Step_Rocker
Senior Member
- Aug 31, 2021
- 197
- 323
Uwepo wa mambo wa ya ajabu ambayo yanakosa maelezo ndio chanzo cha mwanadamu kufikiri uwepo wa nguvu kubwa kuliko yeye ulipoanza.By the way dini inaweza isiwe suala la kubwa kwangu.
Lakini ni kwamba, nikisoma nadharia zingine hasa sayansi ya AUSTRONOMY inanifanya mimi kwa mawazo yangu mwenyewe ni conclude tu kusema Mungu yupo.
Mfano : katika sayansi ya anga za juu (Austronomy) ni kwamba kila kitu kilichoko angani kinazunguka (every object in the universe is moving or is in motion).
Ni kama na maana kwamba Dunia inazunguka,Mwezi unazunguka,Sayari zote zinazunguka,Jua linazunguka,Galaxy (mkusanyiko wa nyota) zinazunguka,Black holes zina zunguka n.k
Yaani kifupi ni kwamba hakuna kitu hata kimoja ambacho kimo hewani kimesimama wima tu hakizunguki,every object is in motion.
Lakini sasa kinachonishangaza, kwenye hii tasnia ni kwamba "ulimwengu unazunguka kwa kufata kanuni maalum".
Yaani unavyoviona angani vyote vinazunguka kwa kufata system/formula ama mfumo maalum na ndiyo maana huoni vikigongana hovyo wakati ukiangalia ni kama viko shaghala paghala (bila mpangailio).
Isingekuwa hivi vitu viko kwenye mfumo maalum basi dunia yetu hii ingeshagogwa na vitu vingine vikubwa sana angani na ingeshasambaratika muda tu.
Coz kwenye anga kuna vitu vikubwa sana ambavyo ukifananisha na Dunia, Dunia itaonekana kama kipande cha kokoto tu.
Hivyo basi, universe kuwa katika mpangalio maalum na kufata kanuni , ndiyo kunanifanya nipate wazo kuwa "Lazima kutakuwa na fundi aliyedizaini hivi vitu na kuviongoza (kama remote controller).
Trust me huu ulimwengu usingekuwa na fundi maalum wa kuungoza basi vitu angani vingekuwa vinagongana kila dakika hata dunia sasahivi isingekuwepo ingeshafanywa kifusi mda.
Sasa huyo fundi ndiye nimekuja kudhani kwamba ndiyo atakuwa huyo Mungu anaesemwa kwenye vitabu vya dini.
Lakini sasa nimeenda na kwenye vitabu vya dini, sifa anazopewa nikilinganisha na matukio ya baadhi ya vitu humo humo kwenye vitabu vya dini, naona kabisa vinakosa ushirikiano/haviendani.
Nimeamua nikupe mfano mmoja tu wa AUSTRONOMY, ila ukitaka mwingine pia nitakupa
Na naona kabisa kwenye kutafuta ama kutaka ushirikiano na nguvu hio kubwa kila mmoja alipata experience yake kama nilivosema awali.
Sasa hapo utaona kutokua na uwezo wa kueleza matukio ya aina fulani watu hao wakakabidhisha uwezo huo kwa kitu kingine Tunaita MuNGu na wakaanza kuhalalisha mambo mengine humo ndani, ambayo hayana uhusiano na uwezo wa mungu kuumba na kufanya mambo makubwa.
Mfano; unaweza kuta kundi fulani la watu wanawachukia watu fulani kwa sababu zai binafsi tu ili waeneze hio chuki kwa watu wengine watasema, watu wenye tabia fulani ni chukizi kwa mungu muumba mbingu. Sasa chuki yako na uumbaji wa mungu wapi na wapi.
Kutoka 20:7 Inasema usilitaje jina la bwana mungu wako bure.
Ukisoma biblia tafsiri ya KJV inasema
"You shall not take the name of the LORD your GOD in vain"
Biblia tafsiri ya J.B ROTHERHAM
"Thou shall not utter the name of the yahweh your GOD for falsehood"
Akimaanisha usitumie jina la mungu kuhalalisha mambo yako ya kipimbavu.
Ukiangalia history biblia ni mkusanyiko wa vitabu mbalimbali ambavyo watu fulani waliona mafundisho yake yanafanana fanana ama lengo la waandishi hao tofauti tofauti ni kama lilikua moja.
Ndio maana unakuta kuna matoleo mbalimbali ya biblia na yote waandaaji watakuambia waliongozwa na roho mtakatifu ili kukusanya vitabu hivyo.
Na je kama roho ni mmoja mbona awaongoze makusanyo yalio tofauti?, mbona waprotestanti wawe na vitabu kiasi fulani kwa biblia zao, mbona mayaudi wa kanisa la orthodox maybe wakubali mafundisho ya vitabu mfano vitabu vya enoch lakini waprotestant waseme vitabu hivyo havijavuviwa na roho mtakatifu, ni roho mtakatifu gani aliwavuvia waorthodox.
Ukiangalia fact kwa umakini hapo utakuta kuna interest za watu kwenye kuupata ukweli ndio maana ukweli halisi huwezi upata kwenye hivyo vitabu zaidi ya kuongeza maarifa juu ya mambo fulani tu.
Hata kristo alitoa onyo juu ya maandiko
Yohana 5:39-40....
Maandiko pekee hayatoshi bali kumtazama yeye kuutazama ukweli, ukweli ndio utatuweka huru. Na tukubaliane labda tungekua na toleo la kwanza la biblia huenda tungefahamu uhalisia wa mambo yalivyo lakini kwa hii tuliyonayo sasa imechezewa sana, kuna interest ya makundi ya watu fulani sana na wamehalalisha mambo kwa mgongo wa MUNGU.
Nimeegamia upande wa biblia sina ufahamu sana kwenye quran. Tuna mengi ya kujifunza sana mkuu.
Na kuegamia sana vitabu vya dini kujifunza ukweli ni kuishia kua mfia dini.