Naamini Mungu yupo ila nashindwa kuuelewa ukamilifu wake, labda muendelee kunifunza

Naamini Mungu yupo ila nashindwa kuuelewa ukamilifu wake, labda muendelee kunifunza

Ukiangalia kwa ukaribu upande wa dini ulikua na ni mpango wa mwanadamu kuutafuta ukweli ama nguvu ambayo ni kubwa kuliko sisi.
Sasa katika hizo harakati za kutafuta kila mmoja kaja na nadharia tofauti kulingana na exPerience yake.

Ukiangalia kwa ukaribu zaidi ni kwamba dini unaweza kua ulikua ni mpango mzuri zaidi labda wa kujiunganisha na huyo alie mkubwa kuliko sisi, lakini kilichotokea na kinachotokea ule ambao ukweli ulioanza kuonekana au umewahi kupatwa umebadilishwa kila mmoja akiserve interest anazozijua yeye.

So kuelewa vizuri ni bora kuanza kujitizama kuanzia ndani (look within) I'm uta-experience kwa namna tofauti na kuachana na hizi stori stori zingine.
Mkuu una kitu, utafika Mbali sana
 
Wakuu poleni kwa upambanaji.

Binafsi mimi kuna mda huwa nikitulizaga kichwa changu huwa naanza kujiuliza maswali mengi sana kuhusu mimi (binadamu) na ulimwengu kiujumla (Universe).

Maswali kama sisi (binadamu) ni kina nani,tumetoka wapi asili yetu, kwanini tupo (dhumuni la kuishi), mwisho wetu ama hatima yetu ni nini, Ulimwengu wa vitu je kama sayari, nyota, galaxies zimekuwepo vipi na nini hasa mwisho wake.

Hapo juu ni baadhi tu ya maswali ambayo huwa naiuliza sana akili yangu ikiwaga katika hali ya utulivu.

Lakini cha kusikitisha ni kwamba, katika maswali yote hayo ambayo huwa najiuliza, sijawahi kupata jibu la uhakika kuniridhisha kuhusu hayo maswali yangu.

Nimekuwa nikifanya bidii kubwa sana kupata majibu ya maswali yangu kupitia usomaji wa majarida au vitabu vihusuvyo historia,sayansi, dini na Falsafa lakini kote bado sijapata majibu ya kuniridhisha tofauti na kuambulia majibu ya kinadharia tu ambayo yana strength kiasi chake lakini pia yana weakness sehemu nyingi tu.

Na nikiri wazi tu kuwa katika usomaji wangu wa nadharia hizo zote (historia, sayansi, dini, falsafa) sehemu ambayo nimeanza kuiamini kunipa majibu ya maswali yangu ni kwenye DINI.

Nikiwa na maana nimeanza kuamini kwamba uwepo na sisi tuliohai na visivyo hai hapa ulimwenguni ni matokea ya Uumbaji ya nguvu kubwa sana inayoitwa MUNGU/ALLAH kama ambavyo dini nyingi zinaelezea nguvu hiyo.

Na leo maswali yangu yanajikita huko kwenye hiyo nguvu (Mungu) maana nimeanza kuiamini lakini pia kila nisomapo BIBLIA (mimi mkristo) inanipa maswali chungu nzima.

Sasa leo swali langu limejikita kwenye UKAMILIFU wa MUNGU.

Naombeni wasomaji mnielewe kuwa sina maana ya kukufuru (maana mara nyingi niulizapo maswali kuhusu MUNGU huwa naambiwa nakufuru) bali mimi nataka kujifunza zaidi kumuhusu huyu Mungu.

Dini nyingi (hasa Ukristo na uislamu) zimekuwa zikimwelezea Mungu kuwa ni Mkamilifu sana,mwenye nguvu nyingi sana, uwezo na akili zake hazichunguziki, hashindwi na chochote n.k.

