Naamini Mungu yupo ila nashindwa kuuelewa ukamilifu wake, labda muendelee kunifunza

Naamini Mungu yupo ila nashindwa kuuelewa ukamilifu wake, labda muendelee kunifunza

By the way dini inaweza isiwe suala la kubwa kwangu.

Lakini ni kwamba, nikisoma nadharia zingine hasa sayansi ya AUSTRONOMY inanifanya mimi kwa mawazo yangu mwenyewe ni conclude tu kusema Mungu yupo.

Mfano : katika sayansi ya anga za juu (Austronomy) ni kwamba kila kitu kilichoko angani kinazunguka (every object in the universe is moving or is in motion).

Ni kama na maana kwamba Dunia inazunguka,Mwezi unazunguka,Sayari zote zinazunguka,Jua linazunguka,Galaxy (mkusanyiko wa nyota) zinazunguka,Black holes zina zunguka n.k

Yaani kifupi ni kwamba hakuna kitu hata kimoja ambacho kimo hewani kimesimama wima tu hakizunguki,every object is in motion.

Lakini sasa kinachonishangaza, kwenye hii tasnia ni kwamba "ulimwengu unazunguka kwa kufata kanuni maalum".

Yaani unavyoviona angani vyote vinazunguka kwa kufata system/formula ama mfumo maalum na ndiyo maana huoni vikigongana hovyo wakati ukiangalia ni kama viko shaghala paghala (bila mpangailio).

Isingekuwa hivi vitu viko kwenye mfumo maalum basi dunia yetu hii ingeshagogwa na vitu vingine vikubwa sana angani na ingeshasambaratika muda tu.

Coz kwenye anga kuna vitu vikubwa sana ambavyo ukifananisha na Dunia, Dunia itaonekana kama kipande cha kokoto tu.

Hivyo basi, universe kuwa katika mpangalio maalum na kufata kanuni , ndiyo kunanifanya nipate wazo kuwa "Lazima kutakuwa na fundi aliyedizaini hivi vitu na kuviongoza (kama remote controller).

Trust me huu ulimwengu usingekuwa na fundi maalum wa kuungoza basi vitu angani vingekuwa vinagongana kila dakika hata dunia sasahivi isingekuwepo ingeshafanywa kifusi mda.

Sasa huyo fundi ndiye nimekuja kudhani kwamba ndiyo atakuwa huyo Mungu anaesemwa kwenye vitabu vya dini.

Lakini sasa nimeenda na kwenye vitabu vya dini, sifa anazopewa nikilinganisha na matukio ya baadhi ya vitu humo humo kwenye vitabu vya dini, naona kabisa vinakosa ushirikiano/haviendani.

Nimeamua nikupe mfano mmoja tu wa AUSTRONOMY, ila ukitaka mwingine pia nitakupa
Uwepo wa mambo wa ya ajabu ambayo yanakosa maelezo ndio chanzo cha mwanadamu kufikiri uwepo wa nguvu kubwa kuliko yeye ulipoanza.

Na naona kabisa kwenye kutafuta ama kutaka ushirikiano na nguvu hio kubwa kila mmoja alipata experience yake kama nilivosema awali.

Sasa hapo utaona kutokua na uwezo wa kueleza matukio ya aina fulani watu hao wakakabidhisha uwezo huo kwa kitu kingine Tunaita MuNGu na wakaanza kuhalalisha mambo mengine humo ndani, ambayo hayana uhusiano na uwezo wa mungu kuumba na kufanya mambo makubwa.

Mfano; unaweza kuta kundi fulani la watu wanawachukia watu fulani kwa sababu zai binafsi tu ili waeneze hio chuki kwa watu wengine watasema, watu wenye tabia fulani ni chukizi kwa mungu muumba mbingu. Sasa chuki yako na uumbaji wa mungu wapi na wapi.

Kutoka 20:7 Inasema usilitaje jina la bwana mungu wako bure.
Ukisoma biblia tafsiri ya KJV inasema
"You shall not take the name of the LORD your GOD in vain"

Biblia tafsiri ya J.B ROTHERHAM
"Thou shall not utter the name of the yahweh your GOD for falsehood"
Akimaanisha usitumie jina la mungu kuhalalisha mambo yako ya kipimbavu.

