Naamini Mungu yupo ila nashindwa kuuelewa ukamilifu wake, labda muendelee kunifunza

Naamini Mungu yupo ila nashindwa kuuelewa ukamilifu wake, labda muendelee kunifunza

Huwezi kuumba viumbe usitake wawe robots but wasipokuwa robots unakasirika. Huu Ni ukichaa. Ukimpa mtu maamuzi mpe, na mbona nchi zilizoendelea ambazo hazishikilii dini Zina amani kuliko nchi za dini. Ina maanisha hauhitaji kitabu kikuambie usiuwe, we mwenyewe unaakili ya kujua kwamba kumtoa maisha mwenzako Ni kosa. Lakini akili hio hio kwa sababu ya dini ndo inafanya mtu kujilipua na kuuwa watu, kupiga watu mawe na kuangusha watu magorofani. Sasa kosa Ni Nini hapa dini au akili ya binadamu.
Kasome vizuri vitabu vya dini uelewe.
 
Kwani kila mbantu anasali? Mbona hatumsikii huyo mbakaso. Waafrica wamepotea sababu ya ulevi wa kupindukia bangi uzinzi kujifanya wajuaji ufisadi tamaa na ushirikina tu.
Yeah kila mbantu anasali mkuu kikabila....WAKOLONI WA KIZUNGU NA KIARABU NDIO WANAKUDANGANYA KUA WAAFRIKA WAMEPOTEA....NIKUULIZE SWALI DOGO......KWAHIYO WAO HIZO JAMII WALIOLETA DINI ZA KIGENI HAWANA TABIA HIZO????
 
Yeah kila mbantu anasali mkuu kikabila....WAKOLONI WA KIZUNGU NA KIARABU NDIO WANAKUDANGANYA KUA WAAFRIKA WAMEPOTEA....NIKUULIZE SWALI DOGO......KWAHIYO WAO HIZO JAMII WALIOLETA DINI ZA KIGENI HAWANA TABIA HIZO????
usichanganye wakoloni waliotumia mwanya wa dini na dini tuanzie hapo kwanza. Ukiniuliza kuhusu manabii na mitume kuhusu kutenda hayo biblia inaonesha hawakuyapendelea na kama waliteleza walikuwa wanyenyekevu wa kutubu. Haya leo hii unataka tushike dini kama za wale fisi wamekufa na irizi mkiani.
 
Wakati Mungu ana muumba mwanadamu, Hakujua kwamba ipo siku mwanadamu atamuasi na kufanya mabaya?

Kama alijua uasi utakuja kutokea kwa nini alisubiri hadi utokee asi uzuie tangu mwanzo??
Ndiyo alijua na ndo maan hukumu ya kwanza na ukombozi uko kwenye kitabu cha mwanzo kabisa. Yani kama angeamua angefuta uumbaji lakini alishaona kuna wanadamu watakao survive na uwepo wa huo huo ubaya so aliona hakuna aja ya kuwipe out his entire creation. Na pia alitoa msamaha na nd maan tumeishi hadi tatizo shetani katufunga tunaona hadi kuishi sio zawadi nzuri zaidi.
 
ni either teacher alitoa mtihani mgumu ambao wenye uwezo mdogo hawawezi japo kuna maswali mengine angeyaleta au mwalimu hajui kufundisha ndio maana sio wote walioelewa


Nb: mimi sijaongelea mitihani mungu aliyotupa mimi naongelea kutuumba sisi bila uwezo ya kufaulu mitihani yake na mbaya zaidi anajua hata kabla hataumba na bado anakuumba ili uje ukosee tu
Wewe nd unatakiwa uprove kuwa nimetenda mema umenionea siyo Mungu nd approve kwamba kwann umeadhibiwa.Yani dini ni hukumu yetu ndugu. Sasa kwanza kwan wewe unajua kuwa utaenda motoni hata kama Mungu yye anajua?
 
Mimi vitu vingi navyoongea hapa ni kutokana na uelewa wangu binafsi sija quote maandiko ya dini japo yamenisaidia kuwa na uelewa huu nilionao.

