Naamini Mungu yupo ila nashindwa kuuelewa ukamilifu wake, labda muendelee kunifunza

Energy is ability of doing work ...yaana pasipo energy hakuna kituchochote kinachoweza kuumbwa wala kufanyika ....kama wewe ni mkristo ndiyo maana maandiko yakasema vyote vilifanyika kwa yeye pasipo yeye hakuna chochote kinacho weza kufanyika ....kitu usicho kijua wewe na kukielewa ni mantiki ya kisanyansi inayo sema even matter is energy too .hapa kuna ufunuo mkubwa sana kuhusu mungu na vitu vyote na jinsi gani vimeumbwa
 
Concept yako ngumu kidogo ebu niwapishe wengine wajifunze kupitia wewe
 
Ninachopinga ni vitu vingi tu. Kwahio wanyama pia walikua concentrated katk eneo moja? Kwanzia kwa penguins mpaka tembo? Maana hapa hatuongelei binadamu tu... kitu kingine miti isingeweza kusurvive ikiwa submerged kwenye maji, ni michache sana.
 
Ninachopinga ni vitu vingi tu. Kwahio wanyama pia walikua concentrated katk eneo moja? Kwanzia kwa penguins mpaka tembo? Maana hapa hatuongelei binadamu tu... kitu kingine miti isingeweza kusurvive ikiwa submerged kwenye maji, ni michache sana.
Mkuu, fahamu kwamba Wanyama ndiyo walianza kuumbwa kabla hata ya Mtu hivyo Wanyama walikua washaanza maisha Yao kabla hata ya Wanadamu.

Na hiyo haimaanishi kwamba Wanyama wote walikua wanaishi kwenye hilo eneo moja lililotokea gharika,

Kuhusu miti, tunarudi pale pale kwamba gharika iliathiri eneo husika lote ambalo Nuhu alikua akiishi na watu wake ...... So kwa mantiki hiyo miti iliyokuepo kwenye eneo husika iliathirika lakini miti kwenye maeneo mengine ya Dunia haikuathirika.
 
Hivi ulishawahi kusoma kitabu cha mwisho kutoka kwa MUNGU kuja kwa walimwengu kinachoitwa QURAN?

Maswali yako yote yamejibiwa humo.

Ngoja nikueleweshe kidogo tu.

Kila unachokiona katika ulimwengu huu asili yake inatoka kwa Mwenyezi Mungu /MUNGU.

Mungu ameumba viumbe na vitu vingi sana katika ulimwengu huu ,vipo ambavyo tunavijua na vipo vingine tusivyovijua.

Katika viumbe vyenye utashi/akili...vimeumbwa vya aina tatu.
Mosi, ni viumbe vinavyoitwa MALAIKA, hawa ni viumbe walioumbwa wakiwa na utashi na asili yao ni Nuru .Malaika hawana jinsia,sio wanaume na wala sio wanawake kiufupi ni kuwa hawana jinsia kama tulivyo mimi na wewe. Hawana matamanio, hawali wala hawanywi.

Pia wao wameumbwa kwa ajili ya kutii tu amri za Mungu hivyo hawana uwezo wa kuasi hata kidogo.

PILI, ni viumbe wanaoitwa MAJINI, hawa ni viumbe walioumbwa kabla ya ujio wa mwanadamu katika ardhi hii,asili yao ni Moto. Hawa wanashabihiana sana na wanadamu katika sifa, ..wana jinsia, wana matamanio, wanakula, wanakunywa, wana akili, wanazaana n.k kubwa zaidi ni kuwa wana utashi na uwezo wa kuchagua (free will) jema na baya. Wamepewa uhuru wa kumtii au kumuasi Mungu. Kiufupi ni watenda madhambi na vile vile ni watenda wema. Lengo kubwa la kuumbwa viumbe hawa si lingine bali ni kumuabudu MUNGU pekee.

Tatu, ni viumbe viitwavyo BINADAMU (MTU) , asili yake ni udongo, wana jinsia ,wanazaana,wanakula,wanakunywa,wana utashi na vile vile wamepewa uhuru wa kutenda mema na mabaya.Kama ilivyo kwa majini, lengo kubwa la kuumbwa mwanadamu ni kuja kumuabudu Mungu katika ardhi hii.
 
KWANINI MUNGU alimuumba Ibilis /lucifer?

