Naamini Mungu yupo ila nashindwa kuuelewa ukamilifu wake, labda muendelee kunifunza

Naamini Mungu yupo ila nashindwa kuuelewa ukamilifu wake, labda muendelee kunifunza

Mariam alimzaa Yesu bila kuguswa/kufanya tendo na Mwanaume.

Hiyo mistranslation ipo wapi hapo?
Bro story ya virgin birth ipo kwenye religion nyingi kabla ya Christianity. Hata Krishna kazaliwa kwa bikira. Story ain't new imeibiwa. Huamini acha sio lazma.
 
Tokea uzaliwe hujawahi ona Polar bears so hawapo. Skia tubishane kwa hoja sio hisia sawa. There is homosexuality in animals umeona wanyama asilimia 1% duniani huna good sample size to claim ur results. Acha kutetea point iliyofeli, na bado hujajibu so tubakane kuuwana na kuibiana Kama wanyama au? Maana ya kuwa binadamu ni Nini Kama unataka uwe Kama mnyama. And why ushoga tu do animals do blowjobs mbona hamkatazi na hio.
In short hakuna Mnyama Shoga.. labda wewe na wenzako muendelee kudanganyana huko Google.


Binadamu amepewa akili nyingi mno ukilinganisha na Wanyama, lakini Wanyama hawafanyi huo ujinga.... So, mtu anaesupport ushoga anakua amejishusha thamani na kuzidiwa utambuzi mpaka na Nguruwe.
 
We ungekuwa Mungu unayejali uumbaji wako ungempa ujumbe lijitu liarabu afu aeneze ujumbe kwa vitishio dunia nzima? This shows ni info yake...kila mtu anajikuta anakutana na Mungu sijui malaika na anasema sheria zake ndo za Mungu na mijitu mnakubali coz mnaogopa kifo. In short all religions are made up.
Maneno unayotumia sio ya Staha, bali yanaonyesha tu chuki neno Kama "Liarabu" "Lijitu"...... Si Maneno mazuri kutoka kwa mtu mwenye hekima🤝🏼


Kama humuamini huyo Muarabu sio mbaya, wewe endelea kumuamini Charles Darwin atakutosha.
 
Bro story ya virgin birth ipo kwenye religion nyingi kabla ya Christianity. Hata Krishna kazaliwa kwa bikira. Story ain't new imeibiwa. Huamini acha sio lazma.
So, kwa mtazamo wako Hiyo story ya Yesu kuzaliwa na Bikra Mariam ni uongo?
 
Maneno unayotumia sio ya Staha, bali yanaonyesha tu chuki neno Kama "Liarabu" "Lijitu"...... Si Maneno mazuri kutoka kwa mtu mwenye hekima🤝🏼


Kama humuamini huyo Muarabu sio mbaya, wewe endelea kumuamini Charles Darwin atakutosha.
Charles Darwin hajachinja mtu na kutishia moto. Sayansi hailazimishi, ujinga unauchagua wewe
 
In short hakuna Mnyama Shoga.. labda wewe na wenzako muendelee kudanganyana huko Google.


Binadamu amepewa akili nyingi mno ukilinganisha na Wanyama, lakini Wanyama hawafanyi huo ujinga.... So, mtu anaesupport ushoga anakua amejishusha thamani na kuzidiwa utambuzi mpaka na Nguruwe.
Screenshot_20230510-205549.png
 
In short hakuna Mnyama Shoga.. labda wewe na wenzako muendelee kudanganyana huko Google.


Binadamu amepewa akili nyingi mno ukilinganisha na Wanyama, lakini Wanyama hawafanyi huo ujinga.... So, mtu anaesupport ushoga anakua amejishusha thamani na kuzidiwa utambuzi mpaka na Nguruwe.
Wewe acha ubishi point ya nature imebugi Kama unataka tule watoto wetu Kama mbwa coz ni wanyama, we Baki na unyama wako sisi ni binadamu.
 