Kuhusu adhabu hata mimi kuna muda huwa najiuliza kwanini Mungu ahangaike kuumba kitu ambacho kina mapungufu alafu aje akiteketeze. Lakini pia pengine maandiko sio makamilifu kutokana yaliandikwa na mwanadamu.

So kuna muda naona kufuata nafsi yako kunasadia ndio maana kuna msemo unasema matendo mema ndio dini ya kweli.
Ndugu adhabu ipo tena kali sana na alieandika ni Mungu mwenyewe. Ibrahim ni mwanadamu kaishi kitakatifu mpaka kwa akina Paul Yohana wameishi hivo em fikiria Yesu aliutwaa udhaifu wetu na bado aliishi kwa mfano wa jinsi ya kutoboa. Mambo tunayoyajaza moyoni nd yanayochangia sana kuona kama kutii amri za Mungu ni ngumu. Lakini kama umeweza itii serikali kwa kutoua kwa kuogopa adhabu au jela basi ni rahisi pia kutotenda dhambi nyingine. Kikubwa kuwa mnyenyekevu kwa Mungu akujaze roho mtakatifu nae atakuongoza hutoishi maisha ya dhambi tena na utaepuka adhabu ya kifo ameen
 
Dini inakupa majibu. We mwafrika si alijua mbingu Ni mawinguni According to bible. Haya mzungu kaenda mwezini. That's just one example out of all, wazungu wanaweka dini pembeni kwamba kila kitu kinawezekana na majibu yanapatikana kwa utafiti sio maneno ya watu wa zamani.
Wewe muafrica kwann kabla ya kuja hyo dini usiwe na technlogy yako. Halafu hizo story za mwezini mbona nyingi tu ni za kutunga. Halafu alokwambia mbingu ipo hapo unapohisi wewe ni nani? Mungu anaishi nje ya upeo wa wanadamu. Wewe mwafrica sayansi nd kifo chako cha kwanza umepew smartphone ya kubishana jamii forums.
 
Nchi nyingi za Ulaya na marekani Zina population kubwa ambao haiamini dini, na wanasayansi wengi hawaamini dini na ndo wameleta maendeleo. Fuatilia sawa
Makao makuu ya makanisa karibu yote yapo huko ulaya sasa unasemaje kuwa huko hawasali tatizo unaangalia media zinachotaka kukuaminisha. Unaona kuwa kwenye dini ndo ela inapotea mwafrica bana nd maan tunasema kilichotufelisha sio dini. Mwafrica anatumia bando zaid ya ef 5 kila siku kushinda tik tok na insta ila akitoa sadaka ya ef 10 jumapili eti dini ina mfirisi Mwafrica anaenda kukesha bar anaacha laki 1 ila akitoa ef 10 kanisani anasema dini inamfirisi . Mwafrica anavaa kiatu cha 75 tishirt 35 suruali 30 ila anaona kununua suruali ya kitambaa ya ef 15 kiatu 25 shati 10 na kutoa sadaka ya 10 dini inamfirisi. Mwafrica anaona kutoa 50k kumlipa mwanamke guest 25k vinywaji 30k usafiri 20k hafirisiki ila kutoa 10k kanisani anaona anafirisika. Ingia kanisani moja ya sehem ambazo zina watu wana standard life ni watu wa makanisani. Kwenye kundi la watu wasiosali kuna walevi wale wa vilabu vya pombe kaangalie lifestyle lao kakompee na watu wa church nenda kaangalie life la watumia madawa ya kulevya wanasaidiwa na makanisa hawa. Unazungumzia tu kinachoingia kanisani ila hujui watu namba moja baad ya serikali kutoa misaada kwenye vituo vya wahitaji ni makanisa hayo hayo.
 
Nieleze kwa Nini uzinzi Ni kosa? Kwa akili isiyo ya dini.. niambie why.
Ni kosa kwa sababu matokeo yake kwa asilimia kubwa ni mabaya. Uzinzi na ndoa kipi kimezalisha watoto wa mitaani wengi zaidi? Kipi kimezalisha masingle moms wengi zaidi? Kipi kimezalisha magonjwa mengi zaidi ya zinaa?
 