Kabla ya kukimbilia kulijibu hili swali ni vema kujua ibilisi ni nani?

Iblis sio malaika kama watu wengi wanavyodhani, sifa kuu ya malaika ni kuwa hawamuasi MUNGU bali wanafanya yale wanayoamrishwa na Mungu.

Iblis ni kiumbe ktk jamii ya majini, ameumbwa kwa Moto. Amepewa utashi na uwezo wa kutii ama kuasi amri za Mungu.Jini huyu alipata bahati ya kulelewa na kukua ktk kundi la malaika huko mbinguni .Alikuja kupewa mtihani na Mungu wa kuwa amsujudie Adam mara baada ya kushindwa mtihani waliopewa pamoja na malaika na Adam .Malaika walitii amri ya Mola wao ila iblis aligoma hivyo kupelekea kulaaniwa.
 
Sina maana hiyo, namaanisha uwe katika form ya uhai alafu maisha yaendelee

Mfano: kuna wadudu flani/panzi wale sijui senene wanaitwa, wanabiolojia hutuambia huwa wana-transform kuwa vipepeo.
Sasa hio si metamorphosis...ni kwa wadudu sio kwa binadamu. The answer is no. Ubongo ukishakufa na wewe umekufa. Mawazo yako fikra zako maamuzi yako maumivu furaha zote zipo kwenye ubongo.
 
Sijasoma katika quran's POV. Ila katk biblia tunaambiwa kua ndege walitumwa kuangalia level za maji. Mara ya kwanza wakarudi kuashiria miti bado iko submerged. Mara ya pili alirudi na tawi la mti kuashiria miti inaonekana afu ndio Nuhu akaachia ndege. [emoji2377]
 
Sasa hio si metamorphosis...ni kwa wadudu sio kwa binadamu. The answer is no. Ubongo ukishakufa na wewe umekufa. Mawazo yako fikra zako maamuzi yako maumivu furaha zote zipo kwenye ubongo.
Kumbe basi unatakiwa ukubali kuwa binadamu baada ya kufa ndiyo mwisho, wake hawezi ku-exist tena kama form ya uhai kwa namna yeyote kama ambavyo sayansi ina suggest kwenye vitu vingine.

Mfano wa vitu hivyo ni mfano Jua letu (THE SUN) ambalo tunaambiwa baada ya miaka kama bilion tano lita undergo process kadhaa na kufa alafu utazaliwa mfumo mpya wa jua ambao hatujui utakuwa na viumbe hai ama laa
 
Quran

Al-Isra' 17:49

وَقَالُوٓا۟ أَءِذَا كُنَّا عِظَٰمًا وَرُفَٰتًا أَءِنَّا لَمَبْعُوثُونَ خَلْقًا جَدِيدًا


Na walisema: Je! Tutapo kuwa mifupa na mapande yaliyo vurugika, tutafufuliwa kwa umbo jipya?


Al-Isra' 17:50

قُلْ كُونُوا۟ حِجَارَةً أَوْ حَدِيدًا



Sema: Kuweni hata mawe na chuma.

Al-Isra' 17:51

أَوْ خَلْقًا مِّمَّا يَكْبُرُ فِى صُدُورِكُمْۚ فَسَيَقُولُونَ مَن يُعِيدُنَاۖ قُلِ ٱلَّذِى فَطَرَكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍۚ فَسَيُنْغِضُونَ إِلَيْكَ رُءُوسَهُمْ وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هُوَۖ قُلْ عَسَىٰٓ أَن يَكُونَ قَرِيبًا


Au umbo lolote mnalo liona kubwa katika vifua vyenu. Watasema: Nani atakaye turudisha tena? Sema: Yule yule aliye kuumbeni mara ya kwanza! Watakutikisia vichwa vyao, na watasema: Lini hayo? Sema: A'saa yakawa karibu!

Al-Isra' 17:52

يَوْمَ يَدْعُوكُمْ فَتَسْتَجِيبُونَ بِحَمْدِهِۦ وَتَظُنُّونَ إِن لَّبِثْتُمْ إِلَّا قَلِيلًا


Siku atakapo kuiteni, na nyinyi mkamuitikia kwa kumshukuru, na mkadhani kuwa hamkukaa ila muda mdogo tu.
 