Mkuu napendekeza usome kitabu HOW DID LIFE GET HERE BY CREATION OR EVOLUTION.
Humo hata hayo ya shetani alitoka wapi yanajibiwa .
Utakipata free kwenye online library WOL.JW.ORG nenda kwenye section ya vitabu.
Mkuu nimeenda huko nimeshindwa kukipata hicho kitabu. Unaweza kupakia hapa tafadhali?
 
Wakuu poleni kwa upambanaji.

Binafsi mimi kuna mda huwa nikitulizaga kichwa changu huwa naanza kujiuliza maswali mengi sana kuhusu mimi (binadamu) na ulimwengu kiujumla (Universe).

Maswali kama sisi (binadamu) ni kina nani,tumetoka wapi asili yetu, kwanini tupo (dhumuni la kuishi), mwisho wetu ama hatima yetu ni nini, Ulimwengu wa vitu je kama sayari, nyota, galaxies zimekuwepo vipi na nini hasa mwisho wake.

Hapo juu ni baadhi tu ya maswali ambayo huwa naiuliza sana akili yangu ikiwaga katika hali ya utulivu.

Lakini cha kusikitisha ni kwamba, katika maswali yote hayo ambayo huwa najiuliza, sijawahi kupata jibu la uhakika kuniridhisha kuhusu hayo maswali yangu.

Nimekuwa nikifanya bidii kubwa sana kupata majibu ya maswali yangu kupitia usomaji wa majarida au vitabu vihusuvyo historia,sayansi, dini na Falsafa lakini kote bado sijapata majibu ya kuniridhisha tofauti na kuambulia majibu ya kinadharia tu ambayo yana strength kiasi chake lakini pia yana weakness sehemu nyingi tu.

Na nikiri wazi tu kuwa katika usomaji wangu wa nadharia hizo zote (historia, sayansi, dini, falsafa) sehemu ambayo nimeanza kuiamini kunipa majibu ya maswali yangu ni kwenye DINI.

Nikiwa na maana nimeanza kuamini kwamba uwepo na sisi tuliohai na visivyo hai hapa ulimwenguni ni matokea ya Uumbaji ya nguvu kubwa sana inayoitwa MUNGU/ALLAH kama ambavyo dini nyingi zinaelezea nguvu hiyo.

Na leo maswali yangu yanajikita huko kwenye hiyo nguvu (Mungu) maana nimeanza kuiamini lakini pia kila nisomapo BIBLIA (mimi mkristo) inanipa maswali chungu nzima.

Sasa leo swali langu limejikita kwenye UKAMILIFU wa MUNGU.

Naombeni wasomaji mnielewe kuwa sina maana ya kukufuru (maana mara nyingi niulizapo maswali kuhusu MUNGU huwa naambiwa nakufuru) bali mimi nataka kujifunza zaidi kumuhusu huyu Mungu.

Dini nyingi (hasa Ukristo na uislamu) zimekuwa zikimwelezea Mungu kuwa ni Mkamilifu sana,mwenye nguvu nyingi sana, uwezo na akili zake hazichunguziki, hashindwi na chochote n.k.

Je hilo lina ukweli ? kupitia Biblia mimi nimeanza kudhani kwamba huenda kweli Mungu ana nguvu nyingi sana ila siyo zote, ana uwezo mkubwa sana ila siyo uwezo wote,ana maarifa mengi sana ila siyo maarifa yote, ana ukamilifu mwingi sana ila siyo ukamilifu wote n.k

Nasema haya ni kutokana na maswali yafuatayo :

1. Kama Mungu ana ukamilifu wote, kwanini sasa alimuumba malaika (Lucifer/shetani) alafu badae akaja kumuasi?
Kama Shetani/Lucifer aliasi maana yake ni kwamba Mungu alimuumba huyu kiumbe akiwa na madhaifu kadhaa na ndiyo maana alishindwa kuitii amri/mamlaka ya muumbaji wake.

Kama Mungu angelikuwa na ukamilifu wote, basi malaika wote wangelikuwa wameumbwa katika namna ya utii pekee, uasi usingetokea na huo uasi unadhihirisha kwamba Mungu aliwaumba hawa malaika wakiwa na udhaifu flani, hawakuwa na uimara wote.