Ukiangalia history biblia ni mkusanyiko wa vitabu mbalimbali ambavyo watu fulani waliona mafundisho yake yanafanana fanana ama lengo la waandishi hao tofauti tofauti ni kama lilikua moja.

Ndio maana unakuta kuna matoleo mbalimbali ya biblia na yote waandaaji watakuambia waliongozwa na roho mtakatifu ili kukusanya vitabu hivyo.

Na je kama roho ni mmoja mbona awaongoze makusanyo yalio tofauti?, mbona waprotestanti wawe na vitabu kiasi fulani kwa biblia zao, mbona mayaudi wa kanisa la orthodox maybe wakubali mafundisho ya vitabu mfano vitabu vya enoch lakini waprotestant waseme vitabu hivyo havijavuviwa na roho mtakatifu, ni roho mtakatifu gani aliwavuvia waorthodox.

Ukiangalia fact kwa umakini hapo utakuta kuna interest za watu kwenye kuupata ukweli ndio maana ukweli halisi huwezi upata kwenye hivyo vitabu zaidi ya kuongeza maarifa juu ya mambo fulani tu.

Hata kristo alitoa onyo juu ya maandiko
Yohana 5:39-40....
Maandiko pekee hayatoshi bali kumtazama yeye kuutazama ukweli, ukweli ndio utatuweka huru. Na tukubaliane labda tungekua na toleo la kwanza la biblia huenda tungefahamu uhalisia wa mambo yalivyo lakini kwa hii tuliyonayo sasa imechezewa sana, kuna interest ya makundi ya watu fulani sana na wamehalalisha mambo kwa mgongo wa MUNGU.

Nimeegamia upande wa biblia sina ufahamu sana kwenye quran. Tuna mengi ya kujifunza sana mkuu.

Na kuegamia sana vitabu vya dini kujifunza ukweli ni kuishia kua mfia dini.
 
We subiri tu aanguke, mwenzako anaachana na Imani potofu na kujiendeleza kisayansi na kitechnolojia na waafrika tukibaki na huu uwoga wetu wa kifikra tutaishia tu kuwekewa satellite na kutengenezewa chanjo.
Msilaumu wengine kwa matokeo yenu. Kama dini ililetwa kwanini hamkuwa matajiri miaka yote wala hamkuwa na technology kubwa kuwazidi wenzenu. Mmekuja kudanganywa na sukari na sabuni kweli nyinyi nd mngetoboa hata kujua kuna kujenga nyumba kweli au barabara au madaraja au hata kujua kusoma na kuandika tu. Vyoo vyenyewe mmefundishwa kutumia mgeweza kutengeneza fedha au baishara au ndege spaceships kwelii? Ichukieni dini kwa mambo mengine ila sio kwenye failures zenu. Kwanza dini gani inakataza watu kuendelea binafsi tuanzie hapo lete na vifungu.
 
We subiri tu aanguke, mwenzako anaachana na Imani potofu na kujiendeleza kisayansi na kitechnolojia na waafrika tukibaki na huu uwoga wetu wa kifikra tutaishia tu kuwekewa satellite na kutengenezewa chanjo.
Wewe mwenyewe unaepinga dini wakati huu si umeshajikomboa kifikra em lete ulichofanya kina mchango gani kweny jamii ya watu milion 60
 
Hii inaonyesha hamna tofauti ya kuomba na kutokuomba kwa sababu kitu kinaweza tokea au kisitokee Ni juhudi tu ndo zinaleta maendeleo. Ndo maana wazungu wanajenga viwanda wakati waafrica wanajenga makanisa.
Je wazungu hawana makanisa? Hayo makanisa ya africa mangap yamejengwa na wazungu? Je nyinyi ambao hamuhamini dini tuonesheni viwanda vyenu. Waafrica tunafeli mambo mengine ila tunatafuta kichaka cha kujifichia mara siasa mara dini na tusipoacha kulaumu watu au dini tutakaa hivi hivi miaka yote.
 
Mkuu hoja inapaswa kusikilizwa na kila mwenye mwili (yaani binadamu).