Je hilo lina ukweli ? kupitia Biblia mimi nimeanza kudhani kwamba huenda kweli Mungu ana nguvu nyingi sana ila siyo zote, ana uwezo mkubwa sana ila siyo uwezo wote,ana maarifa mengi sana ila siyo maarifa yote, ana ukamilifu mwingi sana ila siyo ukamilifu wote n.k

Nasema haya ni kutokana na maswali yafuatayo :

1. Kama Mungu ana ukamilifu wote, kwanini sasa alimuumba malaika (Lucifer/shetani) alafu badae akaja kumuasi?
Kama Shetani/Lucifer aliasi maana yake ni kwamba Mungu alimuumba huyu kiumbe akiwa na madhaifu kadhaa na ndiyo maana alishindwa kuitii amri/mamlaka ya muumbaji wake.

Kama Mungu angelikuwa na ukamilifu wote, basi malaika wote wangelikuwa wameumbwa katika namna ya utii pekee, uasi usingetokea na huo uasi unadhihirisha kwamba Mungu aliwaumba hawa malaika wakiwa na udhaifu flani, hawakuwa na uimara wote.

2. Uumbaji wa Eva (Hawa) unaonesha kulikuwa na madhaifu pia.
Katika Biblia takatifu kwenye kitabu cha mwanzo, kuna mistari inaeleza kuwa "Mungu alimpa usingizi mzito Adam, alafu akabandua sehemu ya ubavu wake na kumfanya/kumuumba mwanamke (Hawa/Eva)".

Alafu Mungu akamwambia Adam kuwa huyu mwanamke atakuwa msaidizi wako

Lakini ni huyo huyo mwanamke ambae shetani (kwenye umbo la nyoka) alienda kumdanganya akachukua matunda ya mti walioambiwa asile yeye akala na akampelekea na mumewe (Adam) pia akala.

Lakini Mungu alivyomuuliza Adam kwanini umekula matunda ya mti ambao nilikwambia usile, Adam alijibu kuwa "Ni huyo mwanamke uliyenipa ndiye aliyeniletea nikala".

Tukio hili linadhihirisha kuwa Mungu alimpa Adam msaidizi (Hawa) ambae ni dhaifu sana na ndiyo maana alisababisha dhambi ikaenda hadi kwa Adam.

Na huenda kama Mungu angelikuwa amempa Adam msaidizi imara asiye na madhaifu basi ile dhambi ya kula tunda ingeepukika.

Uko wapi sasa ukamilifu wote wa Mungu ikiwa aliweza kuwaumba malaika dhaifu (ambao walikuja kumuasi) na pia bado akampa Adam msaidizi dhaifu kabisa ambaye alisababisha dhambi imwendee hadi Adam?

Kwa leo naombeni comment zenu zinifunze kuhusu hilo tu (La ukamilifu wa Mungu) alafu mengine nitauliza siku nyingine, na mengine nitakuwa nauliza humo humo kwenye comments zenu.

NB: Naamini Mungu yupo, kutokana na baadhi ya vitu ninavyoviona ulimwenguni (hasa uumbaji/creation) ambapo kuna baadhi ya vitu hasa sayansi inakosa majibu ya kuridhisha, ila shida yangu kubwa ni sifa za Mungu ambazo anapewa na wanadamu naona kama zinashindwa kujidhihirisha kwenye baadhi ya mambo.

Karibuni mnifunze.
Malaika hajawahi kupinga amri ya Mungu na aliwaumba hivyo wanafanya wanachomrishwa na Mungu

Aliyepinga kumsujudia Adam ni Jini na Majini wamepewa Freewill kama alivyo Kwa binaadam na Kwa sababu binaadam na Majini wamepewa Freewill ndio maana wamewekewa moto na pepo

Quran 15:26
Na tulimuumba mtu kwa udongo unao toa sauti, unao tokana na matope yaliyo tiwa sura.

15:27
Na majini tuliwaumba kabla kwa moto wa upepo umoto.

Na sababu ya Ibilisi kukataa kumsujudia Adam ni majivuni yake tu anasema yeye ni Bora Kwa kuwa yeye ameumbwa Kwa moto

Quran 7:12
Mwenyezi Mungu akasema: Nini kilicho kuzuia kumsujudia nilipo kuamrisha? Akasema: Mimi ni bora kuliko yeye. Umeniumba kwa moto, naye umemuumba kwa udongo

Kuhusu Adam na hawa kula tunda waliikazwa pia ni sababu Wana freewill Yani Wana uwezo wa kufanya chocho hata kile ambacho wamekatazwa na Mungu