2. Uumbaji wa Eva (Hawa) unaonesha kulikuwa na madhaifu pia.
Katika Biblia takatifu kwenye kitabu cha mwanzo, kuna mistari inaeleza kuwa "Mungu alimpa usingizi mzito Adam, alafu akabandua sehemu ya ubavu wake na kumfanya/kumuumba mwanamke (Hawa/Eva)".

Alafu Mungu akamwambia Adam kuwa huyu mwanamke atakuwa msaidizi wako

Lakini ni huyo huyo mwanamke ambae shetani (kwenye umbo la nyoka) alienda kumdanganya akachukua matunda ya mti walioambiwa asile yeye akala na akampelekea na mumewe (Adam) pia akala.

Lakini Mungu alivyomuuliza Adam kwanini umekula matunda ya mti ambao nilikwambia usile, Adam alijibu kuwa "Ni huyo mwanamke uliyenipa ndiye aliyeniletea nikala".

Tukio hili linadhihirisha kuwa Mungu alimpa Adam msaidizi (Hawa) ambae ni dhaifu sana na ndiyo maana alisababisha dhambi ikaenda hadi kwa Adam.

Na huenda kama Mungu angelikuwa amempa Adam msaidizi imara asiye na madhaifu basi ile dhambi ya kula tunda ingeepukika.

Uko wapi sasa ukamilifu wote wa Mungu ikiwa aliweza kuwaumba malaika dhaifu (ambao walikuja kumuasi) na pia bado akampa Adam msaidizi dhaifu kabisa ambaye alisababisha dhambi imwendee hadi Adam?

Kwa leo naombeni comment zenu zinifunze kuhusu hilo tu (La ukamilifu wa Mungu) alafu mengine nitauliza siku nyingine, na mengine nitakuwa nauliza humo humo kwenye comments zenu.

NB: Naamini Mungu yupo, kutokana na baadhi ya vitu ninavyoviona ulimwenguni (hasa uumbaji/creation) ambapo kuna baadhi ya vitu hasa sayansi inakosa majibu ya kuridhisha, ila shida yangu kubwa ni sifa za Mungu ambazo anapewa na wanadamu naona kama zinashindwa kujidhihirisha kwenye baadhi ya mambo.

Karibuni mnifunze.

Mungu yupo kweli,shida ni mpango wake sio huu ambao waanzilishi wa juz Dini wanatifundisha kwa interest zao tuamini na Kuishi Walivyotaka wao,lkn kusudi la Mungu ilikua kumuumba mwanadamu na kumpa kila kitu dunian avitawale na yy Kama muumbaji kutazama viumbe alivyoviumba namna vinaishi kufa na kuja vingine yani hivyo Kama mzunguko wa Sayari zote zinavyofanya na wan Adamu na viumbe vingine vitaishi hivyo ,lkn waliibuka watu wengine Walianza kumsemea Mungu maneno yao juu ya mpango wake kwa wanadamu,pia Mungu hakutaka kumuumba mwanadamu ktk ukamilifu wote ili Kurw na balance na dunia iendelee Kuwepo,uzur wa hao watu walioanzisha dini ni Walitaka huyu mwanadamu Asiwe huru kuamua kila kitu Bali amatengeneza ktk sheria na maandiko mengi ,ila Mungu yy Alitaka tuishi tuondoke waje wengine dunia iwe hivyo,na apo hakuna hukumu hata ya kumuangamiza mwanadamu ,Hzo zote ni propaganda Haiwezekan Mungu Ajue ameumba mtu sio mkamilifu Alfu kwa kutokua mkalifu aje amuhukumu hell no hatofanya hyivyo ,yote yaliyotokea uko nyuma ni madhara kama yanayotokea sasa tu magonjywa ,Vits kuuwana ni kitambo tangu mwanzo kaini alimuua kaka yake abili ,
 
Hamna evidence ya kuwa alifufua mtu...Kama unayo nipe
Evidence hiyo sina, the same kwako ambae baadhi ya vitu huna evidence navyo ila umeamua kuamini.