Nimekuelewa zaidi ulivyosema kuwa "kaumbwa na madhaifu alafu kapewa nafasi ya msamaha akikosea".

Ni hoja nzuri na inayoeleweka.

Lakini na kuja kwa huyu wa upande roho (Yaani shetani), kama shetani ambayo ilikuwa ni roho na bado ilimwasi Mungu, maana yake ni kwamba huyo shetani nae aliumbwa na madhaifu kama tu binadamu.

Swali langu kwako, kwanini Binadamu pekee ndiye apewe nafasi ya kutubu dhambi na kusamehewa alafu shetani yeye anywimwe hiyo fursa ya kuomba msamaha wakati wote wawili (Adam na shetani) waliumbwa wakiwa na madhaifu yaliyopelekea kuasi ?
Shetani alishapewa nafasi bro ila imeshapita hyo nafasi yake maan ukisoma bible shetani alikuwa anaenda mbinguni na kuna malaika ambao aliumbwa pamoja nao na alikuwa kiongozi wao walikuwa wanaona anaonewa mpaka pale alipofanya attempt ya kumuua Masihi nd mbinguni vikapigwa vinubi malaika wote wakashuhudia kuwa shetani ana hatia na akanyang'anywa mamlaka zote za duniani na mbinguni so kafungwa na sasa ni zamu yetu sisi.
 
KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU 0


112_1.gif

1. Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee. 1


112_2.gif

2. Mwenyezi Mungu Mkusudiwa. 2


112_3.gif

3. Hakuzaa wala hakuzaliwa 3


112_4.gif

4. Wala hana anaye fanana naye hata mmoja. 4
 
Duuh...mkuu kumjua Mungu kuna changamoto sana.

Hii ni kwa sababu hadithi nyingi za vitabu vitakatifu hazishabiliani kwa kiasi kikubwa(yaani kwenda sambamba).

Mfano : Biblia inamsema shetani kuwa alikuwa miongoni mwa malaika waliokuwa wanamwabudu Mungu mbunguni, lakini wewe unasema kwa mujibu Qur'an shetani alikuwa Jini na siyo malaika.

Kwa mujibu wa Biblia hakuna mahali panaelezea kuwa shetani aliomba msamaha bali inainesha tu kuwa yeye alikosea mara moja na kuhukumiwa pale pale wala hakuwa nafasi ya kujutia makosa, lakini wewe unasema kwa mujibu wa Qur'an shetani hakunyimwa fursa ya kutubu bali aliendelea kuwa na kiburi.

Mpaka hapo unaweza kuona namna gani vitabu vyetu vya dini vinatuambia stori tofauti kana kwamba kuna zaidi ya Mungu mmoja sijui ?

Sasa mimi nikuulize tena maswali haya mawili yafuatayo :

1.Kama shetani alikuwa akiishi Mbinguni na alikuwa akimwabudu Mungu kabla ya kuasi,Je ina maana tuseme makao ya majini huwa ni mbinguni siyo duniani na wao pia wamwchangamana na malaika wapo huko Mbinguni kumwabudu Mungu ?


2.Je, shetani akiamua hivi sasa aache kiburi na kurudi kwa Mungu kumwomba msamaha,inawezekana akasamehewa na jehanam kufutwa ?
Wewe tu hujasoma vizuri bible mkuu. Shetani alipewa nafasi kabla ya kifo cha Yesu ila baada ya pale nafasi yake ikafungwa milele na Yesu nd aliemnyang'anya shetani funguo za mamlaka zote na nafasi yake haipo tena. Kabla ya Yesu binadamu tulikuwa sawa na shetani na ndo maan kumjua Mungu kulikuwa hadi kuna kuuwawa lakini kwa sasa neema ilifunguliwa so kuasi ni uamuzi wetu tu ila Mungu katupandisha juu sawa nae tena sasa ni sisi hapo.
 
Any way acha iwe mwenye bidhaa zake ndiyo mwenye maamuzi ya mwisho.

Lakini Je, vipi kuhusu sisi kumjua yeye.
Tunamjua yeye kupitia vitabu vyake vya dini (mfano Biblia na Qur'an).