Binaadam ameumbwa Kwa udongo ana Nafsi na matamanio

Jini ameumbwa Kwa moto ana Nafsi na matamanio

Malaika wameumbwa Kwa Nuru Nafsi wanayo lakini hawana matamanio
 
Mkuu kuna vitu vinne muhimu nime-notice kwako ambavyo ni :

1. Akili/utashi (ufahamu wa kutambua zuri na baya)

2. Uhuru wa kufata unachotaka (yaani umepewa demokrasia).

3. Madaraka(Mungu ana mamlaka ya kuamua mwenyewe awafanye nini watu wake hata kama vitawaumiza watu hao).

4. Mungu anajua mwenyewe kwanini aliamua/ameamua iwe hivyo ilivyokuwa/kutendeka, kwa hiyo kuhoji kupata sababu ni sawa na kupoteza muda maana huwezi kupata majibu ya kuridhisha.

Lakini kati ya hayo mambo manne niliyo-notice kwako, jambo la kwanza na la pili (utashi na uhuru wa kufata ninachotaka) siyo mara ya kwanza kuyaskia.

Ila 3 na 4 (madaraka na siri za Mungu mwenyewe) ndiyo ni mara ya kwanza nayaskia kwako, na nakushukuru sana kwa kunipa knowledge mpya.

Lakini mkuu bado maswali yangu hayawezi kuisha hata kama Mungu ametupa UTASHI na DEMOKRASIA ya kuchagua ninachotaka.

Kwenye maandiko ya Biblia, kuna mstari unasema kuwa "Binadamu ni wa thamani sana mbele za Mungu".

That means,pamoja na kwamba sisi ni mojawapo ya asset tu za Mungu, lakini inaonekana Mungu hatuchukulii kama hatuna thamani maana ameshasema kuwa binadamu ni wa thamani mbele zake.

Sasa kama ni wa thamani kwanini aruhusu wengi kupotea kuliko wale wanaofata sheria zake ?

Kwanini amlete kiumbe duniani(shetani) mwenye nguvu kuliko sisi ambaye anajua kabisa lazima atafanikiwa kutupotisha wengi ? Kama kweli Mungu anatupenda na hataki tupotee kwanini amshushe shetani kwetu wakati anajua kabisa yule alikuwa ni malaika lazima ana nguvu kutuzidi ? Upendo wa Mungu uko wapi hapa ? Je, kutuletea shetani ndiyo upendo ? Kwanini asingemtupa kwenye sayari nyingine baada ya kuasi na badala yake kamtupa duniani ? Unawezaje kusema unatupenda wakati umetutupia adui anetuongoza kwenda motoni ?

Na Je, kama kweli Mungu hapendi na kuchukia MAOVU/DHAMBI, kwanini sasa aruhusu yatokee ?

Hivi wewe kitu usichokipenda utaruhusu kitokee ?
Swali zuri

Kama sisi Ni wa thamani mbona shetani ?

Ni kweli sisi ni wathamani lakini tu wa thamani na wenye nguvu katika yeye (tukifuata matakwa yake) nje ya hapo were useless rejea hadithi za nuhu na gomola. Aliteketeza kwa sababu hawakua na thamani tena

Pili shetani yupo ili kutu challenge kama kama Mungu alivyoamua mwenyewe kuwa tupitishwe kwenya majaribio makali na watakao shinda ndio wakwake.

Tatu rejea mfano wa baba na watoto wanne katika challenge ya kujificha.

Ndio anawapenda sana ila kaamua kuwapa challenge yeye kama baba.

Hiki kitu tunafanya hata kwenye familia zetu Kuna na wapa hard condition wanangu ili wawe bora zaidi na ngangari japo nawapenda

Karibu
 
So na wewe unaamini dunia nzima ilijaa maji? Kwa elimu yako ya historia na jiografia? Geological records zinaonyesha hii story Ni ya uwongo. Pia wamisri walikuwa wameshaendelea na hamna kipindi ambacho maendeleo Yao yalikatizwa na mafuriko ya dunia nzima. Story hii Ina makosa mengi nikianza kuongelea siwezi Maliza.
 