Mi naamini sio juhudi tu kuna jambo tu lipo ndio maana Asia wanaamini sana kuhusu Fate/Destiny yani haya maisha ni kama yamepangwa nahisi ndio mana kuna watu wanafanya unabii wa yajayo
Kama nimekuelew hvi❤️
 
Taifa la kiyahudi lilimuasi Mungu hivyo walilaaniwa kutokana na kuua mitume na manabii wa Mungu. Matokeo yake Mungu akawasalitisha kwa maadui zao na mbaya zaidi final prophecy inakuja kutimia soon. Wenyewe wanadhani kuwadhulumu ardhi waarabu (wapalestina) ni kheri kwao ila kiuhalisia ni moja ya makosa watakayokuja kuyajutia mno kwani huko mbeleni watakuja kufyekwa na waislam vibaya mno na ndio itakuwa mwisho wa taifa la uyahudi
 
Kuna utata hapa, hasa ukisoma Biblia ni nani hasa mrithi wa Ardhi ya mzee ya Ibrahimu (ardhi ya palestina).

Japo baadhi ya wanathiolojia wanasema hiyo vita mwishowe Israel itapigwa na hapo hapo ndipo kiama kitafika
 
Mun
Kuna utata hapa, hasa ukisoma Biblia ni nani hasa mrithi wa Ardhi ya mzee ya Ibrahimu (ardhi ya palestina).

Japo baadhi ya wanathiolojia wanasema hiyo vita mwishowe Israel itapigwa na hapo hapo ndipo kiama kitafika
Mungu ameelezea ahadi take juu ya udhalimu wa wana wa israel .

Quran 17:3-8
 
Na kwenye kitabu Cha batman the fury.. batman alisema "kila mtu atakuwa popo siku ya mimi kurudi" . 😂😂😂 Haya Sasa na mi nimeonyesha kipande Cha kitabu.
Bana hebu skia mkiwa kwenye mabishano haya mbishane kwa facts, sio kwa hekaya za waarabu ambao wanalazimisha dunia nzima kuamini. Sisi sio watoto sawa.
 
😅😅😅

Mambo haya ni magumu sana SimbaMpole123.

Weakness moja kubwa ya mambo ya Dini/imani, inabidi uamini bila kuona alafu ukishaamini ndiyo utakuja kuona.

Wakati sayansi inataka uone ndiyo uamini
 
Bana skieni..Mungu hajaumba ulimwengu wenye nyota billion 60 na sayari trillion kadhaa, ili achague kabila la wafuga mbuzi na kondoo jangwani. Hivyo wayahudi wametengeneza huyo Mungu wao ndo maana unaona sheria zake ni sawa na tamaduni zao kipindi kile. Same applies to waarabu. Sasa we kaa apo mtu mzima unafikiri Mungu kawatokea watu milimani na mapangoni na hajakutokea wewe na we unakaa na ndevu zako unakubali ndio kawachagua wao ili akuokoe wewe. Sawa endelea kuwa na akili hizi.
Kila dini inasema sisi tumechaguliwa wengine wanaenda motoni. Ndo ujue dini Ni za watu sio za Mungu.
 
Eti "Kabila la wafuga mbuzi na kondoo" 🤣🤣
 
😅😅😅

Mambo haya ni magumu sana SimbaMpole123.

Weakness moja kubwa ya mambo ya Dini/imani, inabidi uamini bila kuona alafu ukishaamini ndiyo utakuja kuona.

Wakati sayansi inataka uone ndiyo uamini
Issue sio kuona...mbona vitu vingi vya Sayansi sijawahi viona..lakini tafiti hazidanganyi. Ndo maana moja jumlisha moja ni mbili dunia nzima. Ila Kuna dini 45753378 na miungu 57863478 duniani. Ndo maana nasema Sayansi haidanganyi, Sayansi Ina make sense na Sayansi haimtishii mtu vitu vya kufikirika ili icontrol maisha yako. Ndo maana wenzetu wanaenda mwezini sisi tunajazana makanisani. Ndo maana wenzetu wanatengeneza Chanjo sisi tunaombea wagonjwa. Ndo maana wenzetu wanatengeneza magari sisi tunawachangia wachungaji. Ukielewa tofauti ya dini na Sayansi na effect zake zote mbili. Utajua we need science to socially and economically develop
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…