Swali ni Je, kwanini sasa vitabu vya dini vituambie stori tofauti kwenye kitu kile kile kimoja ?

It means kuna kitabu kitakuwa kimepotosha ?
Kuna stori tofauti kutokana na uasi shetani kuvuruga mambo ila sasa dini nzuri ni ile yenye matokeo chanya kwa wanadamu. Kukataza dhambi kama vile uzinzi na uasherati uuaji uongo kutokuheshimu wazazi kutamani mali za wengine( haya nd mambo muhimu ya kuangalia kwenye matokeo ya dini zilizopo)
 
Hivyo vitabu mnavyosoma wajanja wenu akina Paulo wamevichakachua Kwa makusudi Ili kukupotezeni msifuate dini ya Mungu ila mfuate dini yao

Hi yapa the same story Mungu alimuhadithia nabii Musa baadae akaja kumuhadithia mtume Muhammad kuhusu wale malaika walioenda Kwa nabii Ibrahim kumbashiria mtoto Isihaka

Mwanzo 18:2
Akainua macho yake akaona, na tazama, watu watatu wamesimama mbele yake. Naye alipowaona alipiga mbio kuwalaki kutoka mlangoni pa hema, akainama mpaka nchi,
Mwanzo 18:3
akasema, Bwana wangu, kama nimeona fadhili machoni pako nakuomba usinipite sasa mimi mtumwa wako.
Mwanzo 18:4
Na yaletwe basi maji kidogo mkanawe miguu, mkapumzike chini ya mti huu.
Mwanzo 18:5
Nami nitaleta chakula kidogo, mkaburudishe moyo, baadaye mwendelee, iwapo mmemjia mtumwa wenu. Wakasema, Haya, fanya kama ulivyosema.
Mwanzo 18:6
Basi Ibrahimu akaenda hima hemani kwa Sara, akasema, Himiza vipimo vitatu vya unga safi, uukande, ufanye mikate.
Mwanzo 18:7
Ibrahimu akapiga mbio kwenda kundini, akaleta ndama wa ng'ombe aliye laini, mzuri, akampa mtumishi, naye akahimiza kuiandaa.
Mwanzo 18:8
Akatwaa siagi na maziwa, na ndama aliyoiandaa, akawaandikia mbele yao, akasimama karibu nao chini ya mti, nao wakala.
Mwanzo 18:9
Wakamwambia, Yu wapi Sara mkeo? Akasema, Yumo hemani.
Mwanzo 18:10
Akamwambia, Hakika nitakurudia wakati huu huu mwakani, na tazama, Sara mkeo atapata mwana wa kiume. Sara akasikia mlangoni pa hema iliyokuwapo nyuma yake.



Quran 51:24
Je! Imekufikia hadithi ya wageni wa Ibrahim wanao hishimiwa?

25
Walipo ingia kwake wakasema: Salama! Na yeye akasema: Salama! Nyinyi ni watu nisio kujueni.

26
Akenda kwa ahali yake na akaja na ndama aliye nona.

27
Akawakaribisha, akasema: Mbona hamli?

28
Akahisi kuwaogopa katika nafsi yake. Wakasema: Usiwe na khofu, nao wakambashiria kupata kijana mwenye ilimu.

29
Ndipo mkewe akawaelekea, na huku anasema na akijipiga usoni kwa mastaajabu, na kusema: Mimi ni kikongwe na tasa!

30
Wakasema: Ndivyo vivyo hivyo alivyo sema Mola wako Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye hikima na Mwenye kujua.


Bibilia inasema wale wageni Ibrahim alipowaandalia chakula walikula

Quran inasema walipoandaliwa chakula hawajakula na hapo ndipo Ibrahim alipojua kuwa wale ni malaika

Ukweli ni kwamba Malaika hawali chakula so hiyo story katika bibilia imechakachuliwa
Kwenye bible Yesu alikula malaika alipigana na Yakobo sasa unashangaa nini hao malaika kula? Kwenye bible watoto wa malaika waliozaliwa kwa wake wa duniani walikuwa walevi na walafi so hyo kwann ikushangaze mkuu?
 