Malaika hajawahi kupinga amri ya Mungu na aliwaumba hivyo wanafanya wanachomrishwa na Mungu

Aliyepinga kumsujudia Adam ni Jini na Majini wamepewa Freewill kama alivyo Kwa binaadam na Kwa sababu binaadam na Majini wamepewa Freewill ndio maana wamewekewa moto na pepo

Quran 15:26
Na tulimuumba mtu kwa udongo unao toa sauti, unao tokana na matope yaliyo tiwa sura.

15:27
Na majini tuliwaumba kabla kwa moto wa upepo umoto.

Na sababu ya Ibilisi kukataa kumsujudia Adam ni majivuni yake tu anasema yeye ni Bora Kwa kuwa yeye ameumbwa Kwa moto

Quran 7:12
Mwenyezi Mungu akasema: Nini kilicho kuzuia kumsujudia nilipo kuamrisha? Akasema: Mimi ni bora kuliko yeye. Umeniumba kwa moto, naye umemuumba kwa udongo

Kuhusu Adam na hawa kula tunda waliikazwa pia ni sababu Wana freewill Yani Wana uwezo wa kufanya chocho hata kile ambacho wamekatazwa na Mungu

Binaadam ameumbwa Kwa udongo ana Nafsi na matamanio

Jini ameumbwa Kwa moto ana Nafsi na matamanio

Malaika wameumbwa Kwa Nuru Nafsi wanayo lakini hawana matamanio
So na wewe unaamini Kuna majini?
 
So na wewe unaamini dunia nzima ilijaa maji? Kwa elimu yako ya historia na jiografia? Geological records zinaonyesha hii story Ni ya uwongo. Pia wamisri walikuwa wameshaendelea na hamna kipindi ambacho maendeleo Yao yalikatizwa na mafuriko ya dunia nzima. Story hii Ina makosa mengi nikianza kuongelea siwezi Maliza.
Geological records ndo Nini?
 
Geological records ndo Nini?
Utafiti wa kijiolojia. Kuelewa Hali ya kihistoria ya udongo na mawe duniani. Wanaweza jua kwa kutafiti Kama sehemu fulani mda fulani kulitokea kitu fulani Kama Ni mafuriko tetemeko au mmomonyoko. In short hamna evidence ya dunia nzima kujaa maji na hiki kitu hakiwezekani kifizikia na kibiolojia
 
Mkuu tukiacha kuongelea binadamu ambae Mungu anasema amempa Akili na utambuzi wa mema na mabaya na mwisho wa siku akampa uhuru wa kuachagua afanye nini na aache kipi hii kitu ndio tunaambiwa inaitwa "Freewill"

Sasa naomba nikurudishe kwenye viumbe wengine wa Mungu ambao wao ni Malaika, hawa wameumbwa na Mungu kwa utofauti mkubwa na binadamu na miongoni mwa hizo tofauti ni kunyimwa hiyo "Freewill"

Bahati mbaya/nzuri Malaika hawajaumbwa na freewill, hivo hawana uchaguzi kama binadamu alivopewa Uhuru wa kuchagua kipi afanye na kipi afanye

Kwa lugha nyepesi ni kwamba wao ni kama Robots kwa Mungu, ambao kazi yao ni kutekeleza orders za Mungu only and not otherwise

Sasa swali linakuja, kama wao wameumbwa ili kufata Maagizo ya Mungu tu, waliopata wapi uwezo wa kuamua kama ilivo kwa binadamu, waliweza vipi kuji organise na kupanga kumpindua Mungu?

Majibu ni mepesi tu, kuwa hivi vitabu vimeandikwa na binadamu ndomana vina mapungufu mengi sana, ingekuwa ni vitabu ya Mungu kusingekuwa na contraindications za ajabu ajabu
Ngoja kwanza wapi huko pamesema malaika hana utashi.

Kabla sijaendelea
 
Utafiti wa kijiolojia. Kuelewa Hali ya kihistoria ya udongo na mawe duniani. Wanaweza jua kwa kutafiti Kama sehemu fulani mda fulani kulitokea kitu fulani Kama Ni mafuriko tetemeko au mmomonyoko. In short hamna evidence ya dunia nzima kujaa maji na hiki kitu hakiwezekani kifizikia na kibiolojia
Utafiti huo ni timilifu kwa asilmia ngap?
 