So it's both teams to score... Wazee wa kubet wanaita GG🙌🏼
 
Kwanza nikuweke sawa kuwa, mimi simfikirii Mungu kuwa sawa na binadamu.

Nimesema kuwa Mungu ana uwezo mwingi,akili nyingi,maarifa.mengi,ukamilifu mwingi ila kati vyote hivyo anavyo katika hali ya wingi na siyo katika hali ya ukamilifu wote (100%) ama ya kutokuwa na kikomo

Nasema hayo sija- Qoute kokote ila nimesema ni kutokana na jinsi anavyojipambanua yeye ndani ya vitabu vyake vitakatifu (rejea mifano miwili ya maswali niliyatolea mfano kwenye uzi).

Mungu angelikuwa na sifa zote hizo za ukamilifu basi hizo kasoro zilizojitokeza (zikapelekea dhambi) zingeweza kuepukika iwapo uumbaji huo angeufanya katika ukamilifu.

Zingatia kwamba, sijaribu kumkosoa/kumsahihisha Mungu katika uumbaji wake bali nataka tu kujua kwanini itokee hivo wakati yeye ana ukamilifu wote na uwezo wake hauna kikomo ?

Labda mnambie kama hizo kasoro aliziumba kwa maksudi kwa sababu anazozijua mwenyewe hapo nitawaelewa ila mkiendelea kunambia aliumba katika ukamilifu wote, hapo nitaendelea kuwauliza maswali yasiyoisha.

Mfano wako wa mpira kuwa na wachezaji 22 na kushindana kuingiza goli kwa miguuu.

Huu mfano kumbuka ni wa kanuni (sheria za kibinadamu ambazo tumeziweka wenyewe) na mara kwa mara hufanyiwa marekebisho kulingana za uhitaji.

Mfano sasahivi wanafikiria kupunguza dakika za kucheza ziwe 40 kwa kila kipindi badala ya 45.

Kwa hiyo hizi ni kanuni ambazo tumweziweka na tunazibadilisha muda wowote tutakaotaka
Kuna kitu kinaitwa Utashi (Unaweza kuangalia maana ya utashi hapa: Utashi - Wikipedia, kamusi elezo huru).

Mungu ameumba binadamu na viumbe vingine vikiwa na utashi ndani yake. Angeweza kutuumba bila kuwa na utashi kitu ni ambacho kingesababisha kumuita Mungu asiye na haki. Ametupa Utashi ili tuweze kumuita Mungu ni mwenye Haki ikiwa ni moja ya sifa kati ya sifa nyingi ikiwemo Ukamilifu.
Sasa hapo kwenye utashi ndipo tunapoona viumbe ambao tumeumbwa na Mungu tunaweza kuwa na uchaguzi katika kila jambo.

Quantum phisics inathibitisha hilo ya kuwa katika kila kipindi, muda au wakati viumbe tukiwemo binadamu tuna uwezo wa kuamua jambo fulani huku kukiwa na machaguzi mawili, aidha aahe au afanye.

Sasa kutokana na utashi huo sisi wenyewe viumbe wa Mungu tumejikuta tukichagua vilivyosahihi na vilivyosahihi kulingana na namna tunavyodhani wenyewe. Ndio maana kuna ambao wanamkana Mungu na kuna ambao wanamtukuza Mungu.

Lakini pamoja na Mungu kutupa uhuru huo wa kuamua (Utashi), kwa kuwa Mungu ni mwenye Haki ametupa uwezo wa kutambua jambo zuri na baya hasa kwetu binadamu ili hata itakapofika siku ya hukumu ifanyike katika Haki.

Utashi ndio unaotupa matokeo ambayo mtoa mada yanampa maswali, hayo ni maono yangu.
 
Mkuu nimeenda huko nimeshindwa kukipata hicho kitabu. Unaweza kupakia hapa tafadhali?
Mkuu hichi kitabu unalisoma online, simu yangu ndogo siwezi kukipakua...

Sasa ingia google andika
HOW DID LIFE GET HERE BY CREATION OR EVOLUTION mwisho weka wol.jw.org
utapata sema kipo kwa kingereza.
 
Back
Top Bottom