Hivi umeelewa nachomaanisha. Chakula kikiwa kibaya au kina makosa analaumiwa mpishi au chakula.
Kwakuwa wanaomlaumu mpishi hawajui siri labda mchele ulikuwa mbaya au hujui kuwa kuna mchele hauivi kabisa kutokana na mbegu yake je nalo linaweza kuwa kosa la mpishi?
 
Labda namm niongezee hapo hapo kwa uelewa wangu mdogo, Mungu alitaka watu au malaika wamtii, wampende, wamfuate kwa hiari yao kiasi fulani na ku appreciate ukuu wake japo alikuwa na uwezo au ana uwezo wa kutuendesha kama robots.

Lakini jaribu kufikiri angekuwa na ufahari gani kuongoza au kuwa na kundi la watu wanaofanya vitu kama robots bila mapenzi yao?

Ni kama wewe Leo uwe na mpenzi anayekupenda kwa moyo wake na anayekupenda kwa madawa utaona utofauti.

So kwa kumalizia mi naona Mungu aliacha hayo mapungufu ili mwisho tujidhihirishie wenyewe bila yeye kutuma nguvu kuwa yeye ni mkuu,Alpha na Omega.
Ukishasikia "Mungu alitaka" ujue huyo si Mungu.

Ujue huyo ni character katika hadithi ya watu, ndiyo maana wamempa mpaka tabia ya kutaka, ambayo ni tabia ya watu. Tabia ya ambao hawajajitosheleza.

Mungu, mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, hana matakwa yoyote, kajitosheleza kwa kila kitu.

Kutaka ni ishara ya kutokuwa mkamilifu, kutojitosheleza.

Unataka kula, kwa sababu una njaa, una tamaa ya chakula, hujajitosheleza, hujajikamilisha kwenye hilo jambo.

Kutaka ni tabia ya kutokukamilika, kutojitosheleza, Mungu aliyejikamilisha na kujitosheleza hana nafasi ya kutaka.

Sasa Mungu kama ni mkamilifu na kajitosheleza atatakaje?
 
Kwa hiyo turudi kule kule kwenye sayansi kuwa "In every action there is equal and opposite reaction" 🥱

Lakini mkuu kama Mungu ndiye alimfanya Lucifer kuwa shetani kwa nguvu zake mwenyewe basi kazi yake itakuwa haina maana.

Kwa sababu kwa muktadha wako wewe even now Mungu ndiye anae ku-control

Utende dhambi ama usitende,uende mbinguni ama jehanam, yaani kana kwamba sisi hatuna free will tena isipokuwa Mungu ndiye anakifsnyia wewe maamuzi kwa free will zake mwenyewe.

Kama nitakuwa nimekuelewa vizuri lakini.
Free will hakuumbiwa binadam ila ni laana au adhabu kwa binadamu kutokana na kuasi. Binadamu aliumbwa ayajue mema tu ila akaasi kwa kula tunda la mema na mabaya hivo Mungu kwa kuwa anajua binadamu ni dhaifu akamzuia kula tunda la uzima wa milele ili mwisho wa siku hichi kiumbe dhaifu kinachojua mema na mabaya kikijua kitaishi milele basi ujue hakuna jema litafanyika. So kifo na matatizo nd kinasababisha kwa asilimia kubwa watu wanasali pia. Lakini pia shetani hakufanywa na Mungu kama Hawa angekataa pale shetani angetupwa peke ake na asingewatempt watu tena na angachomwa moto tu ila tulimkubali so Mungu akamtumia kama jaribu letu.
 
Vyovyote vile. Lakini hatakiwi kumuadhibu mtu kisa makosa yake mwenyewe. Unamuumba mtu na nyege afu akifanya mapenzi Ni dhambi mpaka sijui ndoa. Hizi sheria Ni za makabila ya kale sio Sheria za muumba yote
Hiyo ni roho ya ulalamishi ni mbaya zaidi kuliko hata umasikini. Wewe hata ungeumbwa bila hizo tamaa za mwili ungehoji kwann hujaumbwa hivo. Jikane kwanza ukitaka kumuelewa Mungu sio undefine maisha yako unavojidesign na nd unamdesign Mungu wako hivo hivo.
 
