana ambavyo ukifananisha na Dunia, Dunia itaonekana kama kipande cha kokoto tu.
Hivyo basi, universe kuwa katika mpangalio maalum na kufata kanuni , ndiyo kunanifanya nipate wazo kuwa "Lazima kutakuwa na fundi aliyedizaini hivi vitu na kuviongoza (kama remote controller).
Trust me huu ulimwengu usingekuwa na fundi maalum wa kuungoza basi vitu angani vingekuwa vinagongana kila dakika hata dunia sasahivi isingekuwepo ingeshafanywa kifusi mda.
Sasa huyo fundi ndiye nimekuja kudhani kwamba ndiyo atakuwa huyo Mungu anaesemwa kwenye vitabu vya dini.
Lakini sasa nimeenda na kwenye vitabu vya dini, sifa anazopewa nikilinganisha na matukio ya baadhi ya vitu humo humo kwenye vitabu vya dini, naona kabisa vinakosa ushirikiano/haviendani.
Nimeamua nikupe mfano mmoja tu wa AUSTRONOMY, ila ukitaka mwingine pia nitakupa