Utafiti huo ni timilifu kwa asilmia ngap?
Fatilia wewe Sasa.. kwa akili za mtu mzima ipi rahisi kuaminika dunia nzima kujaa maji au hizo tafiti. Haya wanyama wote wameeneaje kwenye lile boat. Na dunia kujaa maji kufunika milima inamaanisha watakuwa katika high altitude wanyama na watu wote wangekufa kwa baridi na pressure. Mwisho wa siku hii story ipo kwa wahindi na wamesapotamia na zimeandikwa zamani Sana inamaanisha imeibiwa. So inaonyesha iliandikwa na watu ambao hawana ujuzi wa dunia ndo maana Ina makosa mengi. Kasome the Epic of Gilgamesh (moja wapo wa hizi story za mafuriko..karibia kila dini inayo yake)
 
Maswali kama sisi (binadamu) ni kina nani
Kwa kawaida wengi hudhani ni huo mwili lakini sio kweli. Kwa wakristo ukisoma mwanadamu alivyoumbwa utajua wewe ni nani. Soma kitabu cha Mwanzo kwenye uumbaji

tumetoka wapi asili yetu,
Asili yetu ni Mungu mwenyewe na ni kama ilivyo asili ya kila unachokiona. Ila mwanadamu akapendelewa kwa kuwa na mfano wa asili yake yaani Mungu.

kwanini tupo (dhumuni la kuishi),
Dhumuni ni kuwakilisha uwepo wa Mungu duniani na kuitawala dunia na vyote viijazavyo. Lakini tumesahau dunia inatawala wanadamu. Ukielewa maana ya utawala utatawala kila eneo la maisha yako.
mwisho wetu ama hatima yetu ni nini,
Ni kutawala pamoja na Mungu milele. Mungu alishatukomboa tulikojichuuza. Kwa vile tuna utashi huru ni jukumu la mateka kuondoka utumwani au kubakia ikiwa umezoea utumwa. Mlango uko wazi yaani Neema.
Ulimwengu wa vitu je kama sayari, nyota, galaxies zimekuwepo vipi na nini hasa mwisho wake.
Ni kwa namna ile ile ulimwengu wetu umepatikana.
.
 
Fatilia wewe Sasa.. kwa akili za mtu mzima ipi rahisi kuaminika dunia nzima kujaa maji au hizo tafiti. Haya wanyama wote wameeneaje kwenye lile boat. Na dunia kujaa maji kufunika milima inamaanisha watakuwa katika high altitude wanyama na watu wote wangekufa kwa baridi na pressure. Mwisho wa siku hii story ipo kwa wahindi na wamesapotamia na zimeandikwa zamani Sana inamaanisha imeibiwa. So inaonyesha iliandikwa na watu ambao hawana ujuzi wa dunia ndo maana Ina makosa mengi. Kasome the Epic of Gilgamesh (moja wapo wa hizi story za mafuriko..karibia kila dini inayo yake)
Tunapo ongelea Mungu maana yake tunazungumzia muweza wa yote.

Kama aliweza kufufua wafu anashidwaje kuwafanya viumbe waishi kwenye anga za juu

Japo haikusemwa Ni futi ngapi above

Pia Mimi siamini 100% wataalamu walioshindwa hata kutabili mvua kiusahihi

Karibu
 
Mi nilidhani unataka kuuliza kwanini kuna watu wanaishi maisha yaliyonyooka na wengine tunataabika
Ni uchaguzi. Hicho ulichonacho ndicho uliomba kwa Mungu.

Kumbuka kuomba sio kupayuka na kukesha makanisani ukisali.
 
Lakini kabla hiyo imani ya Mungu mpya kuletwa, historia inaonesha kuwa Mababu zetu (Waafrica Weusi) walikuwa na imani zao kabla hata hizo za Mungu mpya kuletwa.
Lakini nguvu inayotenda kazi ni moja tu kwa imani yoyote. Ni Mungu muumba.

Umaweza ukawa na imani yako leo na ukapokea nguvu ya Mungu yuleyule muumba.

Ni somo refu na pana lakini ukweli ndip huo. Hata mchawi anaenda kwa nguvu ileile ya Muumba. Ndio maana kwa mawazo maovu ya wanadamu kuna maarifa Mungu amewafungia wanadamu.

Ova
 
Back
Top Bottom