SIna reference ya kwenye Biblia lakini tufanye tu mfano wa kibinadamu.

Kama Adam angeumbwa akiwa na option ya utii pekee bila kuwekewa option ya uovu pembeni basi huyo Adam angekuwa mkamilifu/timilifu sana.

Pia angekuwa hasinzii,hachoki,hahisi njaa n.k
Adam option ya uovu aliipata baada ya kuasi. Alikuwa hajui mabaya ila aliyatamani nd maan alipojaribiwa kidogo alikubali sababu alikuwa na shauku ya kuyajua hayo na Mungu akampa zawadi yake ambayo ikaja kuwa laan yake.
 
Waislamu wana sanamu za maumbo ya nyota na mwezi na wakrsto wana sanamu za watu na misalaba na wahindu pia wana sanamu na Wabudha pia wana sanamu.Na dini zetu za kiafrika kuna sanamu pia.
Ukristo gani una sanamu za kuchonga wakati biblia imekataza. Zungumzia system ya ukristo na njia zake usizungumzie eti kwa sababu katiba inasema kiongozi achaguliwe na wananchi halafu akatokea kiongozi akapindisha katiba kwa kulazimisha aongoze wananchi wewe uanze kusema katiba hii ni mbovu mbona fulani kafany hivi.
 
Ukishasikia "Mungu alitaka" ujue huyo si Mungu.

Ujue huyo ni character katika hadithi ya watu, ndiyo maana wamempa mpaka tabia ya kutaka, ambayo ni tabia ya watu.

Mungu, mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, hana matakwa yoyote, kajitosheleza kwa kila kitu.

Kutaka ni ishara ya kutokuwa mkamilifu, kutojitosheleza.

Unataka kula, kwa sababu una njaa, una tamaa ya chakula, hujajitosheleza, hujajikamilisha kwenye hilo jambo.

Kutaka ni tabia ya kutokukamilika, kutojitosheleza, Mungu aliyejikamilisha na kujitosheleza hana nafasi ya kutaka.

Sasa Mungu kama ni mkamilifu na kajitosheleza atatakaje?
Hicho ni kiswahili tu ila Mungu aliamuru kwa alivoona yeye yafaa.
 
Unajua unasema hivi katika karne ya 21 kwa sababu ya Sayansi na technology. Watu wakale waliamini kwamba miungu(mizimu ya mababu) ilikuwa inaisha kwenye mapango. Baadae wagiriki wakaja na Zeus ambae yupo juu ya mlima Olympus. Baadae wayahudi wakaja na Mungu aliyejuu mawinguni. Na saa hivi hayupo katika ulimwengu. Hii inaonyesha kwamba hizi dini zimetengenezwa kuwa na Mungu ambae haonekani na hawezi kuwa proven. Tumeambiwa yupo kila mahali at the same time hayupo ulimwenguni.. hahaha hizi dini zinajitahidi kumficha Mungu na kuwatishia watu Moto ambao haupo na watu wanaamini
kwanini unampangia Mungu jinsi ya kumjua kwa njia zako za kipagani wewe ni nani kwake au unaweza mpa faida gani zaidi ya kumjazia tu dunia mpaka akushobokee ushaambiwa unataka kumuona utamuona kwa terms zake acha dhambi uzinzi na uasherati usengenyaji na matusi acha tamaa za mwili usiabudu miungu mingine waheshimu wazazi wako na umkubali kuwa yeye ni muumba wa mbingu na nchi ujinyenyekeze kwake then utamjua. Mungu hajidhihirishi kwa terms za wanadamu hata siku moja ni kwa anavoona yeye. Yani unataka Mungu akufuate bar nd uamini yupo sasa kungekuwa na maan gani ya watu kuacha dhambi ili wamuone Mungu.
 
Hicho ni kiswahili tu ila Mungu aliamuru kwa alivoona yeye yafaa.
Hayo ni maneno tu, ndiyo maana huwezi hata kuthibitisha kwamba huyo Mungu yupo, achilia mbali kutiobitisha aliamuru chochote.

Ukibisha, thibitisha huyo Mungu yupo.
 
Back
Top Bottom