Naamini Mungu yupo ila nashindwa kuuelewa ukamilifu wake, labda muendelee kunifunza

Naamini Mungu yupo ila nashindwa kuuelewa ukamilifu wake, labda muendelee kunifunza

Hahhh yap, naelewa kama upo vuguvugu.

Lakini waulize wanaoamini Theories kama Evolution kwamba:-
1. Je, Kuamini kwamba zamani watu walikua na mikia... Ila kutokana na kutoitumia ilifanya mikia idhoofike na kutoweka (Use & Disuse Theory)

2. Na, kuamini kwamba Mtu alivyo leo, ndiyo hivyo alivyoumbwa,.... Na hajawahi kuwa na mkia.

Imani ipi inahitaji kujitoa akili hapo?
Kisayansi binadam bado ana mkia hata sasa 😅😅
 
Bora sisi au Bora wewe ambae unaamini kuliko na mwanga na Giza baadae dunia ikatengenezwa, baadae jua mwezi na nyota zote(ulimwengu mzima Sasa jiulize dunia ilikuwa wapi na Ina ukubwa gani kutengenezewa siku 3 na ulimwengu uliobaki siku 1), mimea kutengenezewa kabla ya jua(sijui inakuwaje bila photosynthesis), watu wawili katika bustani, mmoja katokea na udongo mwingine mbavu, Kuna matunda ya uzima wa milele na ujuzi, Kuna wanyama wote na mimea yote katika bustani moja lakini hamna kifo mpaka mwanamke atapoongea na nyoka na kuambiwa ale tunda. In short Bora niamini the gradual process of evolution kuliko kuamini hii hekaya
Hao watu wengine hata hawaelewi atheism ni nini.
 
Inategemea na ulipo, unataka kufanya nini.

You have to be selective.

Huko bongo watu wanaweza kukuua kwa sababu uko tofauti nao.
I don't think bongo wanashida na atheism. Unless iwe too public na too threatening national security. Lakini if normal hawawezi kukuua
 
Simba

Lakini mkuu tuende mbele turudi nyuma.

Hata hapo kale sana kabla hata Yesu hajazaliwa, kipindi ambacho ulimwengu ulitawaliwa na ustaraabu wa kigiriki.

Kulikuwa na wasomi wa kigiriki ambao ulimwengu bado unawaheshimu mpaka leo.

Mfano kina Socrates,kina Aristotle na kina pilato.

Hawa jamaa kuna wapo walioamini kwenye MATERIALISM (kama hii yako) na kuna wapo walioamini kwenye IDEALISM (kama kina hateeb10 ).

Walioamini kwenye IDEALISM walikuwa wanasema THE SOURCE OF ALL KNOWLEDGE IS FROM GOD (hapa ndipo dini imejikita zaidi nadhani)

Na wale walioamini kwenye MATERIALISM walisema KITU CHOCHOTE AMBACHO HUWEZI KUKIONA,KUKIGUSA,KUKIHISI,KUKIONJA BASI HICHO KITU HAKIPO NA HAKIJAWAHI KUWEPO.

Swali langu kwako, ina maana hao wasomi wakigiriki wa kale ambao waliamini kwenye IDEALISM hizo stori nako kuna mahali walizitoa ? Maana ni kale sana kabla hata ya hivi vitabu vya dini kuwepo wala yesu hajaja duniani bado
Naomba SimbaMpole123 pita hapa hujanijibu bado
 
Bora sisi au Bora wewe ambae unaamini kuliko na mwanga na Giza baadae dunia ikatengenezwa, baadae jua mwezi na nyota zote(ulimwengu mzima Sasa jiulize dunia ilikuwa wapi na Ina ukubwa gani kutengenezewa siku 3 na ulimwengu uliobaki siku 1), mimea kutengenezewa kabla ya jua(sijui inakuwaje bila photosynthesis), watu wawili katika bustani, mmoja katokea na udongo mwingine mbavu, Kuna matunda ya uzima wa milele na ujuzi, Kuna wanyama wote na mimea yote katika bustani moja lakini hamna kifo mpaka mwanamke atapoongea na nyoka na kuambiwa ale tunda. In short Bora niamini the gradual process of evolution kuliko kuamini hii hekaya
Kwa akili yako na Uwezo wako wa ufahamu,... Ndiyo maana unadhani eti haiwezekani dunia na viumbe wote kutengenezwa siku 3.

Basi Mimi nakuambia hata angetaka kuumba kila kitu kwa sekunde, Muumbaji angeweza tu.

Kama Dunia na viumbe wote tunaweza kusambaratika na kutoweka na ndani ya sekunde moja,.... Kipi kinakushangaza dunia na viumbe ulivyotaja kuumbwa ndani ya siku 3?
 
Huyo Mungu mwenyewe huwezi kuthibitisha yupo.

Katika kuamini huyo Mungu yupo umekuwa sawa na hao waamini dini.

