Naamini Mungu yupo ila nashindwa kuuelewa ukamilifu wake, labda muendelee kunifunza

Kwa hiyo na we unaamini majini yapo. Na yameumbwa kwa moto. Sasa hata story yako inaonyesha Mungu mliyemtunga Hana nia na sisi. Anakubaliana kabisa na shetani eti anamwachia apoteze wengi wachache waokoke. Mi sielewi mnafurahia Nini. Hivi Leo ukahukumiwa kuunguzwa milele au mama ako au mtoto wako, we utakuwa na furaha. Shida ya dini zinapenda kutenga watu eti sisi tutaokoka nyie mtaungua, yaani mnafurahia watu kuungua mnajiaminisha dini yenu ya kweli na mnafanya vitu vya ajabu kisa mwarabu kawaambia, hio sio Imani hii Ni kutokuwa na maadili na kufikiri. Haya Leo hii hizo hekaya za waarabu za uongo na siku ya kufa ukamkuta Krishna, utajiteteaje, utasema sikujua au...hebu fikirieni nje ya box lenu bac, Kuna dunia nje ya Islam
 
Bravo bravo bravo
 
Jamani si nimekuelezea gods walikuwepo tokea binadamu walikuwa hunters na gatherers, mi sijazungumzia vitabu Mimi
 
Ila hatuambiani nyoka waliongea na mwezi ulipasuka na kurudi bana
 
Hamna nguvu ya ajabu, no ghosts. No kafara...no magic ..Kama umeskia ni Imani zake tu huyo na yaliyomo akilini, mtu kuuliwa it's natural na wanaweza kusema ni kafara. Ila there's no such thing is dark power sijui kucontrol dunia iende. Bac waambie wacontrol Vita ya Ukraine iishe Bei zishuke si wamarekani ndo wanamashetani au wazungu
 
Mambo ya lugha makabila na rangi si inaeleweka kwamba ni migration au Hujui historia. Kingine mambo ya dunia kuwa maji kabla ya binadamu na story ya Noah na zoo la wanyama kwenye safina zinahusianaje. Tatu hamna mtu kaletwa na kitu tumetokana na mazingira, Kama hivyo from amino acids which are the building blocks of life, to single celled organisms, to multicellular organisms.. miaka million iliyopita. Ila that's what science says na Ina evidence nyingi kuliko story yenu ya Adam na Hawa katika bustani na nyoka anayeongea.
 
Na mbaya zaidi kinachanganya ni kuwa hata majini/mashetani ambayo watu wanaamini yalikuwepo kabla na yenye ufahamu Yanaamini na kujua kabisa kuwa kuna uwepo wa Mungu.
Mungu Yupo! Ila ukisema kuutafuta ukamilifu wake na udhaifu huuwezi kuupata maana hekima ya Mungu ni haina kipimo..it is beyond human scope.
 
Majini. They don't exist.
 
Man u r a genius
 
Umemueleza vizuri sana, ila, kwa mtu ambaye amechagua mwenyewe kutoelewa, kuelewa ni vigumu sana.

Na hata akielewa ataweka upinzani wa "cognitive dissonance" tu.
 
πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜… bora wewe umesema kwa uwazi kuwa haipo, ila kiranga alikuwa amenichanganya kidogo kuonesha hata hiyo nguvu hajawahi kuiskia.

Mkuu kwa sababu wewe umesema wazi kuwa hiyo nguvu haipo, mimi sitakuuliza maswali mengi tena kuhusu hilo ila ningeuliza kaswali kafupi tu kuwa : Unawaelezea wale wanaoonekana kwenye media na kusema kuwa wamepitia hizo imani, mfani kina PASCHAL CASSIAN na ANDY CHANDE,

Je ni vichaa ? Waongo ambao wamekuja kutupotosha na simulizi zao ?

Ani wewe unaweza ukawaelezea kwa namna gani watu kama hao ?


NB : Vita ya ukraine na Urusi wapo wanaoamini imeletwa na hao (illuminati), na siyo hivyo tu hata world wars 1&2 wapo wanaoamini vililetwa na wale jamaa japo mimi siamini katika wazo hilo.
 
By the way supernatural power mimi huwa naiskia tu kuwepo kinadharia na mara nyingi huadhaniwa kwamba yenyewe hutenda pale binadamu anapokuwa ameshindwa
 
By the way supernatural power mimi huwa naiskia tu kuwepo kinadharia na mara nyingi huadhaniwa kwamba yenyewe hutenda pale binadamu anapokuwa ameshindwa
Kwa hiyo mtu akishindwa kuyavuta maji yashuke mlima, halafu gravity ikaweza, hiyo gravity inakuwa supernatural power?
 
Kiranga nna swali kwako : umejitambulisha vizuri kuwa wewe ni Atheist, na kuna mtu mmoja maarufu sana duniani anaitwa Elon Musk naye ana imani kama yako.

Lakini Elon Musk ni mwanasayansi pia naweza nikasema (japo ni injinia) ila yeye anaamini katika uwepo wa ALIENS.

Je, vipi wewe kama Atheist unaamini katika uwepo wa viumbe hao pia ?
 
Skia..mfano we umelala ukaamka ukaona malaika chumbani kwako kakutokea na kakuongelesha. Je, utaamini kwamba sheria za ulimwengu wa asili zimepishana kwa ajili yako au wewe macho yako na ubongo wako umekosea kutafsiri Hali halisi. Watu wanaona vitu ndio..Kama vile Fatima watu 3000 waliona jua linachezacheza..Ila jua lilicheza, au akili zao ndo ziliwachezea hio michezo. Tafuta real video ya anything supernatural, halafu ndo ukubali na iwe true coz vitu vya hivyo vingetangazwa taarifa za habari main, hizi story zipo hata bongo lakini hazitangazwi kwa sababu zipo kwenye akili tu.
 
Siamini katika kuamini, nataka kujua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…