Afu we sijui unaongea nini kwa hiyo dunia nzima isipokuwa pango la Muhammad ilikuwa bar au sio. Afu unakamia tamaa za kimwili..sio tamaa Ni natural mechanisms za evolution ambazo wanyama wote wanazo. Kwa Nini Ni kosa mi kutimiza haja zangu za kimwili. We ukiwa na njaa si unatamani kula. Mbona huachi kukidhi hio tamaa ya mwili.
Chakula kina madhara gani? Na je kila mtu akitumia tamaa za mwili unajua madhara yake?
 
Dogo soma Biblia yako sawa. The four corners of the earth resting in pillars. Haya dunia ipo hivyo au. Mambo ya fungu la kumi si wizi huo. Slave obey ur masters as u obey Jesus Christ. Skia ingia Google tafuta verses condoning slavery utaziona zipo kote la kale na jipya sawa. Wakristo hamsomi Biblia yenu unaongea tu.
Uwe unasoma bible kujua ilikuwa inazungumzia kitu gani. Sasa hujui kuwa waliokuwa wafalme enzi hizo walikuwa wapagani au. Yesu wapi amewahi chukua watumwa kwa kuwatesa na kuwanyanyasa. Mbona wewe leo hii uko chini ya raisi na unamtii je hyo inaamanisha kuwa raisi akiamua akunyanyase inakuwa urais ni kitu kibaya? Halafu pia ukiwa mtumwa ukiwabishia mamaster mwisho wa siku ni kifo kitu ambacho ungetumia amani kisingetokea. Mbona Mandela aliwasamehe wazungu na kuongea kiamani na wakaondoka south kwahyo lazima ujifunze kuishi na mazingira. Mbona hyo sayansi inataka kuwaobey walimu wetu.
 
Ni sawa na mi nakuambia nitakubaka usiponipa hela na we unatoa hela na unasema kakuokoa kutoka kwenye kibako. Siwezi weka maisha yangu kwenye control tactics za watu wa zamani wasioijua dunia.
Wewe unawaza dhambi nd maan umetolea huo mfano. Kwani ukimkosea mzazi wako akakususa na kukuambia usipoomba msamaha usikanyage nyumbani utamlaumu mzazi hapo?
 
Hahahahah! Kulingana na maneno yako unaonyesha dhahiri kuwa mungu kuna watu wake huwa anawachagua mapema tu ndio maana wengine anawapa neema then wengine anawazidisha maovu ili wapotee mazima ili baadae aje awaadhibu wakati uovu aliwawekea mwenyewe tena makusudi.

Halafu unavyoiona dini ni kitu kizuri yaani ni zawadi ya mungu kwa wanadamu kana kwamba tusiosali sio wa mungu na unasahau kuwa dini hizi zimefika africa karne ya 18. Je waliokuwepo hapo kabla wasiojua hizo dini mungu atawafanyaje??

Ila any way naamini mungu wa kwenye hivyo vitabu vya dini sio muumba wa ulimwengu.
Biblia inasema kutojua sheria za Mungu sio kosa hivo waafrica wa mwanzo wasiokuwa na uelewa hawana hukumu maan dini nd hukumu yenyew kwahyo kama mtu hakuwa nayo basi hawez hukumiwa. Mtu anawezaje kwenda jela bila katiba? Lakini sio waafrica wote hawakujua dini ndugu kuna washiha wa ethiopia kuna wamisri hawa wametajwa vizuri tu kwenye bible haya maziwa makuu ya victoria tanganyika nyasa yametajwa vizuri tu hivo wapo wengi tu waliokuwa wanajua dini ya kweli. Ndiyo anawachagua ila hakuna ajuaje siri so huwezi ukaanza kujihisi kuwa labda ujachaguliwa nd uanze kutenda maovu.
 
