Kabla sijaanza kumjibu
Kiranga Hoja zake, nataka kwanza niwaulize swali wewe na
SimbaMpole123 .
Kuna nadharia ya uwepo wa jamii za siri Duniani kama Freemason & Illuminati.
Na jamii hizo zimejulikana sana kwenye kuu-control ulimwengu uende vile wao wanataka na pia kuwapa wanachama wao mafanikio kama utajiri n.k lakini kwa njia ya kafara za damu ya watu.
Jamii hizi zimeonekana kuwepo kote duniani mpaka hapa TANZANIA wanasema kuna jengo lao liko hapo POSTA DAR ES SAALAM kama ndiyo HQ kwa upande wa Tanzania.
Tumeshuhudia watu mbali mbali wakihusishwa na hizo imani ikiwemo marehemu Steven Kanumba, Sir Andy Chande ambae pia alifanikiwa kuwa kiongozi mkubwa tu ndani ya jamii hiyo.
Sasa mimi nime-base zaidi kwa hawa ambao walifanikiwa kutoka salama huko na wamefanikiwa kuwa hai hata sasa na wamekuja kusimulia maovu yote yaliyoko huko kama Kafara, magic power n.k
Mfano wa watu hao ni PASCHAL CASSIAN ambae pia alikuwa mshindi wa bongo star search 2009, amesema mengi sana kuhusu freemason na mpaka sasa bado anasema na ni kwa sababu pia yeye amewatumikia.
Swali langu kwenu nyie
Kiranga na
SimbaMpole123 , Je mnaamini katika uwepo wa nguvu hizo za majaabu kuwa zipo au hamwammini kabisa mnaona ni uzushi tu wa kinadharia