Unarudi kule kule unakokukataa.
Mkuu sidhani kama ulinielewa hapo
 
By the way dini inaweza isiwe suala la kubwa kwangu.

Lakini ni kwamba, nikisoma nadharia zingine hasa sayansi ya AUSTRONOMY inanifanya mimi kwa mawazo yangu mwenyewe ni conclude tu kusema Mungu yupo.

Mfano : katika sayansi ya anga za juu (Austronomy) ni kwamba kila kitu kilichoko angani kinazunguka (every object in the universe is moving or is in motion).

Ni kama na maana kwamba Dunia inazunguka,Mwezi unazunguka,Sayari zote zinazunguka,Jua linazunguka,Galaxy (mkusanyiko wa nyota) zinazunguka,Black holes zina zunguka n.k

Yaani kifupi ni kwamba hakuna kitu hata kimoja ambacho kimo hewani kimesimama wima tu hakizunguki,every object is in motion.

Lakini sasa kinachonishangaza, kwenye hii tasnia ni kwamba "ulimwengu unazunguka kwa kufata kanuni maalum".

Yaani unavyoviona angani vyote vinazunguka kwa kufata system/formula ama mfumo maalum na ndiyo maana huoni vikigongana hovyo wakati ukiangalia ni kama viko shaghala paghala (bila mpangailio).

Isingekuwa hivi vitu viko kwenye mfumo maalum basi dunia yetu hii ingeshagogwa na vitu vingine vikubwa sana angani na ingeshasambaratika muda tu.

Coz kwenye anga kuna vitu vikubwa sana ambavyo ukifananisha na Dunia, Dunia itaonekana kama kipande cha kokoto tu.

Hivyo basi, universe kuwa katika mpangalio maalum na kufata kanuni , ndiyo kunanifanya nipate wazo kuwa "Lazima kutakuwa na fundi aliyedizaini hivi vitu na kuviongoza (kama remote controller).

Trust me huu ulimwengu usingekuwa na fundi maalum wa kuungoza basi vitu angani vingekuwa vinagongana kila dakika hata dunia sasahivi isingekuwepo ingeshafanywa kifusi mda.

Sasa huyo fundi ndiye nimekuja kudhani kwamba ndiyo atakuwa huyo Mungu anaesemwa kwenye vitabu vya dini.

Lakini sasa nimeenda na kwenye vitabu vya dini, sifa anazopewa nikilinganisha na matukio ya baadhi ya vitu humo humo kwenye vitabu vya dini, naona kabisa vinakosa ushirikiano/haviendani.

Nimeamua nikupe mfano mmoja tu wa AUSTRONOMY, ila ukitaka mwingine pia nitakupa
Sio kwamba vinazunguka kwa mfumo maalumu. Bali ni balance ya gravity tu ndio inakeep vitu in orbit. Na sio kweli kwamba bodies hazigongani... zinagongana sana tu and it happens alot. Angalia ile far side ya mwezi, imejaa craters izo ni bodies zinagongana. Jupiter nayo inakua bombarded with meteors sana, dunia nayo... na sindio ilioua dinosaurs?
Vitu vyote viko in motion kwasababu universe ni matokeo ya mlipuko mkubwa so universe inatanuka, chukulia bomu mfano vile debris znavokua zinasambaa..
 
😅😅😅 designer ni energy, na energy ndiyo gravity yenyewe
 
Mimi bado niko wa vugu vugu kwanza [emoji28][emoji28]

Ila tofuatì yangu na yao ni kwamba mimi naamini kuna designer wa kila kitu hapa duniani ambaye jina lake mimi bado sijamjua
Ukiamini kuna designer wa kila kitu una contradict msingi wako kwamba kilicho complex/ chenye order kinahitaji designer.

Kwa sababu hata huyo designer ana order na complexity.

Yani unasema haiwezekani hii mifumo complex iwepo bila designer, halafu unasema kuna designer aliye complex ambaye ka design kila kitu, hivyo hana designer.

Hiyo contradiction unaiona hapo?
 
Sio kwamba vinazunguka kwa mfumo maalumu. Bali ni balance ya gravity tu ndio inakeep vitu in orbit. Na sio kweli kwamba bodies hazigongani... zinagongana sana tu and it happens alot. Angalia ile far side ya mwezi, imejaa craters izo ni bodies zinagongana. Jupiter nayo inakua bombarded with meteors sana, dunia nayo... na sindio ilioua dinosaurs?
Vitu vyote viko in motion kwasababu universe ni matokeo ya mlipuko mkubwa so universe inatanuka, chukulia bomu mfano vile debris znavokua zinasambaa..
Mbona hatuoni dunia ikitoka kwenye mfumo wake au ikilosogelea sana jua ili iungue.

Kama hilo halitokei jua ndiyo mfumo maalum wenyewe ninao uzungumzia mimi
 
Back
Top Bottom