Wewe story ya Babel Ni ya uongo soma historia ya Babylon vizuri ndo utaelewa. Na kuchanganya lugha sio sababu kwa maana hata Burj khalifa imejengwa na watu tofauti wa nchi na lugha mbalimbali na Ni refu kuliko Hilo Babel na watu wametengeneza ndege, rockets zinaenda mpaka pluto. Haya Kama Mungu yupo mawinguni mbona hakuchanganya lugha za Hawa watu wa sayansi na ujenzi wa maghorofa marefu duniani.
Wewe Mungu anatenda kwa mapenzi yake usifikiri mawazo yako nd atayafuata kama aliamua awachanganye wale wa kipindi kile sio lazima wa sahv awachanganye unampangiaje. Halafu Yesu ametoa hukumu mpya hivo sahv wanadamu wamepewa uhuru wa kufanya unavotaka. Halafu eti wamejenga watu wa lugha mbali mbali unadhani kwann kuna michoro kwenye engineering ujue kuna umuhimu wa kuzungumza lugha moja nd maan hata iandikwe kwa lugha gani pi=3.14. Halafu hao unaowaamini wenyewe tu wanakinzana kuhusu hata hayo mambo ya anga. Story ya mwezini ina ukakasi gravity yenyew ina ukakasi au hujui kwann ipo relativity theory na ina maelezo tofauti na hayo ya sijui nini kinazunguka nn. Kama babel hutak nambie kuhusu kilo 2500 juu ya pyramidi zilifikaje eneo la tukio kwanza kutokea mjini maan halikutengenezwa pale na je juu lilipandaje kwann linapoint exactly kwenye same direction na centre of the earth na pyramid za mexico pia. Dini ingeandika kila kitu kitabu kisingetosha hivo vimeandikwa vitu vya msingi ili uache dhambi. Wewe unaleta strory za space hujui siku hizi wanasema space ni kama kitambaa fulani kwahyo vitu vinazungukwa kuteleza yani assume kama uzungushe golori kwenye kitambaa hivi.
 
Lakini saa hivi hauabudu milima na mito kwa sababu unaelimu ya juu vinavyofunction. Elimu na internet ndo inafanya dini ionekane haina maana kwa sababu majibu ya watu wa kale sio ya sahihi na wanasayansi wamegundua vitu vingi kwa sababu wameamua kuutafuta ukweli na sio kuogopa zawadi na adhabu za kufikirika.
Wewe unapotosha hapa. Mbona wayahudi wengi nd wagunduzi wakuu wa dunia na nd watu wa kwanza kuwa na dini hyo unayoponda.
 
Kasome vizuri vitabu vya dini uelewe.
Vitabu vya dini vinaeleza kwann nchi zilizoshika dini ndio hazina amani zaid?
Chukulia mfano Japan, ni nchi ambayo kwa asilimia kubwa haina dini. Ila ndio miongoni mwa nchi zenye amani zaidi...
 
Ndugu adhabu ipo tena kali sana na alieandika ni Mungu mwenyewe. Ibrahim ni mwanadamu kaishi kitakatifu mpaka kwa akina Paul Yohana wameishi hivo em fikiria Yesu aliutwaa udhaifu wetu na bado aliishi kwa mfano wa jinsi ya kutoboa. Mambo tunayoyajaza moyoni nd yanayochangia sana kuona kama kutii amri za Mungu ni ngumu. Lakini kama umeweza itii serikali kwa kutoua kwa kuogopa adhabu au jela basi ni rahisi pia kutotenda dhambi nyingine. Kikubwa kuwa mnyenyekevu kwa Mungu akujaze roho mtakatifu nae atakuongoza hutoishi maisha ya dhambi tena na utaepuka adhabu ya kifo ameen
Amina mtumishi, lakini pia tunaokolewa kwa Neema sio kwa nguvu, akili wala uwezo wetu.
 
W
usichanganye wakoloni waliotumia mwanya wa dini na dini tuanzie hapo kwanza. Ukiniuliza kuhusu manabii na mitume kuhusu kutenda hayo biblia inaonesha hawakuyapendelea na kama waliteleza walikuwa wanyenyekevu wa kutubu. Haya leo hii unataka tushike dini kama za wale fisi wamekufa na irizi mkiani.
Wewe umejuaje kuhusu hao manabii na mitume??????? Si wakoloni ndio walikuletea vitabu vyenye adithi zao????????? Huna uhakika gani na hizo simulizi mkuu???
 
Back
Top Bottom